Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-19 20:59:25    
Chuo kikuu cha Nairobi Kenya chaendeleza lugha ya kiswahili

cri

Mwandishi wetu wa habari aliyeko Nairobi Kenya hivi karibuni amefanya mahojiano na Bwana Abud Bashir Mchangamwe ambapo walizungumzia ukuaji wa lugha ya kiswahili nchini Kenya.

Bwana Abud Bashir hivi sasa anajishughulisha na uandishi wa vitabu vya lugha ya kiswahili katika kiwango cha shule za msingi, na hiyo ndiyo njia yake ya kujipatia riziki yake ya kila siku. Mwaka 1956 Bwana Bashir alikuwa mwalimu wa shule ya msingi, na baadaye mwaka 1957 alichaguliwa kuwa mwalimu mkuu katika shule ya Wanga, huko alifundisha hadi mwaka 1963, ambapo alijiunga na chuo kikuu cha Berminghan kwa kozi ya miezi 9 baada ya kupata udhamini wa masomo. Miezi hiyo 9 ilikuwa muhimu kwake ya kujifunza mambo ya idara za elimu, ambapo yeye na wenzake waliona tatizo la wanafunzi pengine watatu au wanne, ambao walioshindwa kusoma vitabu.

Anashukuru kuwa alipata pale chuo kikuu cha Nairobi kumwoeshea mtaala wa fasihi wa kidato cha 5 na kidato cha 6 kwa maana wizara ya elimu ya Kenya iliwaambia kuwa iko haja ya kuanzisha kiswahili katika kidato cha 5 na 6, kwa hiyo alipata pale walitayarisha mitaala.

Anasema, wanafanya juhudi za kutayarisha vitabu vya kufundisha lugha ya kiswahili, vilevile wanajaribu kuonesha njia ya kuikuza lugha ya kiswahili ili somo la kiswahili lifundishwe katika darasa la kidato cha 8. Na jambo kubwa lionalomsaidia kwa hakika ni pale rais wa kwanza wa Kenya hayati Jommo Kenyata alisema waziwazi mwaka 1978 kuwa kiswahili kitakuwa lugha ya taifa ya Kenya. Kauli hiyo ya hayati Kenyata iliwatia nguvu sana, na maendeleo ya kiswahili ya hivi sasa nchini Kenya yanafuata agizo hilo.

Mwandishi wetu wa habari alimwuliza, ilikuwaje na shughuli zake za kufundisha na kukuza kiswahili, Bwana Bashir alisema, kwa maana lugha ya kiswahili na lugha ya kiafrika, walitumia "silabi" kuliko neno mojamoja. Na zile silabi zinaambatana sana na sauti. Na ni rahisi wanafunzi kujifunza na kusoma lugha nyingine za kiafrika kwa kutumia lugha ya kiswahili. Ameona kuwa baada ya miezi mitatu tu, wanafunzi wanaweza kusoma kiswahili bila shida yoyote na ni rahisi kupiga hatua kutoka kusoma katika lugha ya kiswahili na kuingia katika kusoma lugha ya kiingereza. Bwana Bashir anatoa msaada huo kwa wanafunzi.

Mwaka 1977 Bwana Bashr alianza kujishughulisha na kuandika vitabu vya kiswahili, kufanya uchunguzi zaidi juu ya kufundisha kiswahili, na huo ni msingi mzuri wa kuandika vitabu vya kiswahili. Alisema, anapenda kuendelea na juhudi za kukuza lugha ya kiswahili nchini Kenya. Anafurahi kusikia vipindi vya Radio China kimataifa vikitangazwa kwenye wimbi la FM 91.9, anafurahia zaidi marafiki wa China kutangaza matangazo ya kiswahili na kuchapa kazi kwa ajili ya kuendeleza lugha ya kiswahili. Pia anashukuru kuhojiwa na mwandishi wetu wa habari na kupata nafasi ya kutoa maelezo yake juu ya maendeleo ya lugha ya kiswahili. Anaona pengine ni maelezo hayo ni madogo, lakini huo utakuwa ni mchango wake kwa wanafunzi vijana wanaojifunza kiswahili.

Idhaa ya Kiswahili 2006-04-19