Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-29 15:07:54    
Ukuta mkuu

cri

Ukuta mkuu unachukuliwa na wachina kuwa ni fahari ya taifa lao, ukuta mkuu wenye urefu mkubwa ambao ni moja kati ya miradi mikubwa zaidi katika historia ya binadamu unatambaa kwenye ardhi kubwa ya sehemu ya kaskazini ya China. Ukuta mkuu si kama tu ni mali ya urithi wa utamaduni duniani, bali pia ni kivutio cha kimaumbile chenye mtindo maalum.

Ukuta mkuu wa China ulijengwa kuanzia kipindi cha madola ya kivita cha China ya kale zaidi ya miaka 2000 iliyopita, ukuta mkuu huo ni mradi mkubwa zaidi wa ulinzi uliojengwa kwa miaka mingi zaidi katika China ya kale. Mwaka 221 kabla Kristo, baada ya mfalme Qin Shihuang kuunganisha China nzima, ukuta mkuu wa madola mbalimbali ya wakati huo uliunganishwa. Ilipofika Enzi ya Han ya kabla na baada ya Kristo, sehemu nyingi za ukuta mkuu uliojengwa mwanzoni wakati wa enzi mbalimbali ziliharibika, na sehemu kamili iliyobaki ya ukuta mkuu huo ndio ukuta uliojengwa katika Enzi ya Ming ya zaidi ya miaka 700 iliyopita.

Je mradi huo mkubwa namna hii duniani ulijengwa na watu gani? Katibu mkuu wa Taasisi ya ukuta mkuu wa China inayoshughulikia utafiti na uhifadhi wa ukuta mkuu Bwana Dong Yaohui alituambia:

Watu walioshiriki katika ujenzi wa ukuta mkuu waligawanyika kuwa wa aina tatu, wa kwanza ni askari wa jeshi, kwani kujenga ukuta mkuu ilikuwa ni hatua ya serikali, na jeshi lilikuwa ni uti wa mgongo wa wajenzi wa ukuta; wa pili ni vibarua na wa tatu ni wahalifu walioadhibiwa kushiriki kwenye ujenzi wa ukuta.

Mradi mkuu wa ukuta mkuu ulijengwa kwa kufuata sura ya kijiografia, sehemu nyingi za ukuta mkuu zilijengwa kwenye milima mirefu au tambarare zenye vipengele vya hatari, kwani ukuta mkuu uliojengwa kwenye sehemu hizo uliweza kuonesha vizuri uwezo wake wa kujilinda. Katika ukuta mkuu, vilijengwa vidungu vingi vya uangalizi na vidungu vya kuonesha moto wa kutoa tahadhari. Maofisa na askari waliokaa kwenye ukuta mkuu waliweza kutegemea kuta imara zenye kimo cha juu kupambana na maadui waliowashambulia; walipokuta washambulizi wengi waliweza kuwasha moto kwenye vidungu ili kutoa habari na kuomba msaada. Tokea kujengwa kwa ukuta mkuu huo, mapigano makali yalifanyika chini ya ukuta huo mkuu.

Hivi sasa ukuta mkuu si tena jengo la kijeshi, bali umekuwa mabaki maarufu ya kale. Ukuta mkuu huo kila mwaka unawavutia watalii wa China na wa nchi za nje wapatao zaidi ya milioni 10. Katika ukuta mkuu huo, sehemu yake iliyoko hapa Beijing ni sehemu imara zaidi ambayo inaonekana kuwa ni ukuta mkubwa wenye mvuto zaidi. Kwani ukuta wa sehemu hiyo ulifanya kazi muhimu ya kulinda mji mkuu na makaburi ya wafalme. Hivi sasa sehemu za Badaling, Mutianyu na Simatai zilizoko kwenye kitongoji cha Beijing zote zimekuwa sehemu za vivutio vya ukuta mkuu.

Miongoni mwa sehemu hizo, "Ukuta mkuu wa Badaling" ulioko kaskazini ya Beijing unajulikana zaidi kuliko ukuta mkuu wa sehemu nyingine. Ukuta Mkuu wa Badaling ulijengwa kuwa imara zaidi, ambao ulihifadhiwa vizuri zaidi kuliko wa sehemu nyingine, watalii wengi wanapenda kupanda ukuta mkuu wa sehemu hiyo. Ukuta mkuu wa Badaling ulijengwa kwa kufuata milima, na unatambaa kwenye sehemu ya juu na chini, ukuta huo ulijengwa kwa mawe mengi makubwa ya miamba, wastani wa kimo cha ukuta huo ni mita 8. Kila baada ya sehemu ya zaidi ya mita 200 kuna kidungu cha uangalizi, kwa kweli kinga ya ulinzi iliwekwa kwenye sehemu nzima ya ukuta mkuu.

Msichana kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 Bi. Helena Darcq ametembelea Ukuta mkuu wa Badaling mara nyingi, alisema daima hawezi kusahau aliyojihisi wakati alipopanda juu ya ukuta mkuu kwa mara ya kwanza. Alisema:

Siwezi kusahau siku ile nilipopanda ukuta mkuu wa China, ambapo niliona ukuta mkuu unatambaa kwa kufuata milima iliyoelekea mbali, machoni mwangu pote palikuwa na rangi ya kijani, mandhari ya huko ni nzuri iliyoje. Na kitu kilichonigusa zaidi moyoni, ni kuwa tulipanda ukuta mkuu kwa kufuata ngazi moja moja, tulitumia nguvu kubwa na kutokwa jasho, lakini tuliona mandhari nzuri ya kupendeza sana.

Tukielekea sehemu ya mashariki ya Ukuta mkuu wa Badaling tutafika Ukuta mkuu wa Mutianyu. Ukuta mkuu wa sehemu hiyo pia umehifadhiwa vizuri na kikamilifu. Kwenye Ukuta mkuu wa Mutianyu, kuna roshani tatu zilizojengwa kwa safu tatu, hiki ni kivutio pekee kwenye sehemu nzima ya ukuta mkuu. Aidha, katika sehemu ya Ukuta mkuu wa Mutianyu, miti inasitawi zaidi kuliko sehemu nyingine, hasa katika majira ya mchipuko, miti na maua ya rangi mbalimbali ya sehemu hiyo ya ukuta mkuu yanawavutia zaidi watalii.

Na tukiendelea kuelekea mashariki ya Ukuta mkuu wa Mutianyu tutafika Ukuta mkuu wa Simatai. Hii ni sehemu yenye milima mirefu zaidi, ambapo ukuta mkuu kama ulijengwa kwenye miamba mikali, hali yake ya hatari inawashangaza sana watu, hiki ni kivutio cha ukuta mkuu wa sehemu hiyo.

Zaidi ya hayo, katika sehemu ya Beijing pia kuna sehemu mbalimbali maarufu za ukuta mkuu, kama vile Ukuta mkuu wa Mlango wa Juyong, na Ukuta mkuu wa Mji mdogo Huanghua, kila sehemu ina vivutio vyake.

Wasikilizaji wapendwa, ukuta mkuu wa China ni jengo kubwa ambalo pia ni ushahidi wa historia ya mabadiliko ya jamii ya China katika zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Watu fulani wanasema, ukuta mkuu ni kama mgongo wa taifa la China, lakini kwa watu wa China, ukuta mkuu unawakilisha moyo wa taifa la China. Mtalii mmoja kutoka kisiwa cha Taiwan Bwana Lai Baojia alisema, kila alipotembelea Ukuta mkuu, huwa anaona fahari akiwa mchina. Alisema:

Ukuta mkuu unawakilisha moyo wa taifa, pia unawakilisha akili na werevu wa wachina. Ukiona ukuta huo mkuu uliojengwa katika miaka mingi iliyopita ambao unatambaa na kuwavutia watu katika dunia, hakika utaona fahari ukiwa mchina.

Idhaa ya kiswahili 2006-05-29