Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-05 16:40:53    
China yapiga vita kuingiza fedha haramu katika mzunguko wa fedha

cri

Wakati kamati ya kudumu ya bunge la umma la taifa inapokagua kwa mara ya pili mswada wa sheria ya kupambana kuingiza fedha haramu katika mzunguko wa fedha, tarehe 24 mwezi Agosti Benki ya Wananchi wa China, ambayo ni benki kuu ya taifa, ilitoa "taarifa kuhusu kupambana na vitendo vya kuingiza fedha haramu katika mzunguko wa fedha nchini China mwaka 2005". Taarifa hiyo inasema Benki ya Wananchi wa China itaendelea kutafuta mbinu ya usimamizi ya kupambana na kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha, kuendesha shughuli za benki kwa mujibu wa sheria, kugundua matukio makubwa ya uhalifu ya kutia fedha haramu katika mzunguko wa fedha na kuwaadhibu vikali wahalifu hao.

Hatua hii inamaanisha kuwa China inapiga vita uhalifu huo mpya wa kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha. Taarifa inasema katika mwaka 2005, idara za usalama, Benki ya Wananchi wa China na idara za usimamizi wa fedha za kigeni ziligundua maduka haramu 47 ya fedha pamoja na yale ya fedha za kigeni yanahusika na fedha za Renminbi Yuan zaidi ya bilioni kumi, kukamata fedha zenye thamani ya Yuan milioni zaidi ya 31; kukamata watuhumiwa 165, ambao walitozwa faini na fedha zao Yuan milioni zaidi ya 10 zilitaifishwa.

Kutokana na uchambuzi uliofanywa kutokana na matukio yaliyogunduliwa, kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha nchini China kuna umaalumu wa kipekee, hususan fedha zilizoingizwa kwenye mzunguko wa fedha na maduka haramu ya kisirisiri, ambayo yanawasaidia wahalifu kuhamisha fedha katika nchi za nje kwa mbinu ya kuingiza fedha katika mzunguko wa fedha na biashara ya fedha za kigeni, na kuwa moja ya njia za kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha kwa wala rushwa, wahalifu wakwepa kodi, biashara ya magendo na kuwatorosha watu katika nchi za nje.

Wataalamu husika wamesema hatua ya kisheria ni yenye ufanisi na muhimu zaidi ya kudhibiti uingizaji wa fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha. Hivi sasa China imejenga kwa hatua ya mwanzo mfumo wa kisheria wa kudhibiti uingizaji wa fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha na kufuata hatua kwa hatua vigezo vya kimataifa.

Mwezi Oktoba mwaka 2005, China iliidhinisha "Mkataba wa Kupambana Ufisadi wa Umoja wa Mtaifa", hatua ambayo inaonesha dhamira na azma ya kisiasa ya serikali ya China kushiriki kwenye harakati za kimataifa za kupambana na vitendo vya kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha na kubeba majukumu husika.

Pamoja na ongezeko la vitendo hivyo na mabadiliko yake, kiwango cha usimamizi wa kudhibiti vitendo vya kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha kinainuka kwa udhahiri kuliko miaka ya nyuma. Mwaka 2006 harakati za kupambana na vitendo hivyo nchini China ziliendelezwa kwa undani zaidi, na kupanuka hadi kuingia kwenye sekta za soko la hisa na bima kutoka sekta ya benki. Hivi sasa idara za usimamizi zitafuata kigezo cha kimataifa na kuboresha kanuni husika za usimamizi za sekta za bima na soko la hisa.

Takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2005, mitaji ya sekta ya benki nchini China ilichukua zaidi ya 90% ya jumla ya mitaji ya sekta ya mambo ya fedha, na sekta ya benki imekuwa sehemu muhimu ya muundo wa sekta ya mambo ya fedha nchini. Benki kuu ya taifa ni benki ya serikali, hivyo benki za biashara, mashirika ya utoaji mikopo ya sehemu ya vijiji na sehemu ya uwekaji akiba ya fedha ya posta zimethibitishwa kuwa ni idara muhimu zinazosimamiwa kwa udhibiti wa kuingiza fedha haramu katika mzunguko wa fedha.

Kanuni zilizorekebishwa na kutungwa na benki kuu ya taifa mwaka 2006 zinazojulikana kama "kanuni za kupambana na vitendo vya kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha za miundo ya mambo ya fedha ya sekta ya benki", "kanuni za kudhibiti vitendo vya kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha kwa miundo ya mambo ya fedha ya sekta za soko la hisa na bidhaa zitakazozalishwa" pamoja na "kanuni za kudhibiti vitendo vya kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha kwenye miundo ya mambo ya fedha ya sekta ya bima" zitatangazwa na kuanza kutekelezwa katika nusu ya pili ya mwaka huu, baada ya kusikiliza maoni ya watu wa sekta mbalimbali za jamii, mapambano dhidi ya vitendo hivyo yataendelezwa hadi kwenye sekta za soko na hisa na bima.

Habari zinasema pamoja na kuendelezwa kwa kina kwa harakati za kudhibiti vitndo hivyo, idara za usimamizi zitafuata kwa makini kigezo cha kimataifa cha kushughulikia vitendo hivyo na kuboresha zaidi kanuni za usimamizi za sekta za bima na soko la hisa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-09-05