Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-31 19:51:51    
Mapishi ya kupika vipande vya nyama ya kuku pamoja na mbegu za yungiyungi

cri

Mahitaji: Nyama ya kuku gramu 250, mafuta gramu 50, ute wa mayai mawili, kiasi kidogo cha mbegu za yungiyungi, maharagwe mabichi, sukari, mvinyo wa kupikia, chumvi, M.S.G, vitunguu maji, tangawizi na wanga.

Njia:

1. Chemsha maji halafu tia mbegu za yungiyungi, baada ya kuiva pakua. Kata nyama ya kuku iwe vipande, kata vitunguu maji na tangawizi viwe vipande, weka vipande vya nyama ya kuku kwenye bakuli, tia chumvi, mvinyo wa kupikia, M.S.G, ute wa yai, kasha korogakoroga.

2. pasha moto tia vipande vya nyama ya kuku, korogakoroga, tia vipande vya maharagwe mabichi na mbegu za yungiyungi, korogakoroga, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, tia mvinyo wa kupikia, chumvi, M.S.G, maji ya wanga, halafu korogakoroga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-05-31