Katika siku 3 zilizopita, vikundi 17 kutoka sehemu ya Asia na bahari ya Pasifiki vilifanya mazoezi ya utoaji misaada baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi kwenye mji wa Shijiazhuang, kaskazini mwa China ili kuimarisha uwezo wa ushirikiano kati ya vikundi vya utoaji misaada vya kimataifa.
Mazoezi ya safari hiyo ya utoaji misaada baada ya tetemeko la ardhi yalifanyika kutokana na pendekezo la ofisi ya mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mambo ya kibinadamu, mazoezi ya aina hiyo yaliwahi kufanyika mara 3, lakini hii ni mara ya kwanza mazoezi ya utoaji misaada baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi yaliyofanyika nchini China, ambayo yameshirikiwa na vikundi vingi vya kimataifa kutoka sehemu ya Asia na bahari ya Pasifiki, kufanyika nchini China.
Tokea Jumamosi iliyopita vikundi vya utoaji misaada kutoka nchi 17 zikiwemo China, Japan, Marekani, Australia, Philippines, Korea ya Kusini na India, vilifanya mazoezi katika hali ya kufanana na ya halisi yenye uharibifu mkubwa inayoletwa na tetemeko la ardhi, chini ya uratibu na ushirikiano wa ofisa wa Umoja wa Mataifa.
Ofisa wa ofisi ya mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mambo ya kibinadamu Bw. Arjun Katoch alisema, mazoezi yalitimiza lengo lililowekwa.
"Mazoezi hayo ya siku tatu ni nafasi nzuri sana kwetu. Katika muda huo, tulibuni matatizo mbalimbali tunayoweza kukabiliwa nayo katika mazingira ya maafa, kwa mfano suala la ushirikiano, suala la mawasiliano ya habari na suala la vipingamizi vya lugha. Naona mazoezi hayo yaliandaliwa vizuri sana na kufanikiwa."
Naibu mkurugenzi mkuu wa idara ya tetemeko ya ardhi ya China Bw. Zhao Heping alisema, China ni nchi iliyokumbwa na maafa mengi ya tetemeko la ardhi, na inahitaji sana kufanya mazoezi makubwa ya utoaji misaada ya kimataifa.
"Kufanya mazoezi ya sehemu ya Asia na bahari ya Pasifiki kuhusu tetemeko la ardhi nchini China, kunasaidia kukagua ushirikiano kati ya idara ya usimamizi ya kukabiliana na matukio ya dharura ya China na vikundi vya utoaji misaada vya kimataifa, kunakuza uwezo wetu wa kutoa misaada baada ya kutokea kwa maafa makubwa, kujifunza wazo na teknolojia ya kisasa ya vikundi vya utoaji misaada vya nchi za nje, na kutuwezesha kujiweka tayari kukabiliana na matukio ya dharura na kupunguza hasara inayoletwa na maafa."
Kikundi cha utoaji misaada duniani cha China kilishiriki kwenye mazoezi hayo. Mkurugenzi wa ofisi ya utoaji misaada baada ya kutokea maafa ya idara ya matetemeko ya ardhi ya China Bw. Huang Jianfa alisema, kikundi cha utoaji misaada duniani cha China kiliundwa mwaka 2001, na kilishiriki kwenye shughuli za utoaji misaada nchini Iran, Indonesia na Pakistan. China inatarajia kikundi hicho kitajifunza uzoefu wa kisasa wa vikundi vya nchi za nje kutokana na mazoezi hayo, na kuinua ufanisi wa kazi za kikundi hicho cha China.
Bw. Huang Jianfa alisema, "maafa makubwa yanaathiri sehemu fulani au dunia nzima. Katika siku za baadaye, ushirikiano huo wa kimataifa hakika utaimarishwa zaidi. Hivi karibuni, tutatuma kikundi cha utoaji misaada cha China kushiriki kwenye semina kamili nchini Singapore, licha ya hayo tumejenga kituo cha mafunzo cha utoaji misaada baada ya kutokea kwa maafa, tena tutaalika waalimu kutoka nchi za nje kufundisha nchini China, mbali na hayo tutatoa mafunzo ya teknolojia kwa nchi zinazoendelea ili kukuza uwezo wao wa kukabiliana na matukio ya dharura.
Ofisa wa ofisi ya mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mambo ya kibinadamu Bw. Peter Thomas alisema, katika miaka ya hivi karibuni serikali ya China ilitoa misaada mingi duniani baada ya kutokea matetemeko ya ardhi na kutoa mchango mkubwa kwa nchi zilizokumbwa na maafa, na anatarajia kuwa China itatoa mchango mkubwa zaidi duniani katika kukabiliana na matetemeko ya ardhi.
Idhaa ya Kiswahili 2006-08-09
|