Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-21 18:27:28    
Wasikilizaji wasifu matangazo ya CRI 91.9 FM Nairobi Kenya

cri

Tarehe 27 Februari mwaka huu, matangazo ya CRI 91.9 FM yalianzishwa rasmi huko Nairobi Kenya. Hiki ni kituo cha kwanza cha matangazo ya FM kilichoanzishwa na Radio China kimataifa katika nchi ya nje. Karibu nusu mwaka umepita tangu kituo hiki kianzishe matangazo yake kwenye wimbi la FM, kituo hiki kinaendeshwa vizuri na kimesifiwa kwa kauli moja na watu wa pande mbalimbali nchini Kenya.

Katibu wa Ikulu ya Kenya anayeshughulia uhusiano wa kiumma ambaye pia ni msemaji wa serikali ya Kenya Bwana Alfred N. Mutua alipohojiwa na waandishi wetu wa habari alisifu sana kuanzishwa kwa CRI 91.9 FM na matangazo yake mazuri huko Nairobi Kenya. Alisema:

Kuanzishwa kwa matangazo ya CRI 91.9 FM Nairobi Kenya ni jambo la kufurahisha, ambalo linazifanya nchi mbili Kenya na China ziwe karibu zaidi katika mambo ya utamaduni, tunafurahia sana. Tuna furaha ya kusikiliza sauti kutoka China, sauti hiyo inawaletea wananchi wa Kenya mawazo mapya, na kuwawezesha wananchi wa Kenya wapate hisia walizo nazo wananchi wa nchi nyingine.

Matangazo ya CRI 91.9FM yanarushwa hewani kwa kupitia kituo cha matangazo cha Shirika la utangazaji la Kenya KBC kilichoko Limuru. Meneja mkuu wa Shirika la KBC Bwana Hezekiel Oira aliwaelezea hali ya matangazo ya CRI 91.9 FM katika nusu mwaka uliopita tangu yaanze kurushwa hewani, akisifu ushirikiano wa aina hiyo kati ya Shirika la utangazaji la Kenya KBC na Radio China kimataifa. Alisema:

Kuna uhusiano wa kirafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Radio China kimataifa na Shirika la utangazaji la Kenya, tangu matangazo ya CRI 91.9 FM yaanze kurushwa, sauti ya matangazo ni safi sana, vipindi vyake vinahusu sekta mbalimbali, wananchi wa Kenya wanavipenda sana. Maingiliano na ushirikiano kati ya Shirika la utangazaji la Kenya na Radio China kimataifa utasukuma mbele maingiliano ya kiutamaduni na mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya CRI 91.9 FM yanasikika huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya wenye idadi ya watu milioni 2 hivi. Tokea matangazo hayo yaanze kurushwa hewani, vipindi vya matangazo ya Radio China kimataifa vinapendwa sana na wasikilizaji wake wengi. Dereva Thomas Naliyek ni msikilizaji mtiifu wa matangazo ya CRI 91.9 FM. Alisema:

Ninapoendesha gari nasikiliza mara kwa mara matangazo ya Radio China kimataifa, vipindi vyake vingi vinahusu Kenya na China. Nafurahi sana kuweza kusikiliza matangazo kutoka China, nitaendelea kusikiliza kila mara.