Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-23 16:57:51    
Benki ya dunia yainua kadirio la ongezeko wa uchumi wa China kwa mwaka huu

cri

Benki ya dunia tarehe 10 hapa Beijing ilitoa toleo lake la kila miezi mitatu kuhusu "Uchumi wa China" ikikadiria juu zaidi ongezeko la uchumi wa China  kuwa asilimia 9.5 mwaka huu. Mtaalamu wa uchumi wa ngazi ya juu wa Benki ya dunia Bwana Louis Kuijs alisema, ingawa benki ya dunia imeinua zaidi makadirio ya ongezeko la uchumi wa China mwaka huu, lakini hii haimaanishi kuwa hali ya ongezeko la kupita kiasi imeonekana katika uchumi wa China, bali ni kwa sababu China iko katika kipindi cha maendeleo ya uchumi, hivyo ongezeko la kasi la uchumi wa China la miaka mfululizo ni la hali ya kawaida.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na idara ya takwimu za taifa la China, katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu, uchumi wa China uliongezeka kwa haraka, thamani ya jumla ya uzalishaji mali wa China iliongezeka kwa asilimia 10.2 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

Mtaalamu Louis Kuijs alisema, kutokana na ongezeko la kasi na lenye nguvu la uchumi wa China katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu, hivyo Benki ya Dunia imeinua zaidi makadirio ya ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka huu kuwa asilimia 9.5 badala ya asilimia 9.1 kama ilivyokadiria hapo kabla. Alisema:

Kwa hali ya jumla, kudumisha kiwango cha ongezeko la asilimia 10 la uchumi kunalingana na hali ilivyo ya sasa ya uwezo wa uzalishaji wa mali nchini China, katika hali ambayo uwekezaji na utoaji nafasi za ajira unaongezeka, na mageuzi ya kiteknolojia yanafanyika katika sekta mbalimbali, na hii ni hali mwafaka kwa China kudumisha ongezeko hilo la uchumi.

Bwana Louis Kuijs alidhihirisha pia kuwa, bado kuna hali ya wasiwasi katika ongezeko la kasi la uchumi wa China. Alitoa mfano kwa kusema, katika miezi mitatu ya mwanzo mwaka huu, uwekezaji katika mali zisizohamishika za jamii nzima ya China uliongezeka kwa asilimia 28 kuliko mwaka jana wakati kama huu, ambapo thamani ya uuzaji bidhaa iliongezeka kwa asilimia 27 kuliko mwaka jana wakati kama huu, lakini ongezeko la thamani ya uuzaji wa rejareja wa vitu vya matumizi ya jamii lilikuwa chini ya asilimia 13, hali hii imeonesha kuwa, ongezeko la uchumi wa China lilitegemea zaidi uuzaji wa bidhaa katika nchi za nje na upanuaji wa uwekezaji. Amesema China inatakiwa kupanua matumizi ya nchini ili kusaidia ongezeko la uchumi wake.

Bwana Louis Kuijs alisema Benki ya dunia imeona kuwa, serikali ya China inafanya juhudi za kuweka mkazo katika kuunga mkono maendeleo ya mambo ya watu wa jamii badala ya kuwekeza kwenye mali zisizohamishika peke yake, na inatumia sera ya ushuru nafuu kwa kuwahamasisha watu wa jamii wawekeze vitega uchumi kwenye shughuli za huduma badala ya shughuli za utengenezaji na biashara na nchi za nje. Hatua hii imeonesha kuwa serikali ya China inafanya marekebisho juu ya njia ya kujipatia ongezeko la uchumi, ili kuongeza hali ya uwiano ya ongezeko la uchumi. Alisema:

Kutimiza hali ya uwiano ya ongezeko la uchumi ni moja kati ya malengo makubwa zaidi katika mpango wa 11 wa China wa maendeleo ya miaka mitano ijayo, serikali ya China inataka kupunguza hali isiyo ya uwiano katika maendeleo ya uchumi, ili kujipatia ongezeko la uchumi kwa miaka mingi mfululizo. Serikali ya China imechukua hatua kadhaa kama vile kuwaelekeza wananchi katika matumizi yao, kuvitoza ushuru viwanda vinavyotumia nishati kwa wingi sana na kutoa uchafuzi mkubwa zaidi, kurekebisha sera ya ushuru wa matumizi ya magari, na kuzingatia zaidi kutenga fedha kwa ajili ya mambo ya vijijini.

Bwana Lousi Koijs alisema, Benki ya dunia inapenda kushirikiana na serikali ya China katika kutatua matatizo yaliyopo katika maendeleo ya uchumi wa China, ili kuisaidia China kutimiza maendeleo yenye uwiano.

Alisema kutoana na ongezeko la kasi la uchumi wa China katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu, Benki ya Dunia inaona kuwa ongezeko la kasi la uchumi wa China litadumu kwa muda, lakini kadiri sera za China za marekebisho na udhibiti zinavyotekelezwa, ndivyo ongezeko hilo la uchumi litakavyopungua hatua kwa hatua.

Idhaa ya kiswhaili 2006-05-23