Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-02 19:58:25    
Mashindano ya kimataifa ya wanafunzi wa vyuo vikuu kuongea lugha ya Kichina yafanyika katika taasisi ya Confucious ya Nairobi

cri

 

Tarehe 31 mwezi Mei, ni sikukuu ya Duanwu, sikukuu hiyo ni muhimu sana kwa wachina katika utamaduni wetu. Katika siku hiyo maalum, mashindano ya kimataifa ya wanafunzi wa vyuo vikuu kuongea lugha ya Kichina yalifanyika katika taasisi ya Confucious ya Nairobi, mashindano hayo yalijulikana kama "Daraja la lugha ya Kichina". Mashindano ya mwanzo yanafanyika katika nchi mbalimbali duniani kwa wakati mmoja, na Kenya ni mojawapo, kama washindi wa nchi nyingine, mshindi mmoja wa Kenya atapewa fursa ya kushiriki katika fainali itakayofanyika Beijing China mwezi ujao.

Wasikilizaji wapendwa, mliosikia sasa hivi ni mshindani mmoja akiimba wimbo wa kichina uitwao wimbo wa mapenzi ya Kangding.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika nchini Kenya, na idara iliyoandalia mashindano hayo ni Taasisi ya Confucious ya Nairobi, ambayo ni tasisi ya Confucious ya kwanza na ya pekee barani Afrika. Hivyo tunaweza kusema kwamba hayo ni mashindano yenye umuhimu maalum.

Kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, mkuu wa taasisi ya Confucious ya Nairobi Bw. Mbeche alitoa hotuba akisema:

"kwanza tunawakaribisha wageni wetu wanaokuja hapa kushuhudia mashindano hayo, na sisi tunaamini kwamba nyote mnaoshiriki katika mashindano hayo mtafanya kazi vizuri."

 

Mashidano hayo yaligawanyika katika sehemu tatu, yaani kutoa hotuba kwa lugha ya Kichina, kujibu maswali kuhusu utamaduni wa China na kuonesha kipaji cha usanii. Baada ya kuchujwa, walibaki wanafunzi 9 wanaoweza kushiriki katika mashindano hayo, hao wote ni wanafunzi wa taasisi ya Confucious ya Nairobi. Wanafunzi hao wamejifunza lugha ya Kichina kwa muda wa miezi mitatu tu, lakini Kichina chao kimefika kiwango cha kuweza kutoa hotuba. Hotuba zao zilihusu mambo mbalimbali kama vile maandiko ya Kichina, Gongfu ya Kichina na Mchezo wa Olympiki utakaofanyika Beijing mwaka 2008. Wakati wa mashindano, walionesha hamu kubwa ya kufahamu utamaduni wa China, na kwa kweili, wamejua mengi.

Mshindani mmoja anayeitwa Lena Christine, ni mshabiki wa Radio China Kimataifa, katika hotuba yake, alisema:

"Napenda Radio China Kimataifa ni kwa sababu inatangaza kwa Kiswahili sanifu. Nimesikiliza radio hiyo kwa muda mrefu, kwa kupitia sauti hiyo kutoka China, nimejua mambo mengi kuhusu China. Kipindi ninachopenda zaidi ni Safari Nchini China, katika kipindi hiki, mtangazaji anatumia sauti yake nyororo kutuelezea vivutio vya mandhari ya China, nikifumba macho, ninaona kama nimefika China, ukuta mkuu unasimama mbele yangu, na ngurumo ya Mto Huanghe pia inasikika."

Mshidani mwingine anayeitwa Ruth Njeri alitaja mkutano na rais Hu Jintao katika hotuba yake. Wakati rais Hu Jintao wa China alipofanya ziara nchini Kenya alikutana na wanafunzi na walimu wote wa Taasisi ya Confucious ya Nairobi, na Njeri ndiye aliyetoa hotuba kwa niaba ya wanafunzi wote, na kuongea na rais Hu kwa lugah ya Kichina. Alisema:

"Rais Hu alishikana mikono na kila mwanafunzi na mwalimu, sisi tukiwa wanafunzi wa taasisi ya Confucious tunajivunia sana. Tunaona kuwa kuchagua kujifunza lugha ya Kichina ni uamuzi mzuri kabisa maishani mwetu. Tuna matumaini kuwa siku moja tutapatia fursa kusafiri nchini China, na kushuhudia utamaduni wa China."

Mbali na kuongea vizuri Kichina, washindani pia walionesha vipaji vyao vya usanii. Mshindani mmoja aliwashangaza wageni wote kwa kusoma shairi moja la enzi ya Tang ya China.

Shairi hilo linaeleza jinsi watu waliokaa mbali na nyumbani kwao wanavyokumbuka maskani yao. Bila kujua maana ya shairi hilo, hawezi kusoma vizuri namna hiyo, .

Washindani wote walifanya vizuri, hali ambayo iliwafanya waaamuzi waone taabu ya kutoa uamuzi. Baada ya kujadiliana kwa muda mrefu, balozi wa China nchini Kenya ambaye pia ni mwamuzi mkuu wa mashindano hayo Bw. Guo Chongli alitangaza jina la mshindi wa kwanza.

"Anayeshika nafasi ya kwanza ni Ruth Njeri"

 

Baada ya kumtunukia mshindi wa kwanza hati na zawadi, balozi Guo Chongli alieleza matumaini yake kwa wanafunzi wa taasisi ya Confucious. Akisema,

"Natumai kwamba ninyi mtajitahidi zaidi katika masomo ya lugha ya Kichina na utamaduni wa China. Hivi sasa, uhusiano kati ya Kenya na China uko katika kipindi kizuri, na biashara kati ya nchi hizo mbili pia inaendelea kwa kasi, hivyo tunahitaji wakenya wanaojua Kichina na utamaduni wa China kutoa mchango wao kwa mawasiliano na urafiki kati ya Kenya na China."

Mwishoni, shughuli hiyo ilifika kilele chake katika wimbo wa Kichina wa maua ya jasmini ulioimbwa na wanafunzi wote. Tarehe 6 Mwezi Julai, Ruth Njeri atakwenda nchini China kushiriki katika mashidano kwa niaba ya Kenya, tunamtakia kila la heri katika safari ijayo.

Idhaa ya Kiswahili 2006-06-02