China na Afrika zote ni nchi zinazoendelea, ushirikiano kati ya China na Afrika unategemeana na ni wakunufaishana. China ina teknolojia nyingi zinazofaa kwa nchi za Afrika, uwekezaji wa makampuni ya China bila shaka utasaidia kustawisha uchumi wa nchi za Afrika. Nchi za Afrika zina rasilimali nyingi ambazo zinahitajiwa na China.
Nchi za Afrika na China zimekuwa marafiki makubwa, urafiki kati ya China na Afirka umeendelea kwa zaidi ya nusu karne, hasa baada ya kuanzishwa kwa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2000, uhusiano kati ya China na Afrika umeingia katika kipindi kipya cha maendeleo.
Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa Afrika ya taasisi ya uhusiano wa kimataifa ya China Bwana Xu Weizhong alisema, katika miaka ya karibuni, uhusiano wa kiuchumi kati ya China na nchi za Afrika umeingia kipindi kipya cha maendeleo ya pande zote. Thamani ya biashara ya pande mbili mbili kati ya China na nchi za Afrika imeongezeka kwa kasi, ambapo ongezeko lake katika miaka mitano iliyopita lilikuwa mara nne hivi kutoka dola za kimarekani bilioni 10.5 ya mwaka 2001 hadi dola za kimarekani bilioni 40 ya mwaka 2005. Na mwaka 2005, asilimia 30 ya mafuta ya China iliyoyaagiza kutoka nchi za nje yalitoka nchi za Afrika. Nchi za Afrika zimekuwa washirika wakubwa wa kiuchumi wa China.
Bwana Xu Weizhong aliongeza kuwa, ushirikiano kati ya China na Afrika ni wa kunufaishana, unatokana na mahitaji ya kila upande. Katika miaka ya karibuni, ili kuondoa hali ya kuwekwa kando katika utandawazi wa kiuchumi duniani, nchi nyingi za Afrika zimechukua sera ya kuelekea mashariki, zinatumaini kufanya ushirikiano na nchi za mashariki hasa China. China ikiwa nchi inayoendelea pia inahitaji kushirikiana na kuungana mkono na nchi za Afrika katika mambo ya kisiasa na kulinda maslahi ya pamoja, China inahitaji uungaji mkono wa nchi za Afrika katika suala la kupinga shughuli za kuitenga Taiwan ilitengana na China na kuunga mkono muungano wa amani wa taifa la China. Kwa upande mwingine, maendeleo ya uchumi wa China pia yanahitaji rasilimali kutoka nchi za Afrika.
Bwana Xu Weizhong alisema, hivi sasa, ushirikiano wa nishati umekuwa sekta muhimu ya ushirikiano kati ya China na Afrika, hivyo jambo muhimu la kufanya ni kuvumbua mtindo mpya wa ushirikiano wa nishati amabo si kama tu utafuatana na utaratibu wa soko huria na wa kunufaishana, bali pia utatofautiana na njia ya unyag'anyi ya nchi za magharibi katika uchimbaji wa maliasili.
Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa Asia magharibi na Afrika ya taasisi ya jamii na sayansi ya China Bwana Yang Guang alisema kuwa, katika miaka ya karibuni, kutokana na mahitaji ya kupambana kwa pamoja na ugaidi na kugombea rasilimali hasa mafuta ya Petrolia, bara la Afrika kwa mara nyingine limefuatiliwa sana na nchi za magharibi. Japokuwa kutokana na kuwa, baadhi ya nchi bado zinakabiliwa na msukosuko wa kisiasa, ambao umeathiri maendeleo ya uchumi, lakini Chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika, nchi za Afrika zinajitahidi kujiendeleza kisiasa na kiuchumi, na kupata mafanikio kadha wa kadha.
Ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika ni wa kunufaishana na wenye usawa, unakaribishwa na nchi za Afrika. Lakini hivi sasa baadhi ya makampuni ya China bado hayana matakwa ya kuwekeza katika nchi za Afrika, hivyo wanahitaji kufahamishwa hali halisi ya nchi za Afrika. Kwa upande mwingine serikali ya China inatakiwa kuyaunga mkono makampuni yatakayowekeza katika nchi za Afrika kwenye kiwango kikubwa zaidi katika utoaji wa mikopo nafuu.
Bwana Yang Guang alisema, kwa upande wa kiteknolojia, makampuni mengi ya China yanafaa kuwekeza katika nchi za Afrika na kuanzisha viwanda. Kwa mfano, teknolojia ya China ya kutengeneza televisheni na friji inahitajiwa sana na nchi za Afrika. Dawa za Cotecxin zilizotengenezwa na makampuni ya China zimethibitishwa na shirika la afya duniani kuwa dawa zenye sifa maalum ya kutibu ugonjwa wa maralia. Bara la Afrika si kama tu lina rasilimali nyingi, bali pia lina vivutio vingi vya utalii, na kuwahimiza wachina kutalii katika nchi za Afrika si kama tu kunaweza kuwafanya wachina wafahamu vizuri zaidi hali halisi ya nchi za Afrika, bali pia kunaweza kustawisha uchumi wa nchi za Afrika.
Idhaa ya kiswahili 2006-05-12
|