Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-17 21:55:44    
Mapango ya mawe ya Longmen

cri

Wasikilizaji wapendwa, leo tunawaongoza kwenda katika Mji wa Luoyang kutembelea Mapango ya mawe ya Longmen na kutazama maua ya peony.

Mji wa Luoyang ni mji wa kale ulioko katikati ya mkoa wa Henan, China, mji huo ni moja kati ya sehemu za machimbuko ya ustaarabu wa taifa la China. Mji huo una vivutio vyake viwili maarufu yaani Mapango ya mawe ya Longmen yenye historia ya miaka 1500 na maua ya peony yanayochanua vizuri mjini humo.

Mapango ya mawe ya Longmen yapo umbali wa kilomita 13 kutoka kusini mwa mji wa Luoyang, katika sehemu hiyo, milima miwili ya mashariki na magharibi inakabiliana na kati ya milima hiyo kuna Mto Yi unaotiririka, mandhari ya sehemu hiyo ni nzuri sana. Kwa kuwa sehemu hiyo ilikabiliana na mlango wa kasri ya ufalme, na wafalme wa China zamani walisifiwa kuwa ni dragon, hivyo sehemu hiyo ilipewa jina la Longmen, maana yake kwa kichina ni mlango wa dragon. Kwenye miamba ya milima hiyo miwili toka mashariki hadi magharibi yenye urefu wa kilomita moja, kuna mapango ya mawe zaidi ya 2300 yaliyochongwa moja baada ya lingine katika zama za kale za China, ambapo kwenye mapang hayo, mafundi wa uchongaji wa mawe wa China katika zama za kale walichonga sanamu za Budhaa zaidi ya laki moja, watalii waliofika katika mapango hayo wote wanaweza kuuliza, je, ni nani waliochonga sanamu hizo ndani ya mapango, na kwa nini?

Mwishoni mwa karne ya 5, mfalme wa Enzi ya Wei ya kaskazini ya China aliamini dini ya kibudha, ilisemekana kuwa, watu waliochonga sanamu nyingi za Budha, walijaliwa zaidi kutoka kwa Budhaa, hivyo mfalme wa Enzi ya Wei ya kaskazini aliamua kutoboa mapango na kuchonga sanamu za Budha ndani yake. Aidha, mawe ya sehemu ya Longmen ni yenye sifa nzuri, ambayo yanafaa kutoboa mapango na kuchonga sanamu.

Mapango ya mawe ya Longmeng yalijengwa vizuri kwa zaidi ya miaka 400 ambayo yalipita Enzi ya Wei ya kaskazini na Enzi ya Tang, enzi hizo mbili zilikuwa enzi zenye ustawi zaidi katika China ya kale. Zaidi ya asilimia 90 ya mapango ya mawe yaliyohifadhiwa sasa katika sehemu ya Longmeng yalijengwa katika zama za enzi hizo mbili.

Mfanyakazi wa Mapango ya mawe ya Longmeng Bi.Yang Ting alisema, kutokana na mapango yaliyotobolewa kwenye zama za enzi hizo mbili, watu wanaweza kuona mitindo tofauti ya uchongaji wa sanamu za Budhaa wa enzi hizo mbili za Wei ya kaskazini na Tang. Alisema:

Pango la katikati lilijengwa katika zama za Enzi ya Wei ya kaskazini, ndani inaabudiwa sanamu ya Budha mkuu Sakyamuni, sura ya Budha mkuu Sakyamuni inaonekana ni nyembamba, shingo ya sanamu ni ndefu, hata sanamu yenyewe inaonekana ni yenye kimo kirefu kiasi, kwani katika enzi ya Wei ya kaskazini, wachongaji walipenda kuchonga sanamu yenye kimo kirefu, sura ya sanamu nyembamba iliwapendeza watu zaidi. Lakini kwenye mapango mawili ya upande wa kusini na wa kaskazini, sanamu za Budha huonekana ni sanamu zenye umbo mkubwa, kwani katika enzi ya Tang ya China ya kale, watu walipenda kuwa na unene.

Katika sehemu hiyo pia kuna pango moja linaloitwa Pango la Wanfo, jina Wanfo maana yake kwa kichina ni Budha elfu 10. Kwani kwenye kuta za pango hilo, zilichongwa sanamu ndogo za Budha elfu 15, sanamu ndogo zaidi ni yenye kimo cha sentimita 4 tu. Sanamu nyingi za namna hii za Budha zinazong'ara kwenye kuta za pango hilo zimeonesha hali ya kuwawezesha watu wawaabudu Budha.

Katika upande wa kusini wa Pango la Wanfo, kuna Hekalu la Fengxian ambalo ni hekalu maarufu sana katika sehemu ya Mapango ya mawe ya Longmen. Hekalu hilo ni kubwa sana, ndani ya hekalu hilo kuna sanamu moja ya Budha yenye urefu wa mita 17, sanamu hiyo ilichongwa vizuri, sura ya sanamu ya Budha inaonekana kama ni mtu hai, ambayo imesifiwa kuwa ni sanamu ya Budha yenye sura nzuri zaidi kuliko nyingine katika historia ya mapango ya mawe nchini China. Bi.Yang Ting alisema, macho ya tabasamu ya sanamu hiyo yanawavutia zaidi watu.

Watu walisema, katika mapango ya mawe ya Longmeng, hata ukiangalia kila sanamu ya Budha kwa nukta mbili, inakubidi kutumia siku tatu kwa kumaliza kuangalia sanamu zote za Budha. Mwaka 2000, mapango ya mawe ya Longmen yaliorodheshwa kuwa mali ya urithi wa utamaduni duniani. Profesa wa elimu ya utafiti wa mabaki ya kale wa Chuo kikuu cha Beijing Bwana Ma Shichang alisema, thamani kubwa ya mapango ya mawe ya Longmen si kama tu ni kutokana na ukubwa wake na sanaa ya uchongaji wa sanamu ndani ya mapango, bali ni kutokana na mapango hayo kuhifadhi ustaarabu uliotoweka wa kipindi kilichoanzia karne ya 5 hadi karne ya 10. Alisema:

Ndani ya mapango hayo kumehifadhiwa vitu vingi, ambapo hali ya historia, uchumi, sanaa na utamaduni inaonekana katika mabaki yote ndani ya mapango hayo. Kuorodheshwa kwa Mapango ya mawe ya Longmeng kweli kumethibitisha thamani yake halisi.

Wasikilizaji wapendwa, kila mwaka toka mwanzoni mwa mwezi Aprili hadi mwanzoni mwa mwezi Mei ni majira ya kuchanuka kwa maua ya peony, na kila ifikapo majira hayo, tamasha kubwa la maua ya peony hufanyika huko Luoyang mkoani Henan. Naibu meya wa mji Luoyang Bwana Guo Chonbin alisema, historia ya upandaji wa maua ya peony mjini Luoyang imekuwa ya zaidi ya miaka elfu moja, wakazi wa Luoyang wanaona fahari kutokana na maua ya peony yanayoonesha baraka na neema. Alisema:

Maua ya peony ya aina zote duniani yanapadwa mjini Luoyang, aina za maua ya peony mjini kwetu zimefikia zaidi ya 970, tena eneo la mashamba ya kupanda maua hayo ni kubwa sana mjini kwetu, hivyo watalii wanaokuja kwetu wanaweza kuvutiwa zaidi na maua ya peony ya rangi mbalimbali yanayochanua kote mjini.

Idhaa ya Kiswahili 2006-04-17