Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-18 11:22:08    
Chuo cha Confucius cha Seoul kitaingia katika kipindi kizuri katika ufundishaji wa lugha ya kichina

cri
Mkuu wa Chuo cha Confucius cha Seoul cha Korea ya Kusini Bw. Lee Jongyong alipoeleza hali ya ufundishaji wa lugha ya kichina nchini Korea ya Kusini alisema, "Walimu wanaona ni vigumu zaidi katika kufundisha kichina siku hadi siku nchini Korea ya Kusini."

Kadiri wanafunzi wa Korea ya Kusini wanaosoma nchini China wanavyoongezeka, na ufundishaji wa kichina nchini Korea ya Kusini unavyopata maendeleo kwa haraka, ndivyo walimu wa lugha ya kichina wa vyuo vikuu mbalimbali nchini Korea ya Kusini wanavyotambua kuwa kiwango cha kichina cha wanafunzi kimeinuka kwa kiasi kikubwa, na ndivyo walimu wanavyokabiliwa na shinikizo kubwa zaidi.

Bw. Lee Jongyong ni mtaalamu wa elimu ya lugha ya kichina anayejulikana nchini Korea ya Kusini, na alikuwa mwalimu wa lugha ya kichina katika Chuo Kikuu cha Gao Li. Yeye na balozi wa zamani wa Korea ya Kusini nchini China Bw. Kim Hoh-Jong walikuwa watu waliojifunza lugha ya kichina mapema zaidi nchini Korea ya Kusini, ambao walitoa mchango mkubwa kwa ajili ya mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Korea ya Kusini, na kushuhudia maendeleo makubwa ya ufundishaji wa kichina nchini Korea ya Kusini.

Bw. Lee Jongyong alisema kabla ya miaka ya 60 ya karne iliyopita, masomo ya kichina yalianzishwa katika vyuo vikuu vitatu tu nchini Korea ya Kusini kikiwemo chuo kikuu cha Seoul, na kila mwaka vyuo hivyo viliwaandikisha wanafunzi kumi kadhaa. Baada ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Korea ya Kusini na China, vyuo vikuu vilivyoanzisha masomo ya kichina viliongezeka na kuwa zaidi ya 100, na idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaojifunza kichina inafikia zaidi ya elfu 20 kwa mwaka, na hivi sasa idadi hiyo inazidi kuongezeka.

Bw. Lee Jongyong alipozungumzia sababu kuhusu kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaojifunza lugha ya kichina alisema, China na Korea ya Kusini zinatengwa kwa bahari, zote ziliathiriwa na nadharia ya Confucius, na nchi hizo mbili zinafanana kutokana na hali ya jiografia na utamaduni. Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili, kadiri biashara kati ya nchi hizo mbili inavyozidi kupanuka, ndivyo mahitaji ya jamii ya Korea ya Kusini kwa watu wanaofahamu kichina yanavyozidi kuongezeka, na mawasiliano na ufahamu kati ya nchi hizo mbili yanavyokuzwa, na ndivyo watu wa Korea ya Kusini wanaojifunza lugha ya kichina wanavyozidi kuongezeka.

Kutokana na hali hiyo, watu wanaoshiriki kwenye Mtihani wa kiwango cha lugha ya kichina HSK wanaongezeka kwa kiasi kikubwa. Mwaka 2001, watu walioshiriki kwenye mtihani huo walikuwa 6711, na idadi hiyo iliongezeka hadi kuwa elfu 26 mwaka 2005, na inatazamiwa kuzidi elfu 40 mwaka huu.

Kwa kufuata mkondo huo, chuo cha kwanza cha Confucius duniani kilianzishwa mwezi Novemba mwaka 2004 huko Seoul, Korea ya Kusini, na kilipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa serikali ya China na Taasisi ya ushirikiano wa utamaduni kati ya Korea ya Kusini na China nchini Korea ya Kusini. Ili kukidhi mahitaji ya watu mbalimbali ya kujifunza kichina, chuo cha Confucius cha Seoul kinatoa vitabu vya ufundishaji wa kichina kwa wanafunzi hao, kuwaandalia walimu wa lugha ya kichina, kuanzisha masomo ya kichina, na pia kuhimiza hatua kwa hatua elimu ya lugha ya kichina katika mtandao wa internet kutokana na hali ilivyo sasa ya elimu ya Korea ya Kusini.

Ili kueneza lugha ya kichina na kukidhi mahitaji ya watu wenye umri tofauti wanaojifunza lugha ya kichina, Chuo cha Confucius cha Seoul kimeanzisha elimu ya lugha ya kichina katika mtandao wa Internet. Kwenye tovuti ya mtandao wa Internet ya "Gazeti la Korea"linalochapishwa kwa kiasi kikubwa zaidi nchini Korea ya Kusini, chuo cha Confucius cha Seoul kilianzisha vipindi tofauti vya "lugha ya kichina inayotumiwa katika maisha" kinachoandaliwa kwa watu wazima na watoto. Kwenye "Gazeti la vijana wa Korea" linaloandaliwa kwa ajili ya shule za msingi nchini Korea ya Kusini, chuo cha Confucius cha Seoul kimeandaa kipindi maalum cha lugha ya kichina kwa watoto mara mbili kwa wiki ili kueneza masomo ya kichina. Wakati huo huo, chuo hicho pia kinatoa huduma ya kutoa mafunzo ya lugha ya kichina katika makampuni makubwa zaidi ya 20 ya Korea ya Kusini yaliyoanzisha shughuli zinazohusika na China.

Bw. Lee Jongyong ana imani kubwa akizungumzia mustakabali wa Chuo cha Confucius cha Seoul. Ifikapo mwaka 2007, wanafunzi elfu 60 wa shule za msingi na sekondari nchini Korea ya Kusini watajifunza lugha ya kichina katika madarasa 2000. Kikiwa chombo cha kuhimiza mafundisho ya lugha ya kichina na kueneza utamaduni wa China, Chuo cha Confucius cha Seoul kitaingia katika kipindi kizuri cha ufundishaji wa lugha ya kichina.

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-18