Sherehe ya kuchangia dola za kimarekani laki tano kwa makao makuu ya sekretarieti ya mpango wa ushirikiano mpya wa maendeleo ya Afrika NEPAD kutoka kwa serikali ya China ilifanyika tarehe 26 mwezi Juni huko Johannesburg nchini Afrika ya kusini, fedha hizo zitatumiwa katika mradi wa kutoa mafunzo kwa wauguzi na wakunga wa shahada ya pili wa nchi za Afrika.
Kwenye sherehe hiyo balozi wa China nchini Afrika ya kusini Bwana Liu Guijin alisema, waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao alipofanya ziara barani Afrika mwezi Juni mwaka huu alitangaza rasmi kuwa China itagharamia mradi wa mpango wa ushirikiano mpya wa maendeleo ya uchumi barani Afrika, kwa kutoa mafunzo kwa wauguzi ili kusaidia kuinua kiwango cha afya za wanawake na watoto wa Afrika. Sherehe hiyo ilikuwa sehemu ya utekelezaji wa matokeo ya ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao barani Afrika. Alisema mradi wa kutoa mafunzo kwa wauguzi na wakunga wa shahada ya pili kwa nchi za Afrika si kama tu unalenga kutoa mafunzo kwa wauguzi na wakunga wenye sifa bora kwa nchi zinazohusika, bali pia ni kuwachagua wanafunzi hodari wawe walimu ili kuanzisha hatua kwa hatua utaratibu wa utoaji mafunzo kwa wauguzi na wakunga wa shahada ya pili katika vyuo vikuu vitano. Mradi huo umeanzisha ushirikiano halisi kati ya China na mpango wa ushirikiano mpya wa maendeleo ya kiuchumi barani Afrika NEPAD.
Bwana Liu Guijin alisema, kwa kuwa mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika mwezi Novemba mwaka huu, serikali ya China itachukua hatua mwafaka zaidi katika kuzisaidia nchi za Afrika, ili kuongeza ushirikiano halisi katika uhusiano mpya wa kiwenzi kati ya China na Afrika.
Mtendaji mkuu wa NEPAD Profesa Mucawelai alihudhuria kwenye sherehe hiyo, na kusaini cheti cha kupokea msaada. Profesa huyo aliishukuru serikali ya China kwa msaada huo, alisema kutokana na kihistoria, serikali ya China siku zote inashikilia kuziunga mkono nchi za Afrika katika mapigano dhidi ya ukoloni na ubaguzi wa rangi ili kujikomboa, hivi sasa China inaendelea kutoa msaada kwa mpango wa ushirikiano mpya wa maendeleo ya kiuchumi barani Afrika wenye lengo la kuleta maendeleo ya uchumi na jamii ya Afrika. Jambo hilo linaonesha vya kutosha moyo wa kuwa na urafiki, ushirikiano na mshikamano kati ya China na nchi za Afrika. Profesa alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika si kutupia macho tu rasilimali na soko la Afrika, bali pia umetoa uwekezaji wa vitega uchumi vingi katika sekta zinazoleta maendeleo ya jamii, na kutoa mchango mkubwa katika kusaidia kutoa mafunzo ili kuwaandaa watu wenye ujuzi, na kuinua uwezo wa nchi za Afrika wa kujiendeleza.
Bw. Mucawelei alisema, nchi za Afrika zinathamini uhusiano wa kimkakati na kiwenzi kati yao na China, na zinapenda kushirikiana na China ili kusukuma mbele ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili, na kupata matokeo mengi halisi. Pia aliwataka waandishi habari wa Afrika wafanye utafiti kabla ya kutangaza kuhusu uhusiano kati ya Afrika na China, wala siyo kukariri peke yake habari zenye athari mbaya zinazotolewa na nchi za magharibi.
Kutokana na hali duni ya matibabu, kiasi cha vifo vya akina mama wajawazito barani Afrika ni mara 200 kuliko kile cha nchi za Ulaya, vifo vya wajawazito vilifikia asilimia 5. Mradi wa kutoa mafunzo kwa wauguzi na wakunga unalenga kupunguza hali hiyo.
Habari zinasema mradi huo kwanza utatekelezwa kwa majaribio katika vyuo vikuu vitano vya Tanzania na Kenya vyenye somo la wauguzi na wakunga wa shahada ya kwanza, kuanzisha somo la shahada ya pili ya miaka mitatu, na kutoa mafunzo kwa wauguzi na wakunga 50 wa shahada ya pili. Baada ya wanafunzi hao 50 kuhitimu masomo yao mwaka 2008, wale hodari watabaki vyuoni ili wawe walimu, ili kukamilisha hatua kwa hatua utaratibu wa mafunzo ya shahada ya pili katika vyuo vikuu hivyo vitano. Na kumaliza hali ya wauguzi na wakunga wa nchi za Afrika kupaswa kujifunza shahada ya pili katika nchi za magharibi.
Vyuo vikuu hivyo vitano ni Kituo cha Matibabu cha Kikristo cha Kilimanjaro cha Chuo Kikuu cha Tumaini cha Tanzania; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Muhimbili; Chuo Kikuu cha Moi cha Kenya, Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na Chuo Kikuu cha Nairobi. Chuo Kikuu cha Kwa Zuru/Natal cha Afrika ya Kusini kitakuwa chuo kikuu kinachoshughulikia utekelezaji wa mradi huo.
Gazeti la the Herald la Zimbabwe muda si mrefu uliopita lilichapisha makala ikisema, ni kweli China imetupia macho nchi za Afrika ili kuimarisha maendeleo yake ya kiuchumi, lakini vitendo vyake ni tofauti na nchi za magharibi. Ni rahisi kwa wafanyabiashara wa China kuingia barani Afrika kwa sababu China inatilia maanani kufanya ushirikiano wa kiuchumi wa kunufaishana. China inafuata msimamo wa kushirikiana, na inatumai kuanzisha uhusiano wa kiwenzi kati yake na nchi za Afrika kwa njia ya kuanzisha makampuni ya ubia na miradi ya ushirikiano. Hivyo nchi za Afrika zinafurahishwa zaidi na China kuliko nchi za magharibi.
Makala hiyo ilisema, baadhi ya vyombo vya habari vinasingizia kuwa, bidhaa zinazotengenezwa nchini China zina sifa chini, vinakusudia kuwazuia watu wa Afrika wasifanye biashara na wachina. Ni kweli kwamba, baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China zina bei nafuu, lakini zinafaa sana kwa watu wenye mapato ya chini wa Afrika.
Makala hiyo inasema, wachina ni watu wenye busara, wanafanya utafiti kuhusu soko na uwezo wa ununuzi wa watu wa Afrika, halafu kuleta bidhaa zinazofaa kwa watu wa ngazi mbalimbali.
Idhaa ya kiswahili 2006-08-04
|