Magharibi mwa Mkoa wa Hunan, katikati ya China ni sehemu inayowavutia sana watalii. Katika sehemu hiyo, kuna miji mingi ya kale ya makabila mbalimbali iliyojengwa katika sehemu yenye milima na mito yenye sura ajabu na ya kuvutia, miji hiyo ya kale ina mvuto mkubwa wa kikabila. Mji wa Liye ni moja ya miji hiyo.
Mji wa Liye uko kaskazini magharibi ya Mkoa wa Hunan, sehemu hiyo ni chimbuko la kabila la wa-Tujia. Kwa maana ya kichina, neno Liye ni uchimbaji wa ardhi. Mwaka 2002, katika mji huo mdogo wa wilaya, vilifukuliwa vipande vya mianzi zaidi ya elfu 36 vilivyoandikwa nyaraka za serikali ya Enzi ya Qin ya karne ya 2, kufukuliwa kwa vipande hivyo vya mianzi katika sehemu hiyo kulileta data nyingi zaidi kwa watu wa zama tulizo nazo kufanya utafiti juu ya Enzi ya Qin, pia kumeufanya mji mdogo wa Liye uwavutie watu zaidi. Mwongozaji wa watalii Bi.Tian Jing alisema:
Vipande hivyo vya mianzi vimeonesha kuwa binadamu waliishi sehemu hiyo kuanzia kati ya miaka laki moja na laki 5 iliyopita, vipande hivyo vya mianzi vilipofukuliwa vilikuwa vya rangi nyeusi-hudhurungi, baada ya kusafishwa kwa njia maalum, vipande hivyo vilionekana kama ni vipya, lakini maneno mengi yaliyoandikwa kwenye vipande hivyo vya mianzi hayaeleweki, lakini maandiko bado ni wazi.
Katika Mji wa kale Liye, hivi sasa bado kuna njia 7 na vichochoro 6 vilivyojengwa zamani za kale ambavyo bado vimebaki kikamilifu kama vile njia za Zhongfubeijie, Zhongfunanjie, Jiangxijie, na Daoxiangjie. Mjini humo kuna nyumba zaidi ya 500 za makazi ya raia, ujenzi wa nyumba hizo umeonesha mtindo wa jadi wa ujenzi wa majengo katika Enzi za Ming na Qing na mtindo wa ujenzi wa jadi wa majengo ya mbao ya kabila la wa-tujia, nyumba hizo zimekuwa na historia ya kati ya miaka 600 na 700. Ofisa wa mamlaka ya utalii ya Mji wa Liye Bwana Peng Daxian alisema, katika mji huo mdogo wa kale, kila njia ina mtindo wake na hadithi yake ambayo inawavutia sana watu. Alisema:
Kwa mfano, Njia ya Wanshou, hapo awali watu wa mkoa wa Jiangxi walifanya biashara huko, baadaye walijenga nyumba na kukaa huko, siku hadi siku wafanyabiashara waliongezeka na nyumba za makazi zilijengwa zaidi, sehemu hiyo ikawa njia moja, ambapo wakazi wa nyumba zilizojengwa huko wengi zaidi walitoka mkoa wa Jiangxi, hivyo wakazi wa huko waliita njia hiyo ni Njia ya Jiangxi.
Njia ya Zhongfu ni kama mstari wa katikati ya mji wa kale wa Liye, majengo mengi ya Njia ya Zhongfubeijie yameonesha zaidi mtindo wa ujenzi wa majengo ya kabila la wa-tujia. Jengo maarufu zaidi ni karakana kubwa ya kutia rangi ya ukoo wa Yangshi katika mji huo, ambalo lilisifiwa kuwa ni "Jengo kubwa ya kwanza katika sehemu ya kusini mwa Mto Changjiang". Jengo hilo lenye ghorofa mbili lilijengwa kwa mbao, mapambo ya michongo murua kwenye milango na madirisha yanaonesha kuwa jengo hilo ni "jengo kubwa la anasa" la hapo awali, na lilikuwa ambapo ndugu watatu wa ukoo wa Yangshi walifanya bidii kubwa kufanikisha biashara zao za kutia rangi katika sehemu ya kusini mwa Mto Changjiang. Mama mzee Peng Guiju mwenye umri wa miaka 83 ambaye ni mtu wa ukoo wa Yangshi alipoeleza biashara iliyong'ra ya karakana kubwa ya kutia rangi hapo zamani alisema:
Katika jengo hilo kila ndugu alikuwa na vyumba vitatu kwenye ghorofa moja, hivyo ndugu watatu wa ukoo wa Yangshi walikuwa na vyumba 9 kwenye ghorofa tatu za jengo hilo, kila mmoja alishughulikia kazi ya kutia rangi vitambaa, wengine walituletea vitambaa vyeupe, tulitia rangi vitambaa hivyo kuwa vitambaa vya kibluu au kijani-nyeusi.
Katika historia, Mji wa Liye ulisifiwa kuwa ni "mji mdogo wa Nanjing", ambapo Mto Youshui mjini humo umeufanya mji huo mdogo uwe mji wenye pilikapilika za biashara. Mjini humo kila njia inaelekea kwenye gati, na kwenye kando mbili za njia kuna maduka mengi makubwa na madogo ambayo yanaegemeana, majengo mengi ni ya mbao, na kwenye milango na madirisha ya majengo hayo kuna mapambo ya michongo ya aina mbalimbali inayopendeza, michongo hiyo ya picha za maua, majani na wanyama ni kama alama za heri na baraka. Na kila baada ya nyumba kadhaa kuna ukuta mmoja mrefu wa kukinga moto, hata ukuta huo ulijengwa kwa mtindo pekee, paa zake zina mapambo na pembe pamoja na michoro, ambao unaonekana kuwa ni ukuta wa heshima wenye mapambo mazuri. Bibi Peng Huifang anayependa kutalii kwenye sehemu hiyo alisema:
Tukifika kwenye sehemu hiyo tunaweza kujihisi hali nzito ya zama za kale, hata tunaweza kuona kuwa tumefika kwenye zama tofauti.
Baada ya kupita njia hizo za kale na kufika kando ya Mto Youshui?ambao ni mto wenye uso mpana, kando mbili za mto huo ni milima mirefu. Kwenye mto huo meli za uvuvi zinapitapita kila mara, hali kadhalika mashua za watalii. Mtalii kutoka mkoa wa Hubei Bi. Wei Xiaoming alisema, baada ya kufika kwenye Mji wa Liye anaona kupiga makasia na kuendesha mashua kwenye Mto Youshui ni jambo la kuburudisha. Alisema:
Nilipanda mashua na kupiga makasia mwenyewe, hivyo niliona raha sana. Siku ile jioni nilipanda mashua kwenye mto, ambapo mwezi ulichomoza, niliona kwenye milima iliyoko mbali pia kuna nyumba zilizojengwa kale, na kwenye kando mbili za mto kulikuwa na watalii wengi waliokuwa wanatembea, na mimi nilipiga makasia kwenye mashua, niliona maji ya mto ni safi, nilisikia raha mstarehe kweli.
Watalii wakifika kwenye Mji wa Liye, kama hawataweza kupata nafasi ya kuonja vyakula vya huko watasikitika sana, hasa Doufu iliyotengenezwa kwa unga wa mchele ya huko, ambayo ni chakula kinachojulikana sana magharibi ya Hunan. Na chakula kilichotengenezwa kwa unga wa ngano kiitwacho Yobaba pia kinapendwa sana na wakazi wa huko, pamoja na chakula cha figili chungu pia kinajulikana sana huko. Bi.Zhang Hengzhi kutoka Zhongqing alisema:
Nimefika kwenye Mji Liye unaojulikana katika sehemu ya magharibi ya Mkoa wa Hunan, nimepata kumbukumbu nyingi juu ya vyakula vya mji huo, naona vyakula vinavyojulikana zaidi vya mji huo kama vile Doufu iliyotengenezwa kwa unga wa mchele, chakula cha figili chungu na chakula cha Youbaba kweli ni vyakula vitamu zaidi, hata siwezi kuvisahau.
Idhaa ya kiswahili 2006-08-21
|