Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-26 16:19:51    
China yazingatia uanzishaji wa elimu ya uzazi kwa vijana

cri

Hivi sasa nchini China idadi ya vijana wenye umri wa miaka ya kutoka 10 hadi 24 pamoja na vijana ambao hawajaoa, imefikia kiasi cha milioni 300, pamoja na maendeleo ya kasi ya jamii na uchumi wa China na kuinuka kwa kiwango cha maisha ya watu, vijana wanabalehe wakiwa na umri mdogo zaidi kuliko vijana wa zamani, lakini wanachelewa kuoa au kuolewa wakilinganishwa na vijana wa zamani. Hivi sasa yamejitokiza matatizo ya vijana kuwa na ngono ya mara ya kwanza wakiwa na umri mdogo na kuongezeka kwa vitendo vya ngono kabla ya kufunga ndoa.

Watu wa sekta mbalimbali za jamii ya China wanaona kuwa njia nzuri ya kutatua masuala hayo na kulinda afya za kimoyo na kimwili ya vijana ni kuimarisha elimu ya uzazi. Katika darasa ya shule moja, mwalimu alisema,

"Sasa ninawasimulieni habari tulizosikia wakati tulipojibu maswali ya wanafunzi wenye matatizo ya kimoyo, (lakini majina ya vijana si yao halisi bali ni ya kubuniwa). Huyu ni msichana Yueyue, mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya juu, katika shughuli za shule alifahamiana na mvulana mmoja wa kidato cha tatu. Mwanzoni kabisa maongezi yao yalikuwa kuhusu mambo ya shule yao au mambo kuhusu wanafunzi wenzao. Hapo baadaye karibu kila siku walitaka kutumiana ujumbe kwa simu za mkononi, au kuzungumza katika simu, hatimaye kila siku hawakosi kuwa pamoja wakati walipokwenda shuleni au kurudi nyumbani baada ya masomo. Lakini msichana Yueyue alikuwa na wasiwasi moyoni, hivyo siku moja alikwenda kumuliza mwalimu wa kisaikolojia, 'mwalimu uniambie hii ni kuonesha kuwa nimempenda?'

Wanafunzi wa darasani walicheka kwa sauti ndogo. Mwalimu alisema, kisha aliniuliza tena,'je, mwalimu tutaweza kupendana katika maisha yetu yote?' Mwalimu aliwauliza wanafunzi wa darasani, "Mnaona je, wataweza kupendana katika maisha yao yote? Wanafunzi walishindwa kumjibu mwalimu wao.

Hayo ni mazungumzo kati ya mwalimu na wanafunzi katika darasa la afya ya vijana katika shule ya sekondari ya 171 ya Beijing. Masomo ya elimu ya afya ya vijana yameanzishwa katika shule za miji midogo zaidi ya 10 pamoja na baadhi ya sehemu za vijiji za Beijing. Masomo hayo yalianzishwa kutokana na harakati za jumuiya ya uzazi wa mpango ya China, ambayo ni mambo muhimu ya elimu ya mambo kuhusu kujamiana na afya ya uzazi katika mradi unaojulikana kwa "Afya ya Vijana".

Hapo zamani, ufahamu waliopata vijana kuhusu elimu kimsingi ya afya ya vijana uliandikwa katika kitabu cha afya ya mwili kilichofundishwa katika darasa la afya shuleni, mtindo wa elimu ulikuwa rahisi, shule ilizingatia kufundisha ufahamu wa afya ya mwili na haikuzingatia uongozaji wa mambo ya hisia na kisaikolojia. Masomo ya afya ya vijana yamejaza pengo hilo, ni ya kisayansi zaidi na ni rahisi kupokelewa na wanafunzi.

Sasa tuchukue mfano wa darasa lile la sekondari ya 171. mambo muhimu ya darasa lile ni kuhusu namna ya kuingiliana kati ya wavulana na wasichana. Kwanza kabisa, mwalimu alisimulia hisia na mapenzi ya juujuu kati ya mwanafunzi mvulana na mwanafunzi msichana, kisha kuacha wanafunzi kujadiliana ili kuwasaidia wanafunzi kufahamu mambo ya kipindi cha kubalehe kutoka pande za mwili, kimoyo na kijamii, na kuwasaidia kufahamu njia ya kufanya maingiliano kati ya mvulana na msichana, kujua kuheshimu watu na kujidhibiti. Mwalimu pia aliwaambia wanafunzi kuwa mambo kuhusu kujamiana yatakuweko katika maisha yote ya binadamu, na kuwaambia ni busara kuchukua msimamo wa kisayansi na kwa uangalifu kuhusu suala hilo. Masomo ya "Afya ya Kipindi cha Kubalehe" yamependwa na wanafunzi.

Mwanafunzi Su Min mwenye umri wa miaka 16 ana hamu kubwa juu ya masomo hayo alisema:

Mwalimu ametueleza ipasavyo na kutuwezesha tutambue kuwa mawasiliano kati ya wasichana na wavulana ni ya kawaida, tumefurahia masomo hayo, kwenye darasa tunaweza kubadilishana vilivyo maoni yetu ya moyoni.

Hivi sasa masomo hayo yameanzishwa rasmi katika shule karibu 300 zilizoko katika sehemu mbalimbali nchini. Kwa mfano katika sekondari ya juu ya 54 ya Beijing, wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili, kila wiki wana darasa moja la somo la afya katika kipindi cha ujana. Wanafunzi wa sekondari hiyo wameanzisha wenyewe tovuti moja ili kuwawezesha wanafunzi wabadilishane maoni kuhusu masomo. Tovuti hiyo imewafurahisha wanafunzi, na walimu wao pia wanawaunga mkono. Mwalimu wao Bibi Chen Hong alisema, tovuti hiyo inaweza kuonesha maoni ya wanafunzi, uendeshaji wa tovuti hiyo unasaidiwa na shule. Alisema:

Baada ya kuhitimu masomo kwa wanafunzi wa awamu hii, wanafunzi wa awamu nyingine wataendelea kuendesha tovuti hiyo inayowasaidia wanafunzi wenyewe, ambapo wanafunzi wote wanaweza kushiriki kwenye kazi ya tovuti hiyo.

"Mradi wa Afya ya Vijana" unaotekelezwa na jumuiya ya uzazi wa mapngo ya China, licha ya kuanzisha masomo husika, pia zimeanzishwa harakati nyingi zinazoimarisha afya za vijana. Elimu ya kipindi cha kubalehe iliyoanzishwa na jumuiya ya uzazi wa mpango ya China itaendelezwa zaidi, jumuiya hiyo imeweka mpango wa kukuza kwa maradufu "Mradi wa Afya ya Vijana" katika miaka mitano ijayo.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-26