Kwenye mkutano mkuu wa bunge la umma la taifa la China wa mwaka huu, sehemu mpya ya Binhai ya mji wa Tianjin ulioko kwenye pwani ya kaskazini ya China ilichukuliwa na serikali kuwa wilaya ya inayowekwa kipaumbele katika maendeleo ya miaka 5 ijayo. Kutokana na mpango uliowekwa, sehemu mpya ya Binhai itaendelezwa kuwa sehemu ya uchumi la kisasa chenye kituo cha kisasa cha uzalishaji bidhaa, kituo cha kimataifa cha usafirishaji na usambazaji wa bidhaa pamoja na mazingira ya asili ya kupatana kwa viumbe. Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari alipoitembelea sehemu hiyo alifahamishwa kuwa kufuatilia maendeleo ya mwafaka kati ya uchumi na jamii pamoja na mazingira ya kimaumbile kumekuwa lengo muhimu la ujenzi wa sehemu mpya ya Binhai katika siku za baadaye.
Mji wa Tianjin ulikuwa na wazo la kujenga sehemu mpya ya Binhai mnamo miaka ya 90 ya karne iliyopita, eneo la ustawishaji la uchumi na teknolojia la Taida la mji wa Tianjin, likiwa moja ya maeneo muhimu ya sehemu mpya ya Binhai lilifungua mlango na kuendelezwa miaka 10 iliyopita. Hivi sasa nguvu ya jumla ya eneo la Taida, ambalo ni moja ya maeneo ya ustawishaji wa uchumi na teknolojia ya ngazi ya taifa, inachukua nafasi ya kwanza kwa miaka mingi mfululizo miongoni maeneo zaidi ya 50 ya ustawishaji ya ngazi ya taifa, hadi mwishoni mwa mwaka 2005, kampuni na viwanda vyenye mitaji ya kigeni vilivyoko kwenye eneo la ustawishaji vimezidi 4,000, na jumla ya mitaji iliyowekezwa imezidi dola za kimarekani bilioni 29.
Kampuni ya Motorola, ambayo ni maarufu sana duniani, ilijenga kiwanda cha simu za mkononi kwenye eneo la ustawishaji la Taida mwaka 1994, mkurugenzi wa ofisi ya uenezaji na shughuli za pamoja za kampuni ya Motorola Bw. Yang Boning alisema, hivi sasa, kiwanda cha simu za mkononi kilichoko kwenye eneo la Taida ni kituo cha kwanza kwa ukubwa cha uzalishaji wa simu za mkononi cha kampuni yaMotorola humu duniani, mbali na hayo, kampuni ya Motorola inaimarisha kwa mfululizo utfiti wa teknolojia kwenye kituo hicho.
"China ni moja ya sehemu muhimu sana ya kampuni ya Motorola duniani, China ni soko kubwa kabisa duniani. Simu zinazozalishwa kwenye kiwanda cha eneo la Taida licha ya kutosheleza mahitaji ya soko la China, zinasafirishwa katika nchi za nje. Aidha, kampuni ya motorola inasehemu mbili nchini China, ambazo moja ni ya uzalishaji, na nyingine ni ya utafiti. Miradi mingi ya utafiti siyo kwa ajili ya soko la China peke yake, bali ni kwa ajili ya masoko ya dunia nzima. Soft ware za simu zilizoagizwa na wafanyabiashara wa nchi za Ulaya na Marekani zilitokana na utafiti wa kituo chetu cha utafiti kilichoko kwenye eneo la Taida."
Bw. Yang Boning alisema, katika kipindi cha mwanzo baada ya kampuni ya Motorola kuwekeza nchini China, ufunguaji mlango wa China ulikuwa cha kiwango cha chini, na kulikuwa na vizuizi vingi kwa uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni, lakini eneo la ustawishaji la Taida liliruhusu kampuni ya Motorola kujenga kiwanda chenye mitaji ya kampuni yake pekee, jambo ambalo linaonesha eneo hilo la ustawishaji linazingatia sana kanuni ya ufunguaji mlango kwa nchi za nje.
Kwenye msingi wa kujiimarisha kwa eneo la ustawishaji la Taida, wasanifu wa sehemu mpya ya Binhai ya mji wa Tianjin walianza kufikiria namna ya kuleta maendeleo makubwa zaidi kwa kutumia ubora wa huko. Kuangalia ramani ya China, sehemu mpya ya Binhai ya Tianjin iko katika pwani ya bahari ya Bo ya Chna, kwenye pwani hiyo kuna banfari kubwa iliyotengenezwa a binadamu nchini China na mabohari ya kuwekea bidhaa zisizotozwa kodi, licha ya hayo huko penye ubora kwa maendeleo ya sekta za uchukuzi na usambazaji bidhaa.
Bandari ya mji wa Tianjin una maeneo ya bahari na nchi kavu jumla ya kilomita za mraba karibu 200, ambapo meli zenye uwezo wa kubeba tani laki 1.5 zinaweza kuingia na kutoka badari hiyo wakati wowote bila ya kujali hali ya hewa, uwezo wa bandari hiyo wa kushughulikia mizigo ni tani zaidi ya milioni 200 kwa mwaka. Eneo la mabohari ya kuwekea bidhaa zisizotozwa kodi katika bandari ya Tianjin yakiwa ya kwanza kwa ukubwa kwenye sehemu ya kaskazini mwa China, linavutia kampuni nyingi za kisasa za usambazaji bidhaa na viwanda vya usindikaji na biashara kuwekeza huko. Hadi mwishoni mwa mwaka uliopita, eneo la mabohari lilivutia kampuni na viwanda vya China na nchi za nje zaidi ya 5,700 kuingia kwenye eneo hilo vikiwemo vituo vya usindikaji vya nafaka, mafuta ya kupikia pamoja na chakula cha makopo ya nyanya zinazosafirishwa kwa nchi za nje, vituo hivyo vinachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa katika shughuli za usindikaji wa chakula nchini China. Katika miaka mitano ijayo, sehemu mpya ya Binhai itaendelea kupanua bandari ya Tianjin na eneo la mabohari na kukuza uwezo wake. Katibu wa chama wa kamati ya mawasiliano ya mji wa Tianjin Bw. Liu Mingde alisema,
"Bandari ya Tianjin itajenga njia yenye kina ya usafiri wa meli inayotumiwa na meli zenye uwezo wa kubeba uzito wa tani laki 2.5 na kuwa na uwezo wa kushughulikia tani zaidi ya milioni 300 za mizogo kwa mwaka."
Wasikilizaji wapendwa, sehemu mpya ya Binhai ya Tianjin imekuwa na sekta muhimu za upashanaji habari wa elektroniki, uzalishaji magari, kazi za kemikali ya mafuta ya asili ya petroli, uyeyushaji wa madini, teknolojia ya (viumbe) biology na madawa ya kisasa na uendelezaji wa nishati wa aina mpya. Wakati wa kukuza maendeleo ya uchumi, sehemu mpya ya Binhai haikusahamu namna ya kudumisha maendeleo mwafaka kati ya uchumi, jamii na mazingira ya asili. Miradi ya hifadhi ya mazingira ikiwemo ya kuyeyusha chuma cha pua kilichokwisha tumika na uteketezaji wa takataka inaungwa mkono sana kwenye sehemu mpya ya Binhai. Hivi sasa ardhi oevu(ardhi yenye vidimbwi) yenye eneo la kilomita za mraba zaidi ya 500 kwenye sehemu mpya ya Binhai imahifadhiwa kwa mwafaka, eneo lenye miti na majani limefikia 35% kwenye sehemu ya Binhai, ubora wa maji yaliyokwisha tumiwa na kusafishwa umefikia kiwango cha maji safi ya kunywa, nishati inayotumiwa katika kuzalisha mali yenye thamani ya Yuan elfu 10 ni sehemu moja kwa kumi ya wastani matumizi ya nishati ya China.
Maendeleo bora na ya mwafaka kati ya uchumi na mazingira yameleta mazingira bora ya maisha na kazi kwa wakazi wa sehemu ya Binhai. Katika sehemu hiyo mwandishi wetu wa habari aliona karakana nyingi safi zilizojengwa kwa utaratibu mzuri, barababara pana kwenye maeneo ya makazi wa watu, bustani za mitaani, uwanja wa mapumziko na sehemu nyingi zilizopandwa miti, maua na majani. Bibi Florenee Cherry ambaye amehamia na kufanya kazi huko, alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa kazi za hifadhi ya mazingira ya kimaumbile kwenye sehemu mpya ya Binhai ni nzuri sana na kumshangaza,
"Tokea muda mrefu uliopita, wanafanya kazi kama watu wa Marekani, wanarudisha karatasi na vitu vya plastiki na madini. Hawatupi ovyoovyo karatasi zilizotumika na makopo matupu, wanavitumia kwa mara nyingine tena, njia hii ni ya kuhifadhi mazingira. Nijambo muhimu sana kwa sisi kuhifadhi vizuri mazingira ya makazi yetu na ya dunia. Kwa kuwa mazingira ya maumbile ni ya uwianona ya kupatana, uwiano huo ukivunjika, yatatokea maafa, hivyo tunapaswa kuhifadhi vizuri mazingira yetu."
Wasikilizaji wapendwa, kufuatilia maendeleo ya utulivu, uwiano na ya pande mbalimbali ni lengo la China, ofisa wa kamati ya usimamizi wa sehemu ya Binhai ya Tianjin alisema kuwa katika siku za baadaye Binhai itaendelea kudumisha maendeleo ya muda mrefu ya uchumi na kudumisha mazingira bora ya kimaumbile.
Idhaa ya Kiswahili 2006-05-16
|