Waziri mkuu wa baraza la serikali ya China Bw. Wen Jiabao hivi karibuni alipofanya ukaguzi kwenye shamba la ufugaji ng'ombe la mji wa Chongqing alisema: "Nina tarajio moja la kumfanya kila mchina, kwanza kabisa ni watoto, apate nusu kilo ya maziwa kwa siku."
Kuhusu maneno hayo, ofisa wa wizara ya kilimo ya China tarehe 11 alisema, serikali ya China inachukua hatua nyingi kuhimiza maendeleo ya sekta ya maziwa na kutaka watu wengi wanywe maziwa na kuhimiza tarajio la waziri mkuu litimizwe mapema iwezekanavyo.
Naibu mkurugenzi wa idaya mifugo ya wizara ya kilimo Bw. Zhang Xiwu kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 11 alisema, wastani wa maziwa na chakula cha maziwa aliyokunywa kila mtu ulikuwa ni kilo 21.7 mwaka 2005, kiasi ambacho ni 20% hivi ya wastani wa maziwa aliyokunywa kila mtu duniani. Zaidi ya hayo, matumizi ya maziwa katika sehemu za nchini siyo ya kulingana, watu wengi wanaokunywa maziwa wako katika miji mikubwa na sehemu zilizoendelea kiuchumi, na wakazi wa sehemu za vijijini wanaokunywa maziwa ya ng'ombe ni wachache sana.
Hivi sasa katika baadhi ya nchi zilizoendelea katika sekta ya maziwa, kwa mfano nchini Marekani wastani kiasi cha maziwa anachokunywa kila mtu ni kilo 263,8 kwa mwaka, nchini Australia ni kilo 525.9, wastani wa maziwa anayokunywa kila mtu ni kilo 0.75 na kilo 1.45 kwa siku.
Takwimu iliyotolewa na wizara ya kilimo inaonesha kuwa jumla ya maziwa tani 2864 yalitolewa nchini China mwaka 2005, ambapo wastani wa maziwa aliyokunywa mkazi wa mjini ulikuwa kilo 24.8 kwa mwaka, wakati mkazi wa sehemu za vijijini ulikuwa ni kilo 2 kwa mwaka.
Bw. Zhang Xiwu alisema, utoaji maziwa ulikuwa theluthi moja tu ya jumla ya utoaji wa nyama nchini China mwaka 2005, ukilinganishwa na hali ya Ujerumani, utoaji maziwa ulikuwa mara 4 kuliko ule wa nyama, na mara 4.6 nchini Uholanzi. Katika nchi zilizoendelea utoaji maiwa huwa ni zaidi ya mara 2 kuliko utoaji nyama, hata katika siku ya leo ambapo utoaji maziwa umezidi tani milioni 77.43, nafasi ya maendeleo ya sekta ya maziwa bado ni kubwa sana.
Maziwa yang'omba ni chakula chenye lishe bora, ambayo yanaweza kuimarisha afya za watu. Nchi nyingi zaidi na zaidi zimehusisha kunywa maziwa ya ng'ombe na kuimarisha afya za umma. Nchi ya Japan ambayo iko katika bara la Asia sawasawa na China, katika miaka ya 60 hadi miaka ya 70 ya karne iliyopita iliitikia kwa vitendo halisi wito wa "kikombe kimoja cha maziwa kinaimarisha taifa moja", ambapo wastani wa urefu wa mtoto mwenye umri wa miaka 14 nchini Japan uliongezeka kwa sentimita 10, na uzito wa mwili uliongezeka kwa kilo 8. serikali ya India imeanzisha "mapinduzi ya rangi nyeupe", inajitahidi kuendeleza utoji wa maziwa ya ng'ombe, jumla ya utoaji maziwa umechukua nafasi ya kwanza duniani, na wastani wa maziwa anayokunywa kila mtu umeongezeka na kufikia kilo 90 kutoka kilo 38 kwa mwaka.
Bw. Zhang Xiwu alisema, hatua inayochukuliwa naChina hivi sasa ni kushawishi wananchi wanywe maziwa mengi zaidi, hivyo wakati wa kukuza sekta ya maziwa, inatakiwa kukuza kundi la watu wanaokunywa maziwa.
Serikali ya China imeweka mpango wa 11 wa maendeleo ya miaka 5 ya sekta ya maziwa na mpango wa muda mrefu wa mwaka 2020, na kuhimiza maendeleo ya sekta ya maziwa nchini China kutoka pande mbalimbali zikiwemo kuboresha ng'ombe wa maziwa, njia ya kulisha ng'ombe, kuendeleza viwanda vikubwa vya maziwa, kuongeza ubora wa chakula cha maziwa na kuimarisha hifadhi ya mazingira ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.
Katika wakati huo huo, serikali ya China inapoimarisha mazoea ya kula chakula cha maziwa kwa wananchi, inaeneza "mpango wa kunywa maziwa kwa wanafunzi". Hivi sasa mpango huo umetekelezwa katika shule za sekondari na za msingi 8,862 za jumla ya miji mikubwa na wastani 52, ambao unatoa maziwa kwa wanafunzi milioni 1.90.
Idhaa ya Kiswahili 2006-05-16
|