Mahitaji
Samaki mmoja, kiasi kidogo cha vitunguu maji na tangawizi, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, mchuzi wa soya vijiko viwili, unga wenye ladha ya viungo vitano, sukari kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, na chumvi kijiiko moja.
Njia
1. ondoa vitu vya ndani vya samaki, mwoshe halafu mkate awe vipande, iweke pamoja na mchuzi wa soya, chumvi, mvinyo wa kupikia, vitunguu maji na tangawizi.
2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe joto la nyuzi 70, tia vipande vya samaki vikaange halafu vipakue.
3. washa moto tena, tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi korogakoroga, mimina mvinyo wa kupikia, mchuzi wa soya, maji, chumvi, M.S.G, sukari, unga wenye ladha ya viungo vitano, siki na vipande vya samaki, baada ya kuchemka, punguza moto na endelea kuchemsha kwa dakika 30, halafu vipakue.
4. weka vipande vya samaki kwenye sufuria, chemsha kwa mvuke kwa dakika 15. vipakue na mimina mafuta ya ufuta. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|