Mto Sichuan ni mto mdogo uliopo kusini magharibi mwa China. Kijiji cha Longjia kipo kando ya mto huo. Awali watoto wa kijiji hicho walilazimika kuvuka mto huo kwenda shule ya msingi iliyopo katika upande mwingine wa mto kwa vile ilikuwa hakuna daraja kwenye mto huo. Ili kukakikisha usalama wa watoto hao, mwalimu mwanamke Shi Yuanying alihuria kuchukua kazi ya kuwabeba watoto kuvuka mto huo. Na amekuwa akifanya hivyo kwa muda wa miaka 18.
Hapo awali shule ya msingi ya kijiji cha Longjia kilikuwa na uwezo wa kuwapokea watoto wa kidato cha kwanza na cha pili tu. Watoto wakimaliza masomo ya kidato cha pili, walikuwa wanapaswa kwenda shule nyingine kuendelea na masomo. Lakini shule nyingi zilikuwa mbali sana na kijiji hicho, watoto walikuwa wanapaswa kutembea milimani na mara kadhaa walikuwa na hatari ya kudhuriwa na nyoka wenye sumu. Kwa hiyo watoto wengi wa kijiji hicho waliomaliza masomo ya kidato cha pili waliamua kuacha masomo. Mkuu wa shule ya msingi ya kata ya Baoan kiliko kijiji cha Longjia kilipo Bw. Zhou Jianyun alisema, "Kati ya kijiji hicho na shule yoyote ile ya kata yetu kuna umbali wa kilomita zisizopungua 7, aidha njia za milimani zilikuwa mbaya. "
Kuna shule nyingine iitwayo Bamu iko upande mwingine wa mto Sichuan. Kwa kuvuka mto huo hakukuwa na dakika 10 tu kwenda shule hiyo, lakini wakati huo ilikuwa hakuna daraja kwenye mto huo. Nyumba ya Bibi Shi Yuanying ilikuwa katika kijiji hicho na mwaka 1987 alihamishiwa kwenye shule ya msingi ya Bamu, ambapo kuwabeba watoto kuvuka mto ilianza kuwa sehemu ya kazi yake.
Mwalimu huyo alikumbusha akisema "Si rahisi kuwabeba wanafunzi kuvuka mto. Mume wangu aliniambia kuwa unaweza kuwabeba mwenyewe ikiwa maji si mengi, na kama kina cha maji kiliongezeka nitakusaidia kuwabeba."
Katika siku za masomo bila kujalikama mvua inanyesha au upepo unavuma, mwalimu Shi Yuanying alikuwa ni daraja la uhakika kwa watoto hao, na mlinzi wa usalama wao. Dada Wang Manfei alikuwa mmoja miongoni mwa watoto hao, alikumbusha kuwa siku moja mwalimu Shi akimbeba, walipofika katikati ya mto jiwe moja lililotumika kama hatua lilivutwa na maji na kuacha pengo kubwa.
Alisema "Kuliacha pengo kubwa kutokana na kukosa jiwe moja. Maji yalikuwa na nguvu kubwa, mwalimu alikuwa akianguka na akapoteza viatu vyake."
Katika muda wa miaka 18 iliyopita, mwalimu Shi Yuanying alikuwa anawabeba watoto kuvuka mto huo. Watoto wengi wamemaliza masomo na kuondoka katika kijiji hicho cha mlimani.
Siku moja mwaka 1989 mwalimu Shi Yuanying alimbeba mtoto mmoja kuvuka mto. Walipofika mahali pa mita kadhaa tu mbali na kando, mafuriko yalikuwa yanawakaribia. Bibi Shi Yuanying alisema "Nilipombeba mtoto wa mwisho mafuriko yakakaribia kwa ghafla. Niliona maji ya mafuriko yalikuwa ni umbali wa mita 10 hivi, nilisikia hofu. Niliwaza kama nitaweza kushinda maji au nitashindwa?"
Kwa bahati nzuri Shi Yuanying aliepuka maji ya mafuriko, alifika kando ya mto huku mkondo wa maji kupita baada yake. Tukio hilo likampa kumbukumbu imara hata hivi sasa akilikumbusha anaona hofu. Baadaye mwalimu huyo alichunguza hali ya maji kabla ya kuwabeba watoto kuwavusha kwenye mto.
Kutokana na kuwabeba watoto kuvuka mto kwa miaka mingi, mwalimu Shi aliugua ugonjwa wa baridi yabisi, wakati hali ya ugonjwa ilipokuwa mbaya sana, alikuwa analazimika kulazwa kitandani kwa miezi mitatu. Hata katika kipindi hiki alipolazwa, mwalimu huyo aliwafuatilia wanafunzi wake, akiwa na wasiwasi kuwa huenda watoto hao wangesimamisha masomo kutokana na kushindwa kuvuka mto kwenda shuleni. Kutokana na hali hiyo mwalimu Shi Yuanying alikuwa anawafundisha watoto hao nyumbani kwake akilazwa kitandani.
Mwalimu mwezake Bw. Chen Yijian alisema (sauti 6) "Katika siku hizi ambapo aliposumbuliwa vibaya na ugonjwa alikuwa analazwa kitandani tu. Aliteswa na uchungu mkali kupita kiasi, hata hivyo alisema nafurahia kufanya hivyo kwa ajili ya wanafunzi wangu na kazi yangu."
Hivi sasa mwalimu Shi Yuanying ana umri wa miaka 50 hivi. Anakula mbio mwili tu wakati wa asubuhi na jioni, na amezoea kusahihisha kazi za nyumbani za wanafunzi na kuwasaidia wanafunzi wakati wa adhuhuri. Mwaka 2005 ujenzi wa daraja moja kwenye mto huo ulikamilika, hivi sasa watoto wanatumia daraja hilo kwenda shuleni. Hata hivyo kila siku mwalimu Shi Yuanying anashikilia kwenda na kuondoka shuleni pamoja na wanafunzi wake. Hivi sasa mwalimu huyo anambeba mwanafunzi mmoja mlemavu aitwaye Xiao Lunbing kwenda shuleni. Anatumai kuwa mwanafunzi huyo atapata elimu na kuwa mtu atakayelitumikia taifa. Mwalimu Shi Yuanying vile vile ana matumaini mengine kwamba wanafunzi wake wote wanaweza kuchangia maendeleo ya taifa, kujenga madaraja mengine mengi kwenye maskani yao ili maisha ya huko yawe mazuri zaidi siku hadi siku.
Idhaa ya kiswahili 2006-10-19
|