Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-11 15:56:44    
Bidhaa za hifadhi ya mazingira na udhibiti wa matumizi ya nishati zapendwa na watu

cri

Kwenye maonesho ya udhibiti wa matumizi ya nishati na hifadhi ya mazingira, teknolojia na bidhaa za za udhibiti wa matumizi ya nishati yalivutia watu wengi, baadhi ya bidhaa na teknolojia zenye ufanisi katika kudhibiti matumizi ya nishati zilipendwa na watu.

Ili kuhimiza na kuunga mkono maendeleo ya uzalishaji bidhaa na uenezaji wa teknolojia za udhibiti wa matumizi ya nishati, Beijing iliandaa maonesho ya udhibiti wa matumizi ya nishati na hifadhi ya mazingira, ambayo yalishirikiwa kwa shauku kubwa kampuni na viwanda husika, ambavyo vilileta bidhaa na teknolojia mbalimbali kuhusu udhibiti wa matumizi ya umeme, maji na petroli. Kiongozi wa maonesho hayo, ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha huduma ya udhibiti wa matumizi ya nishati na hifadhi ya mazingira, Bw Chen Huaiwei alisema,

"Maonesho hayo yameshirikiwa na kampuni na viwanda zaidi ya 170, na kuoneshwa teknolojia na bidhaa mpya za udhibiti wa matumizi ya nishati na maji, na za hifadhi ya mazingira. Viwanda vikubwa vinashiriki kwa shauku kubwa, na vitu vinavyooneshwa ni vingi sana, ambavyo vinapendwa na kusifiwa na watu wa sekta mbalimbali za jamii."

Kuendeleza matumizi ya nishati isiyotoa udhafuzi ikiwa ni pamoja na ya upepo, mwangaza wa jua na ya kutokana na mimea, ni moja ya mikazo iliyowekwa katika sera mpya za nishati zinazotekelwa hivi sasa nchini China. Katika maonesho hayo, teknolojia ya kampuni ya teknolojia ya sayansi ya Shengchang ya Beijing ya kuzalisha umeme na kutoa joto kwa kutumia mimea, inafuatiliwa na watazamaji wengi. Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Fu Youhong alisema, kituo kinachozalisha umeme na kutoa joto kwa kutumia mimea, ambayo ni pamoja na mabua ya mihindi na ngano pamoja na punba za mbao, vitu hivyo vinasindikwa kuwa nishati yenye umbo la vitufe. Teknolojia hiyo, si kama tu inaweza kutumia vitu takataka, bali inaweza kupunguza uchafuzi kwa mazingira. Nishati hiyo isiyotoa uchafuzi imesifiwa na wanaviwanda wengi walioshiriki maonesho hayo. Bw. Fu Youhong alisema,

"Katika maonesho hayo, viwanda 7 au 8 hivi vilitutembelea vikitaka maboila yao yarekebishwe na kutumia nishati hiyo mpya. Tumepeleka wahandisi kwenda viwandani mwao kufanya uchunguzi ili kubuni mpango mpya wa kutumia nishati hiyo mpya. Tunajitahidi kukamilisha marekebisho katika viwanda 4 au 5 hivi kutumia nishati hiyo isiyotoa uchafuzi ndani ya mwezi mmoja au miezi miwili."

Sekta za viwanda na majengo nchini China ni sekta zinazotumia nishati nyingi, hivi sasa nishati zinazotumiwa na sekta hizo mbili zinachukua zaidi ya 90% ya jumla ya nishati inayotumiwa hapa nchini, hivyo bado kuna nafasi kubwa katika udhibiti wa matumizi ya nishati. Katika maonesho hayo, zana za udhibiti wa matumizi ya umeme zilivutia watazamaji wengi. Zana hizo zilisanifiwa na kutengenezwa na kampuni moja ya sehemu ya Pudong mjini Shanghai inayojulikana kwa Kangneng, ambazo zinaweza kutumika katika sekta za kazi za kemikali, vifaa vya ujenzi, makaa ya mawe na majengo ya umma ili kudhibiti matumizi ya umeme. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Kangneng Bw. Li Zhihong alisema, zana hizo za udhibiti wa matumizi ya umeme si kama tuna zinaweza kutunza zana za umeme na kuzifanya ziweze kutumika kwa muda mrefu zaidi, bali pia zinaweza kupunguza sana matumizi ya umeme, hivi sasa zana hizo zimefaulu katika ukaguzi wa idara husika ya serikali;

"Zana hizo hivi sasa zinaongoza duniani katika udhibiti wa matumizi ya umeme. Zana za aina hiyo zimetumika katika kampuni kadhaa kubwa nchini China zikiwemo kampuni ya mafuta ya asili ya petroli ya China na kampuni ya kazi za kemikali ya Jilin, na ufanisi mkubwa umepatikana."

Bw. Li Zhihong alisema, hivi sasa zana za aina hiyo zinanunuliwa sana masokoni katika muda wa mwaka zaidi ya mmoja tangu zilipoanza kuuzwa, katika maonesho hayo kampuni ya Kangneng ilipata oda za kampuni kubwa kumi kadhaa ikiwemo kampuni ya Huachen ya mji wa Shenyang. Idara za ujenzi wa miundo-mbinu za miji kadhaa ukiwemo mji wa Chongqing, zimewasiliana na kampuni ya Kangneng zikitarajia kupata zana hizo za udhibiti wa matumizi ya nishati ili kufanya marekebisho juu ya mifumo ya taa za kuangaza wakati wa usiku kwenye barabara za mijini na barabara za kasi. Bw. Li Zhihong ana imani kubwa kuhusu mstakabali wa masoko ya zana hizo za udhibiti wa matumizi ya umeme. Alisema, ifikapo mwaka 2010, pato kutokana na mauzo ya zana za aina hiyo ya udhibiti wa matumizi ya umeme litafikia Yuan bilioni 30.

China ni nchi yenye upungufu mkubwa wa rasilimali ya maji, hususan katika sehemu ya kaskazini mwa nchi hiyo. Hivi bidhaa na teknolojia ya udhibiti wa matumizi ya maji zinafuatiliwa sana na washiriki wa maonesho.

Kuosha kilo zaidi ya 200 za mboga kwa tani 1 tu ya maji, tena maji hayo yanatumika siku moja nzima bila kubadilishwa, tena mboga ni safi baada ya kuoshwa, jambo hilo linalochukuliwa kuwa ni jambo lisilowezekana na watu wengi, lakini limewezekana kwa kutumia mitambo inayojiendesha ya kuosha mbofa kwa kutumia hewa ya ozone. Mfanyakazi wa kampuni hiyo anayeshughulikia mauzo ya mitambo ya aina hiyo aliwasha mtambo wa kuosha mboga, huku akiwaeleza watazamaji, alisema, mtambo huo unatumia teknolojia ya kusafisha maji yaliyokwisha tumika pamoja na teknolojia za ultraviolet radiation, kuua vijidudu kwa hewa ozone na kuchuja uchafu ulioko katika maji kwa active carbon. Mitambo hiyo inaleta ufanisi mzuri katika udhibiti wa matumizi ya maji, hivyo imeagizwa na idara nyingi za serikali pamoja na kampuni nyingi zikiwemo wizara ya usalama na hotali ya Beijing.

Kubadilisha uwanja wa kuwekea takataka kuwa bustani ni jambo linalopendwa na watu, tena linaendana na wito uliotolewa na serikali ya mji wa Beijing wa kuandaa michezo ya Olinpiki ya kijani na kubadilisha 96% ya takataka za mjini kuwa vitu visivyotoa uchafuzi. Teknolojia iliyooneshwa na kampuni ya teknolojia ya hifadhi ya mazingira mjini Beijing kwenye maonesho ya safari hiyo inachangia utimizaji wa lengo hilo. Mkurugenzi wa ofisi ya kampuni hiyo bibi Cao Yang alisema, teknolojia hiyo ya usafishaji ni pamoja na kuchambua takataka na kuzitenganisha kwa mbalimbali, na takataka zilizokwisha safishwa, zinaweza kutumika tena katika ujenzi wa majengo. Bibi Cao Yang alisema, teknolojia hiyo inafuatiliwa idara husika ya serikali ya mji wa Beijing. Aliongeza, "Kampuni yetu hivi sasa inawasiliana na serikali, na tumepewa mradi mmoja katika wilaya ya Fengtai, ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Sisi tutafanya utafiti na kuvumbua teknolojia mpya inayoendana na hali halisi ya China kutokana na maendeleo ya usafishaji takataka, tunaona teknolojia hiyo itakuwa na mstakabali mzuri."

Habari zinasema, mradi aliotaja bibi Cao Yang ni mradi wa ushirikiano kati ya kampuni hiyo na wilaya ya Fengtai, ukiwa ni pamoja na kutumia teknolojia ya usafishaji takataka kurekebisha uwanja mkubwa wa kuwekea takataka kuwa bustani yenye kijito, msitu mdogo, ardhi inayopandwa majani na aina ya nyasi ndefu.

Ili kuunga mkono maendeleo ya kampuni za teknolojia ya udhibiti wa matumizi ya nishati, serikali ya Beijing itatumia teknolojia hizo katika ujenzi wa majengo ya michezo ya Olimpiki, majengo ya umma na viwanda vinavyotumia nishati kwa wingi.

Idhaa ya kiswahili 2006-07-11