Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-23 20:30:08    
Mahojiano kati ya mwandishi wetu wa habari na balozi wa Tanzania nchi China Bwana Charles Sanga

cri

Mwandishi: Mheshimiwa Balozi, siku za karibuni waziri mkuu wa China Wen Jiabao atafanya ziara katika nchi 7 barani Afrika ikiwemo Tanzania, unauonaje uhusiano kati ya Tanzania na China.

Balozi: Uhusiano kati ya Tanzania na China siku zote umekuwa mzuri sana. Uzuri huo tunaweza kusema ulianzishwa na waanzilishi wa mataifa hayo mawili, kwa muda wa karibu miaka 46 sasa, tumekuwa na uhusiano wa karibu sana tumesaidiana katika mambo mengi sana. Ziara hii ni muhimu kwa jambo muhimu kubwa kwamba karibu miaka 10 hajawahi kufanya ziara nchini kwetu Tanzania, nakumba ziara ya mwisho ya waziri mkuu wa China nchini Tanania ilikuwa mwaka 1997, hii inadhihirisha kuwa, hawa viongozi wametambua umuhimu wa kuwatembelea viongozi wetu. Rais wetu, waziri mkuu wetu na waziri wetu wa mambo ya nje wamekuja hapa China kwa ziara,lakini viongozi wa ngazi ya juu wa China kama Bwana Wen Jaibao hawajatembelea Tanzania, kwa hiyo hata kama ziara hiyo ni ya siku moja yaani masaa 24 lakini siyo jambo baya , lakini naamini kwamba ziara yake hiyo itaimarisha zaidi uhusiano kati ya nchi zetu mbili na watu wake.

Mwandishi: Kwa maoni yako unafikiri ni kwa namna gani uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Tanzania unaweza kuboreshwa zaidi ?

Balozi: Kuna mambo mawili, upande wa kisiasa na upande wa kiuchumi. Kama nilivyosema, waanzilishi wa nchi zetu mbili walianzisha uhusiano wa kisiasa zaidi kuliko uhusiano wa kiuchumi, lakini dunia imebadilika, dunia inabadilika, sasa hivi dunia inaangalia zaidi maslahi ya watu. Waanzilishi walijenga uhusiano wetu na hivi sasa hivi dunia zaidi kuangalia suala la uchumi, mwezi Novemba kutakuwa na mkutano kati ya wakuu wa nchi za bara la Afrika na viongozi wa China, jambowa hilo limemeonesha umuhimu wa masuala ya uchumi. Sasa Tanzania tumepata misaada mingi sana ya kiuchumi, lakini misaada hiyo kwa Tanzania kweli ilitusaidia sisi watanzania, China ilitusaidia kujenga reli ya TAZARA, shamba la Mbarali, kiwanda cha urafiki cha Dar es Salaam, na mambo mengi sana. Na misaada hiyo yote kweli haikuleta faida kwa uchina, kiwanda cha majembe cha Ufi kilichopo mjini Dar es salaam.,Lakini sasa hivi mambo yamebadilika China imekuwa nchi yenye nguvu kubwa ya kiuchumi, mahitaji yake ya vitu mbalimbali kwa maendeleo ni makubwa, wenzetu wanahitaji, sisi tumekubali, lakini hawahitaji bure hata kidogo, wenzetu wanakuja na wanataka kununua vitu vyetu kwa bei ya soko, soko la dunia, siyo kwa bei wanayotupangia, sisi tumekubali na tunafaidika, na katika misaada hiyo wanayotoa hapa tunataka vitu vyote viwe na thamani, kama vile wanataka mbao, basi wasinunue magogo, wangeanzisha viwanda vya mbao, watengeneze vitu vinavyohitajika nyumbani, waanzishe viwanda vya samaki, viwanda vya kilimo, tunataka vitu vyetu viwe na thamani zaidi kuliko zamani, ziara hii tunaona jambo hilo litazingatiwa sana, na jambo muhimu ni miundo mibinu, tunaamini sana wenzetu wachina wanaweza kutusaidia sana katika ujenzi wa miundo mbinu, tuna makaa ya mawe, wakitusaidia, tunataka makaa yetu ya mawe yaweze kutumika katika kuzalisha umeme. Umeme uliozalishwa sasa hivi unategemea nguvu ya maji, mabwawa yakikauka, umeme unatakatika, na tuna gesi nyingi sana, tunataka wenzetu watusaidie kutumia gesi majumbani, pia kuzalisha umeme, wenzetu wachina wana uwezo mkubwa katika sekta hiyo, nafikiri jambo hilo katika ziara ya ya waziri mkuu wa China atalieleza na kuamua ushirikiano.

Mwandishi: Unafikiri ziara hiyo ya Bwana Wen Jiabao nchini Tanzania inaweza kusaidia kuendeleza ushirikiano kati ya China na Tanzania hasa katika sekta ya uchumi?

Balozi: Mwaka 2000, China ilianzisha Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, na ushirikiano huo umeimarika sasa kwa kiwango kikubwa sana, kuna maeneo ambayo tunakubaliana sana kushirikiana, moja ni namna ya kushirikiana vizuri zaidi katika ardhi yetu, sasa hivi wenzetu wanajitosheleza sana katika chakula . sisi Tanzania tuna ardhi kubwa sana, lakini bado sehemu kubwa haitumiki katika kazi ya kilimo, nyingine tunakubali kufanya ushirikiano katika sekta ya madini, tuna madini mengi sana, mafuta, dhahabu na madini mbalimbali, lakini vitu hivyo bado viko chini ya ardhi, tunataka kuvitoa kutoka chini ya ardhi ili viweze kutumika, na wenzetu pia wanavihitaji. Aidha, ni kuhusu mambo ya utalii, tuna vivutio vingi vizuri vya utalii, lakini shughuli zetu za utalii bado hazijaendelezwa, Tanzania imekuwa mojawapo kati ya nchi 16 za Afrika ambazo zimekubaliwa kuwapokea watalii kutoka China, ya nne ni kuhusu mambo ya uvuvi, tunataka China itusaidie kuanzisha viwanda vya uvuvi, nyingine tunapenda China itusaidie kuwaandaa watu wenye ujuzi, hatuna watu wengi wenye ujuzi, ila tunawagemea wataalamu kutoka nje, na hivi sasa wachina wanatusaidia sana kutoa mafunzo mbalimbali kwa watu wetu. Na kuhusu biashara, sasa hivi tunanunua zaidi kutoka China, na wachina wananua baadhi tu vitu vyetu, tunapaswa kufikiri kuwa, ni vitu gani wenzetu wanavipenda kuvinunua, tunawataka watuanzishie viwanda vya kubangua korosho, wachina wana uwezo mkubwa sana katika mawasiliano, tunataka watusaidie kujenga barabara na kuboresha hali yetu ya mawasiliano.