Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-25 14:31:26    
Pande mbili za mlango wa bahari zakabili changamoto ya utandawazi wa uchumi kwa ushirikiano

cri

Mkutano wa siku mbili wa baraza la uchumi na biashara la pande mbili za mlango wa bahari wa Taiwan ulifungwa tarehe 15 hapa Beijing. Mkutano huo ulikuwa na mijadala kuhusu umuhimu wa maingiliano ya uchumi na biashara ya pande mbili juu ya uchumi wao, ushirikiano wa kilimo, usafirishaji wa ndege wa moja kwa moja, utalii na mambo ya fedha, na ulitoa mapendekezo ya pamoja kuhusu uimarishaji na uendelezaji wa maingiliano na ushirikiano wa uchumi kati yao. Kwenye mkutano huo China bara ilitangaza kanuni 15 za kisera za kuwanufaisha watu wa Taiwan. Washiriki wa mkutano huo walisema, kwa kukabiliwa na changamoto ya utandawazi wa uchumi, pande mbili za mlango wa bahari wa Taiwan zingeimarisha ushirikiano wa kunufaishana na kustawishwa kwa pamoja.

Utandawazi wa uchumi wa dunia na uanzishaji wa umoja wa uchumi wa kikanda ni mwelekeo wa maendeleo ya uchumi duniani, ambao unaleta nafasi na changamoto kubwa kwa umoja mkubwa wa kiuchumi mbalimbali duniani. Mwenyekiti wa heshima wa chama cha Guomindang Bw. Lian Zhan alipotoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa baraza la uchumi na biashara wa pande mbili, alisema, kwa kukabiliwa na hali ya namna hiyo, pande mbili za mlango wa bahari wa Taiwan zingenufaishana kwa hali yao bora ili kutimiza lengo la kunufaishana na kuwa na maendeleo kwa pamoja. Alieleza umuhimu wa ushirikiano wa pande mbili akichukua mfano wa sekta ya integrate circuit,

"Kutoka usanifu wa integrate circuit hadi uzalishaji wa bidhaa viwandani, China bara inajitahidi kufikia kiwango cha juu. Wakati, mfumo wa sekta ya uzalishaji ya Taiwan umekamilika na kukomaa katika eneo hilo. Lakini soko la Taiwan ni dogo, licha ya hayo, bado haijakuwa na bidhaa zake maarufu zinazojulikana duniani. Hivyo, ikiwa tunaweza kuunganisha uwezo wa uzalishaji, uuzaji, teknolojia na masoko ya sekta za integrate circuit za pande mbili za mlango wa bahari, basi itatoa nafasi kubwa kabisa ya biashara katika kpindi cha nusu ya mwanzo ya karne ya 21."

Toka miaka ya 60 ya karne ya 20, ongezeko la kasi la uchumi wa Taiwan lilidunishwa kwa miaka karibu 40, ambapo wastani wa ongezeko la pato ulifikia 9% kwa mwaka, ambapo Taiwan ilichukua nafasi ya kwanza miongoni mwa "Dragon wanne wadogo barani Asia". Lakini tangu chama cha Minjin kuchukua madara ya utawala mwaka 2000, utawala huo wa Taiwan unafuata siasa ya "kujitenga na China bara" ambayo inakwenda kinyume cha maoni ya watu wa pande mbili za mlango wa bahari, na uchumi wa Taiwan ulianza kuzorota kutokanana ukosefu wa mikakati mizuri ya kiuchumi, ambapo wastani wa ongezeko la uchumi ulishuka hadi 3% hivi kwa mwaka, tena idadi ya watu wanaokosa ajira inaongezeka mwaka hadi mwaka. Mshauri wa taasisi ya utafiti wa uchumi ya Zhonghua, Taiwan Bw. Ye Wanan alisema, katika hali ya namna hiyo, endapo Taiwan haitazidisha ushirikiano na China bara, basi itakabiliwa na hatari.

"Katika miaka 6 ya karibuni, pato la watu wa Taiwan halikuongezeka, hivyo matumizi ya fedha ya watu wa Taiwan hayakuongezeka pia, mahitaji ya ndani ya Taiwan hayakuwa makubwa, na ongezeko la uchumi linategemea mahitaji ya nje, hususan kutegemea kusafirisha bidhaa nyingi kwa China bara. Kutokana na utandawazi wa uchumi wa dunia, hususan baada ya kuanzishwa hatua kwa hatua umoja kati ya China bara na Umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki na umoja kati ya China, Japan na Korea ya Kusini, endapo Taiwan itatengwa nje, njia ya maendeleo ya Taiwan katika siku za baadaya itakabiliwa na hatari kubwa, hivyo inapaswa kuwa na ushirikiano na China bara.

Katika miaka ya karibuni, kwa kuhimizwa na China bara, biashara kati ya pande mbili za mlango wa bahari ilikuzwa kwa haraka. Mwaka 2005, thamani ya biashara ya nje ya Taiwan ilifikia dola za kimarekani bilioni 371, wakati thamani ya biashara na China bara ilifikia dola za kimarekani bilioni 91.2, ambapo thamani ya bishaa zilizosafirishwa na Taiwan kwa China bara ilizidi ile ya bidhaa ilizoagiza China bara kutoka Taiwan kwa dola za kimarekani bilioni 58.1. Lakini kutokana na vikwazo na vizuizi vya kisiasa vilivyowekwa na viongozi wa utawala wa Taiwan, mzunguko wa mitaji na uchukuzi wa mizigo kati ya pand hizo mbili vinaweza tu kufanyika kwa njia isiyo ya moja kwa moja, viwanda vya China bara haviruhusiwi kuwekeza katika kisiwa cha Taiwan, matatizo hayo bado hayajatatuliwa ipasavyo hadi hifi sasa.

Kuhusu masuala hayo, washiriki zaidi ya 400 kutoka pande hizo mbili walisema kwenye mkutano huo kuwa pande hizi mbili zinatakiwa kujadili namna ya kuunda mfumo tulivu wa ushirikiano wa uchumi, kuhimiza uhusiano wa uchumi wa pande mbili kuwa wa kawaida, kufuata mfano uliowekwa, kuwa wa utulivu na kuondolea mbali vikwazo vya aina mbalimbali vilivyowekwa katika uhusiano wa uchumi na biashara wa pande hizo mbili.

Hivi sasa tatizo moja kubwa zaidi katika ushirikiano wa uchumi na biashara wa pande mbili ni kutotimiza mawasiliano ya moja kwa moja, usafirishaji wa bidhaa na abiria unapaswa kupitia sehemu ya tatu. Utafiti uliofanywa na wataalamu wa Taiwan unaonesha kuwa endapo pande mbili za mlango wa bahari zinawaza kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja, kwa uchache kabisa gharama itapungua kwa fedha mpya za Taiwan Yuan bilioni 31 kwa mwaka, kiasi hicho ni kama dola za kimarekani bilioni 1. Hivyo katika mapendekezo ya mkutano wa baraza hilo, washiriki wa pande mbili walitaka kuhimiza watu wa sekta za kampuni za ndege za pande mbili kujadili masuala ya urahisishaji wa kukodi ndege za mizigo, kukodi ndege za abiria katika siku kuu na wikiendi pamoja na kufanya mawasiliano kuwa katika hali ya kawaida, tena kupanga mpango na kuutekeleza mapema iwezekanavyo. Wachambuzi wanaona kuwa mpango huo unaweza kuchukuliwa ni wa muda kabla ya kutimiza mawasiliano ya moja kwa moja kati ya pande mbili. Mbali na hayo, wataalamu husika walitoa mapendekezo yao kuhusu suala la mawasiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili. Bw. Zhang Guan wa idara ya utafiti wa mambo ya Taiwan ya taasisi ya sayansi ya jamii ya China alisema, kabla ya kutimiza mawasiliano ya moja kwa moja kati ya pande mbili, yatimizwe kwanza mawasiliano ya moja kwa moja kati ya baadhi ya miji ya pande hizo mbili.

"Tunaweza kutumia bandari na sehemu za biashara huria zilizoanzishwa na Taiwan katika baadhi ya bandari na viwanja vya ndege, China bara nayo inapanua au kuweka maeneo yenye uwezo unaolingana ili kutimiza mawasiliano ya moja kwa moja kati ya baadhi ya miji ya pande hizi mbili, ikiwemo miji mikubwa ya Beijing, Shanghaina Guangzhou ya China bara na miji ya Taibei, Taizhong na Gaoxiong ya Taiwan."

Baada ya kuendelezwa kwa miaka zaidi ya 20, viwanda vilivyowekezwa na Taiwan katika China bara vimebadilishwa kuwa vyenye teknolojia ya kisasa. Wakati huo huo, China bara inabadilisha mtindo wa ongezeko la uchumi wa taifa. Hivyo kuimarisha uwezo wa uvumbuzi na kuanzisha uchumi wa aina mpya vimekuwa nafasi mpya ya ushirikiano kati ya pande mbili za mlango wa bahari wa Taiwan.

Hivi karibuni, China iliweka mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii ya miaka 5 ijayo, katika mpango huo lengo la uchumi ni kufanya ongezeko la pato la taifa lifikie wastani wa 7.5%. maendeleo ya uchumi na jamii ya China bara yatanufaisha watu wa China bara, na pia yataleta nafasi kubwa ya biashara kwa watu wa Taiwan.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-25