Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-16 18:07:14    
Mji wa kale wa Fenghuang

cri

Mji wa Fenghuang uko katika sehemu ya milimani ya jimbo linalojiendesha la makabila ya watujia na wamiao ya magharibi ya mkoa wa Hunan, China. Katika mamia na maelfu ya miaka iliyopita, mji huo wa kale ulioko kwenye sehemu ya milimani ulikuwa haujulikani kwa watu, hadi zaidi ya miaka 60 iliyopita, baada ya mwanafasihi na mtaalam wa elimu ya historia Bwana Shen Conwen aliyezaliwa huko kusimulia kwa hisia zake nyingi mji huo kwenye hadithi yake ya "Mji ulioko mbali", ndipo mji huo ulipoanza kujulikana nje na kusifiwa na watu kuhusu utulivu, usafi na uzuri wake.

Mji wa kale wa Fenghuang uko kwenye wilaya ya Fenghuang, mji huo unazungukwa na ukuta wa kale wenye historia zaidi ya miaka 400. Maana ya kichina ya jina la mji huo Fenghuang ni Phoenix, jina hilo lilitokana na mlima mmoja ulioko kusini magharibi ya wilaya ya Fenghuang ambao umbo lake linafanana sana na ndege Phoenix anayerukaruka. Wilaya ya Fenghuang ina wakazi zaidi ya laki 3, wengi wao ni wa kabila la wamiao na wa kabila la watujia.

Mji wa kale wa Fenghuang ulijengwa na vichochoro vingi, pembezoni kuna ukuta wa kale, Jumba la kale la kengele, gati la kale na mahekalu ya kale. Njia za vichochoro zilitandikwa vipande vya mawe vya rangi nyekundu nzito vilivyotengenezwa kwa miamba maalum ya zambarau ya huko. Kwenye kando mbili za njia kuna nyumba za kale zilizojengwa miaka zaidi ya mia moja iliyopita, ambazo vigae vya paa vya nyumba hizo vyote ni vya rangi nyeusi, na kuta zake ni za mbao yenye rangi ya kahawia, nyumba hizo zilipangwa vizuri na hali yake ya kiasili bado inaonekana dhahiri. Ingawa watalii walikuwa wengi wakati wa siku za mpukutiko, lakini walikuwa wakitembeatembea vichochoroni, hali ya utulivu bado inaonekana dhahiri.

Katika kichochoro kimoja cha kale, nyumba moja iliyofanana na nyumba ya kale ya Beijing ilikuwa ya mwanafasihi maarufu wa China Bwana Shen Conwen, nyumba hiyo imekuwa na historia ya zaidi ya miaka 150 ambayo ni nyumba ya kale ya huko mji wa Fenghuang.

Nyumba zilizojengwa juu ya nguzo ni majengo yenye mtindo dhahiri ya makabila ya wamiao na watujia. Nyumba hizo, upande wake mmoja uliegemea kando ya mto, upande mwingine unawekwa juu ya nguzo ya miti, nyumba moja baada ya nyingine zinaegemeana juu ya mto, ambazo zimekuwa mvuto mkubwa katika sehemu hiyo ya milima.

Katika mji wa Fenghuan kuna daraja moja lenye historia zaidi ya miaka 600, chini yake kuna duara, daraja hilo lilijengwa kwa miamba na majivu yaliyochanganywa na mchele laini. Daraja hilo lilidhoofishwa na upepo na mvua kwa miaka mingi, lakini bado liko madhubuti na imara.

Katika vichochoro vya mji wa kale Fenghuang, kuna maduka mengi ya kuuzia mazao ya kienyeji ya huko pamoja na mapambo murua ya watu wa kabila la wamiao. Mtalii mmoja kutoka kaskazini ya China alituambia:

Mjini Fenghuang mbali na majengo ya kale, wakazi wa huko pia wanaonekana kuwa ni watu wenye utulivu wanaofuata hali asilia ambayo ni nadra kuonekana katika miji mingine mikubwa. Napenda sana hali ya utulivu ya mji huo wa kale.

Idhaa ya kiswahili 2006-10-16