Tarehe mosi May kila mwaka ni siku ya wafanyakazi duniani. Sikuhiyo mwaka huu ilikuwa na maana sana kwa Bw. Zhu Zhisheng ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Hangzhou iliyopo mkoani Zhejiang, mashariki mwa China. Ni siku ya maana sana kwake kwa kuwa katika siku hiyo, alitunukiwa nishani medali ya May mosi na serikali ya China, nishani hiyo ni sifa ya juu kabisa inayotolewa kwa wafanyakazi wa China.
Bw. Zhu mwenye umri wa miaka 37 ni mfanyakazi wa kutengeneza chuma na chuma cha pua katika kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Hangzhou, ambayo ni kampuni yenye historia ya takriban miaka 50 na inachukua nafasi ya 94 miongoni mwa kampuni kubwa 500 za kwanza nchini China.
Miaka zaidi ya kumi iliyopita, kampuni hiyo ilipokuwa inatafuta wafanyakazi, Bw. Zhu aliyekuwa amehitimu kutoka sekondari ya juu na alikuwa anashughulikia kilimo katika maskani yake yaliyopo milimani kilomita 100 mbali na mji wa Hangzhou. Bw. Zhu alishinda mtihani na kuajiriwa katika karakana ya kuyeyusha chuma cha pua.
Bw. Zhu alikumbusha kuwa mara ya kwanza alipofika katika karakana hiyo, jinsi alivyoshangazwa kwa kushuhudia tanuri kubwa la kuyeyushia chuma cha pua na chuma cha pua ambacho kimeshayeyushwa kinachowaka. Alipata wasiwasi kidogo, anasema "Nilikuwa najisikia hofu kwa kushuhudia moto unaowaka, niliona joto sana. Sura ya namna hii nilikuwa sijawahi kuiona kabla ya hapo."
Kuyeyusha chuma cha pua ni kazi ngumu tanuri la chungu cha kuyeyushia chuma cha pua lenye nyuzi joto 1,700, na kuvumilia joto kali sana.
Kwa ajili ya kufahamu mchakato mzima wa kuyeyusha chuma cha pua, Bw. Zhu Zhisheng alikuwa anasimama mbele ya tanuri hilo kwa masaa kadhaa, bila kujali jasho zinazofululiza kutoka kwenye uso wake na mwili wake, akifuatilia kwa makini mabadiliko ya moto.
Kabla ya Bw. Zhu Zhisheng kuingia kazini, wafanyakazi wengi watokao mijini wamekuwa wakishindwa kazi hiyo. Lakini Bw. Zhu aliyekulia kijijini ana tabia ya kukabiliana na ugumu, akafanikiwa kushinda kazi hiyo.
Hata hivyo kijana huyo hakuridhika na mafanikio hayo. Kwa maoni yake, mbali na nguvu na uzoefu, mfanyakazi anapaswa kuwa na ufundi. Anasema "Mfanyakazi anapaswa kuwa na kiwango fulani cha ujuzi, ufundi na uwezo wa usimamizi. Hayo yote ni masharti ya kwanza ya kufanikiwa katika kazi."
Kwa ajili ya kupata ufundi wa kuyeyusha chuma cha pua na kuwa hodari katika ufundi huo, Bw. Zhu Zhisheng alinunua vitabu vingi vya taaluma ya kuyeyusha chuma cha pua. Alikuwa na bidii katika kusoma vitabu baada ya kazi.
Katika kazi yake, Bw. Zhu Zhisheng aligundua kuwa, bidhaa za chuma cha pua zilizotengenezwa kwa nyakati tofauti zina ubora tofuati, na baadhi ya wakati nyufa zinapatikana katika bidhaa hizo. Je, kwa nini hali ya namna hii inajitokea?
Alitafuta majibu ya maswali hayo kwenye vitabu na katika kazi yake. Alirekodi data za kuyeyusha chuma cha pua, na kuzilinganisha data hizo. Pia aliwauliza wafanyakazi wazee wenye uzoefu mara kwa mara, kiasi ambacho akajulikana sana miongoni mwa wafanyakazi wazee katika karakana yake.
Bw. Luo Gangsheng aliyefanya kazi katika karakana hiyo alimkumbuka kijana huyo akisema, "Baada ya kazi alinitembelea mara kwa mara nyumbani kwangu. Tulijadiliana maswali yake, na jinsi ya kuyatatua masuali hayo."
Jitihada za Bw. Zhu Zhisheng zimezaa matunda. Alivumbua mbinu mbalimbali za kiufundi, na mbinu hizo zimeenezwa katika uzalishaji wa kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Hangzhou na kuiletea kampuni hiyo manufaa makubwa. Mbinu moja baada ya kutekelezwa, wastani wa uzalishaji wa chuma cha pua kwa mwezi ukaongezeka kwa tani elfu 2 na kuokoa matumizi karibu ya RMB laki 8, kiasi ambacho ni sawa na dola za kimarekani laki moja.
Kutokana na uhodari wa kazi yake, miaka sita iliyopita Bw. Zhu Zhisheng aliteuliwa kuwa mkuu wa tume moja ya wafanyakazi, ambapo kwa ajili ya kushinda kazi hiyo mpya, alijiona anapaswa kupata ujuzi mwingi kuhusu usimamizi. Kwa hiyo alijilipa ada na kushiriki masomo ya taaluma ya usimamizi katika chuo kikuu miaka mitatu iliyopita, akapata shahada ya kwanza kwa muda wa miaka miwili na nusu tu.
Kutokana na uongozi wake hodari, tume yake ilikuwa inatia fora katika ukaguzi wa kampuni miongoni mwa vikundi 12 vya kuyeyusha chuma cha pua za kampuni hiyo kila mwaka katika miaka 6 iliyopita.
Katika siku ya wafanyakazi duniani mwaka huu, Bw. Zhu Zhisheng alikuja Beijing na kupewa medali ya May Mosi ambayo ni ndoto ya wafanyakazi wote hapa nchini China.
Wimbo huo wenye kichwa cha "sisi wafanyakazi ni wenye nguvu" ni wimbo anaopenda zaidi kuliko nyimbo nyingine. Bw. Zhu Zhisheng alisema wimbo huo unaonesha umuhimu wa wafanyakazi.
Idhaa ya Kiswahili 2006-05-18
|