Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-18 20:33:07    
Tangazo 0418

cri

Tunapenda kutangaza matokeo ya mashindano ya chemsha bongo kuhusu "Taiwan, kisiwa cha hazina cha China" yaliyofanyika mwaka jana. Kutokana na uthibitishaji wa kamati ya uchaguzi ya Radio China kimataifa, mwaka jana wasikilizaji wetu hawakuweza kupata ushindi maalum, na orodha ya washindi wa nafasi maalum bado haijajulikana, lakini orodha ya majina ya wasikilizaji wetu waliopata nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu imeshajulikana.

Waliopata nafasi ya kwanza ni wawili, Bw. Ras Franz Manko Ngogo wa sanduku la posta 71, Mara, Tarime Tanzania na Bw. Mbarouk Msabah Mbarouk wa sanduku la posta 52483, Dubai U.A.E.

Waliopata nafasi ya pili ni wawili, Bw. Mogire O. Machuki wa sanduku la posta 646, Kisii Kenya na Bw. Mutanda Ayub Shariff wa sanduku la posta 172 Bungoma Kenya.

Waliopata nafasi ya tatu ni watatu?nao ni kama wafuatao: Bw. Stephen Magoye Kumalija wa sanduku la posta 1067, Kahama Shinyanga Tanzania, Bw. Noel E. Mashauri wa sanduku la posta 275 Singida Tanzania, na Bi. Mary Mkombozi wa sanduku la posta 1497 Tabora Tanzania.

Wasikilizaji wetu waliopata ushindi wa nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu, tutawatumia zawaidi kwa wakati. Ni matumaini yetu kuwa, wasikilizaji wetu wote wataendelea na juhudi kushiriki katika mashidano ya chemsha bongo yatakayoandaliwa siku za baadaye mwaka huu, kushiriki ni lengo, kweli si rahisi kuchaguliwa kuwa mshindi katika mashindano ya chemsha bongo. Kila mwaka Radio China kimataifa inaandaa mashindano hayo, na wasikilizaji wa Radio China kimataifa wa nchi mbalimbali duniani wanashiriki chemsha bongo hilo, Radio China kimataifa kila siku inatangaza kwa lugha 43, zikiwemo lugha 38 za nchi mbalimbali, kuwachagua washindi 10 hivi wanaopata nafasi maalum kutoka kwa maelfu ya wasikilizaji wetu walioshiriki mashindano ya chemsha bongo siyo kazi rahisi, kwa hivyo, tunatumai wasikilizaji wetu hamtakufa moyo, kama hamtaweza kuchaguliwa, kwani lengo kuu ni kushiriki, wasikilizaji wetu wengi wakishiriki katika mashindano hayo ya chemsha bongo, tukichapa kazi kwa juhudi, tunaona furaha, kwani kutokana na kushiriki mashindano ya chemsha bongo yanayoandaliwa na Radio China kimataifa, wasikilizaji wetu wengi wameijua China kwa mambo mengi zaidi kadiri siku zinavyoendelea, wasikilizaji wetu wakiweza kuijua China na kutuelewa, mawasiliano na maelewano kati ya China na nchi mbalimbali yataimarishwa siku hadi siku. Radio China kimataifa ni daraja la kuongeza urafiki na mawasiliano kati ya wananchi wa China na wa nchi mbalimbali duniani, tukiongeza maelewano na mawasiliano, tunaweza kusukuma mbele ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na nchi mbalimbali duniani.

Msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa sanduku la posta 1067 Kahama Shinyanga Tanzania anasema katika barua yake kuwa, wanatushukuru kuendelea kuwaletea habari muhimu na nyeti kutoka kote duniani. Anapenda kutumia fursa hii kwa kuipongeza serikali ya Jamhuri ya watu wa China , hususan wakuu wa serikali ya watu wa China kwa kutuma wahandisi wa mradi wa maji, ambao wameletwa nchini Tanzania, katika mikoa ya kanda ya ziwa Victoria katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

Anasema wahandisi hao ambao wanatoa maji kutoka ziwa Victoria wakati mkoa wa Mwanza na kupeleka katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida mpaka kwenye makao makuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko Dodoma. Wahandisi hao kwa kweli wanafanya kazi ya kurizisha sana, na nyenzo zao za kufanya ni za uhakika, wahandisi hao wa China ambao wanatoa maji ndani ya Ziwa Victoria kwa kutumia mabomba maalumu.

Na mitambo yao ya kusukuma maji itawekwa katika sehemu kama zifuatazo: Mkoa wa Mwanza, mtambo wao wa kwanza wa kusukuma maji utawekwa katika kijiji cha Ihelele Misungwi, mtambo huu ndio utakaokuwa mkubwa sana tena ndio mtambo mkubwa kabisa. Mitambo ni mingine itawekwa katika vijiji vifuatavyo: Kijiji cha Mwawile halafu pia Kijiji cha Mhalo, Mwamashimba, vijiji hivyo viko katika mkoa wa Mwanza na vilevile pia mitambo mingine itawekwa katika vijiji vifuatavyo: Kijiji cha Solwa, Katika kijiji cha Solwa mtambo wa maji utagawanywa mabomba mengine yatapeleka maji katika mji wa Kahama, Shinyanga na mabomba mengine yatapeleka moja kwa moja katika mji wa Shinyanga, na vilevile kutoka hapo mkoa wa Shinyanga, mabomba mengine yataenda katika mikoa ya Tabora, Singida mpaka Dodoma. Kwa kweli serikali ya Jamhuri ya watu wa China ninaipongeza sana kwa kuwajali wananchi wa Tanzania wanavyoteseka na uhaba wa maji.Joseph Miroro Ibacho village P O Box 81 40202, Keroka Kenya. Kwa watangazaji, Ninapokea vipindi vyenu kupitia idhaa yetu ya taifa KBC vizuri sana.

Anapenda kuwapa Salamu:

Mogire Machuki, Samuel Getenga, Dura Manani, Charles , Kerama, Samwel Ochwangi, Anthony Ragori, Charles , Monyimbo wakiwa Kisii.David Lutomia Peter Otuoma, Francis Kadenge, Kenyatta ,Lutomia Wakiwa Ruiru. Ras Frans Manko Ngogo, Onesmus Muponda, Mapema Ndura, Emmanuel Kapera, Paroko wa Paroko, George Mlele, Nasola Masiko wote wakiwa Tanzania. Ujumbe: Onesmus Mponda - Asante kwa salamu zako.

Idhaa ya Kiswahili 2006-04-18