Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-29 18:54:15    
Mkutano maalum wa maofisa waandamizi wa baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wafanyika Beijing

cri

Mkutano maalum wa maofisa waandamizi wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika tarehe 17 na 18 Septemba hapa Beijing. Wajumbe kutoka China na nchi 48 za Afrika pamoja na mabalozi wa nchi za Afrika nchini China walihudhuria mkutano huo, ambao walibadilishana maoni yao kuhusu namna ya kuandaa vizuri mkutano wa Beijing wa wakuu wa baraza hilo, kufanya mashauriano yenye usawa na kirafiki na kuafikiana katika mambo mengi. Katibu mkuu wa kamati ya maandalizi ya China ya mkutano wa viongozi wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika yaani mkutano wa 3 wa mawaziri, ambaye pia ni waziri msaidizi wa mambo ya nje wa China Bw. Zhai Jun kwenye ufunguzi wa mkutano huo alisema, huu ni mwaka wa 50 tangu China na nchi za Afrika zianzishe uhusiano wa kibalozi, mkutano wa viongozi utakaofanyika ni mkutano muhimu kabisa katika historia ya urafiki kati ya China na Afrika, na bila shaka utakuwa na athari kubwa kwa umoja na ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta mbalimbali.

Naye katibu mkuu wa kamati ya maandalizi ya China ya mkutano wa Beijing wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, ambaye pia ni naibu waziri wa biashara ya China Bw. Wei Jianguo alipotoa hotuba kwenye ufungaji wa mkutano huo alisema, kufanyika kwa mkutano wa Beijing wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ni uamuzi muhimu wa pande mbili za China na Afrika ili kuzidisha ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili.

Kwenye mkutano huo maalumu wa maofisa waandamizi, marafiki wa Afrika wametoa maoni na mapendekezo mengi kuhusu namna ya kuandaa vizuri mkutano wa wakuu, na kuweka msingi kwa ajili ya mkutano wa wakuu kufunguliwa bila vikwazo hapa Beijing. Amezitaka pande mbili za China na Afrika ziendelee kuimarisha majadiliano, kushirikiana vizuri, na kuufanya mkutano wa Beijing wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika na mkutano wa 3 wa mawaziri iwe mikutano mikubwa zaidi katika historia ya ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika.

Mjumbe maalum wa Ethiopia ambayo ni nchi mwenyekiti mwenza wa pamoja wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, ambaye pia ni balozi wa nchi hiyo nchini China Bwana Hairkilos alisema, tangu baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lianzishwe mwaka 2000, ushirikiano wa pande mbili na pande nyingi kati ya China na nchi za Afrika unaimarishwa siku hadi siku, na kudumisha hali nzuri ya maendeleo. Kwa mfano uaminifu wa kisiasa kati ya China na Afrika umezidishwa, thamani ya biashara inaongezeka mwaka hadi mwaka, na mawasiliano na ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, elimu, utamaduni, afya na nguvukazi zimepata mafanikio makubwa.

Naye mkuu wa mabalozi wa nchi za Afrika nchini China, balozi wa Cameroon nchini China Bwana Eleih-Elle Etian alisema, kufanyika kwa mkutano wa maofisa waandamizi kumeonesha kuwa nchi za Afrika na China zinatilia maanani sana kazi za maandalizi ya mkutano wa Beijing wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, na kufanyika kwa mkutano wa wakuu kumeonesha nia na imani ya pande hizo mbili kujenga uhusiano wa kiwenzi wa kunufaishana na wenye uhai mkubwa.

Aliyekuwa waziri wa habari na elimu ya umma wa Togo Bwana Koku Touzen hivi karibuni alipohojiwa na mwandishi wa habari wa China alisema, mkutano wa Beijing wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika unaotazamiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu utakuwa mkutano wa wakuu wenye umuhimu mkubwa, nchi za Afrika zinafuatilia sana mkutano huo.

Bw. Touzen alisema mkutano huo wa wakuu utazidisha uhusiano kati ya China na Afrika, ambao utakuwa sehemu muhimu siku hadi siku katika historia ya uhusiano wa kimataifa. Siku zijazo watu watakapozungumzia ushirikiano kati ya kusini na kusini bila shaka watataja baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. Bw. Touzen alisema, watu wa Afrika wanafahamu kuwa, China ni rafiki yao mkubwa, kwa sababu China inapenda kuzisaidia nchi za Afrika kwa udhati, na inatetea kudumisha uhusiano wenye usawa na nchi za Afrika. Alipotaja uhusiano kati ya China na Togo Bw. Touzen alisema, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili unaimarishwa siku hadi siku, China imekuwa injini muhimu inayohimiza maendeleo ya Togo.

Idhaa ya Kiswahili 2006-09-29