Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-25 16:42:59    
Siku ya kina mama na Siku ya kina baba: siku za vijana wa China kutoa shukrani kwa wazazi wao

cri

Siku ya kina mama na Siku ya kina baba ni sikukuu mbili za kigeni zilizoingia nchini China katika miaka ya hivi karibuni. Hivi sasa siku hizo mbili zimeenea sana miongoni mwa Wachina, hususan vijana.

Bw. Hules ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo kikuu cha Mongolia ya ndani, katika kadi aliyomtumia mama yake kwa kumpongeza katika siku ya kina mama, aliandika hivi: "Mama, ingawa sijawahi kuelezea upendo wangu kwako, lakini nakupenda daima moyoni mwangu. Nakutakia afya njema na furaha."

Mvulana huyo alimwambia mwandishi wa habari kuwa, "Mpaka sasa sijawahi kuwaambia wazazi wangu nawapende tukiwa ana kwa ana, wala sijawahi kuwakumbatia, lakini nawafahamisha upendo wangu wakati wa siku ya kina mama na siku ya kina baba kila mwaka."

Katika utamaduni wa Kichina, wazazi kuwalea watoto ni fadhila kubwa kuliko nyingine katika uhusiano kati ya watu. Lakini kutokana na Wachina kuwa na tabia ya kujizuia, wanapenda kuhifadhi shukrani moyoni badala ya kuwaambia jamaa zao ana kwa ana. Hata vijana wa China wanaopokea elimu ya kisasa pia wanafuata utamaduni wa jadi. Kwa hiyo siku ya kina mama na siku ya kina baba ambazo ni sikukuu za kigeni zilizoingia nchini China katika miaka ya hivi karibuni, zinatumika na Wachina wanaothamini upendo na kutumia fursa ya kuelezea hisia zao.

Bibi Dong anayefanya kazi katika serikali ya mji wa Huhehaote, magharibi kaskazini mwa China akikumbusha siku ya kina mama ya mwaka uliopita, alisisimka sana na kusema, "Katika siku ya kina mama ya mwaka jana, binti yangu aliye katika mji wa Chongqing alinitumia zawadi na barua ndefu ya kutoa shukrani. Nilikuwa nasisimka sana kiasi nikashindwa kupata usingizi usiku kucha. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa mtoto wangu kuniandikia barua na kunipa shukrani nyingi mno."

Kutokana na shughuli mbalimbali zilizoandaliwa na wafanyabiashara, tunaweza kutambua jinsi Wachina wanavyotilia maanani siku hizo mbili za kigeni. Kabla ya siku ya kina mama ambayo ilikuwa tarehe 14, May kwa mwaka huu, mwandishi wetu wa habari alipotembelea mjini Huhehaote, aligundua kuwa, maduka yenye bidhaa zinazohusiana na wanawake yote yalitumia mbinu mbalimbali za mauzo kwa ajili ya "kina mama wapendwa". Na katika milango ya mihahawa mbalimbali, yalioneshwa mabango ya kuwakumbusha watu siku ya kina mama inakaribia. Ujumbe wa kuwapongeza kina mama ulikuwa unaenea kwenye simu za mikono, na tovuti zinazotoa huduma za kadi pia ziliandaa kadi za ilektroniki kwa ajili ya siku ya kina mama.

Katika shule mbalimbali, zawadi kwa mama ni topiki iliyozungumzwa sana na watoto wengi walitaka kuwapa mama zao shukrani katika siku hiyo maalumu. Mwalimu Agula wa Chuo kikuu cha Mongolia ya ndani alieleza maoni yake akisema, "Katika siku ya kina mama, tunapaswa kutoa shukrani kwa mama. Lakini si lazima kuwanunulia maua au kuwapa zawadi. Labda tunawaandalia chai au kuwasalimia, vitendo hivyo vidogo pia vinaweza kugusa hisia za mama."

Kijana Gerile anayesoma katika chuo kikuu hicho alisema, "Mambo madogo madogo maishani yanaweza kuwafahamisha wazazi wangu kuwa tunawashukuru sana, lakini ni nadra kwetu kubadilishana maeneo matupu ya shurkani. Kwa hiyo wakati wa siku ya kina mama na siku ya kina baba, ninapenda kuwatakia heri ya sikukuu."

Aliongeza kuwa, "Baada ya siku ya kina mama tarehe 14 May, inakaribia siku ya kina baba ambayo itakuwa tarehe 18 Juni kwa mwaka huu. Kwa hiyo sasa nimeanza kufikiria zawadi kwa babangu."

Idhaa ya kiswahili 2006-05-25