Gari la ukusanyaji wa damu lilisimama kwenye uwanja wa utamaduni wa Xidan, ulioko kwenye mtaa wenye maduka mengi mjini Beijing. Bibi Wang Yanqin mwenye umri wa miaka 52 alikuwa mmoja kati ya watu waliojitolea damu kwa hiari alijaza fomu mbele ya gari hilo, ambapo alimwambia mwandishi wetu habari kuwa, zamani serikali iliweka mpango wa kujitolea damu kwa watu wa idara za serikali, shule na viwanda na makampuni, kama watu wengine walivyo, Bibi Wang aliona kuwa ni bahati mbaya kwa watu waliochaguliwa kujitolea damu. Lakini msimamo wake ulibadilika baada ya kuona kuwa wagonjwa wengi walikuwa hawakuweza kupata matibabu kwa wakati kutokana na ukosefu wa damu, hivyo alianza kujitolea damu kwa hiari. Hadi hivi leo, Bibi Wang amejitolea damu mara 5, na kiasi cha damu aliyotoa kimefikia mililita 1000. Hivi sasa watu wanaopenda kujitolea damu kwa hiari kama Bibi Wang wamekuwa wengi.
Bibi Wang Shuiying mwenye umri wa miaka 77 alifanya kazi kwenye kituo cha damu cha Beijing kuanzia mwaka 1956, ingawa amestaafu, hivi leo akiwa mtu wa kujitolea alishiriki kazi ya kujibu maswali ya watu waliotaka kujiojitolea damu ili kuchangia shughuli za kujitolea damu kwa hiari.
Bibi Wang alisema, tangu utaratibu wa kujitolea damu kwa hiari utekelezwe mwaka 1978, shughuli za kukusanya damu zilikuta taabu kubwa, ambapo watu wengi huwa na wasiwasi kuwa, kujitolea damu kutadhuru afya za watu au kuambukizwa maradhi, lakini hivi sasa hali imebadilika kutokana na kueneza ujuzi kuhusu kujitolea damu.
Naibu mkurugenzi wa Kituo cha damu cha Chama cha msalaba mwekundu cha Beijing Bwana Ma Guodong alidokeza kuwa, idadi ya watu wanaotaka kujitolea damu kwa hiari imeongezeka na kufikia asilimia 98.7 mwaka 2006 kutoka asilimia 77.3 ya mwaka 2005, na kati ya watu hao vijana ni wengi zaidi. Katika miezi mitano ya mwaka huu iliyopita, miongoni mwa watu waliojitolea damu kwa hiari, watu wenye umri chini ya miaka 35 wanachukua asilimia 86.53.
Hadi sasa shughuli ya utoaji wa damu kwa hiari zimekuwepo kwa miaka 20 nchini China, na sheria inayohusika ilianzishswa mwaka 1998. Tarehe 12 Juni mwaka huu, mchezaji maarufu wa China Bwana Pu Cunxin alikwenda kwenye Kituo cha damu cha chama cha msalaba mwekundu cha Beijing, na kushiriki kwenye matangazo ya shughuli za kujitolea damu kwa hiari pamoja na wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Beijing, na kujitolea damu kwa hiari.
Kuanzia mwezi Septemba mwaka 2005, Beijing imeacha kuweka mpango wa kujitolea damu kwa watu wa idara mbalimbali, lakini mahitaji ya damu hayapungui. Takwimu kutoka Kituo cha damu cha Beijing zimeonesha kuwa, tokea mwezi Oktoba mwaka jana damu yote iliyotumiwa kwenye hospitali ilikuwa damu waliyojitolea watu kwa hiari.
Bwana Abu Lizi wa Chuo kikuu cha makabila cha China alimwambia mwandishi wetu kuwa, mwaka jana chuo hicho kiliwekwa mpango wa kuwachagua watu kwenda kituo cha damu cha Beijing kujitolea damu, mwaka huu mpango wa kawaida ulifutwa, ofisi husika ya chuo hicho iliwahamasisha tu, lakini hivi karibuni theluthi mbili ya wanafunzi wa chuo hicho walikwenda kituo hicho kutaka kujitolea damu kwa hiari.
Bwana Ma Guodong alisema, shughuli za kujitolea damu kwa hiari zinaendelea vizuri mjini Beijing, hivi sasa akiba ya damu mjini Beijing ni ya kutosha, na vituo vya kukusanya damu vilivyowekwa zamani katika vyuo vikuu mbalimbali mjini Beijing vimesimamishwa kuanzia mwezi Aprili mwaka huu.
Idhaa ya kiswahili 2006-06-28
|