Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-25 20:08:17    
Chuo cha kwanza cha Confucius chaanzishwa nchini Italia

cri
China na Italia ni nchi zenye historia ndefu na utamaduni wa kale, na maingiliano ya utamaduni kati yao yamekuwa yakidumishwa katika muda mrefu uliopita. Katika miaka 200 iliyopita, mmisionari wa Italia Michele Ruggleri aliitambulisha kwa mara ya kwanza nadharia ya Confucius kwa nchi za magharibi. Tarehe 29, Septemba Chuo cha kwanza cha Confucius cha Italia kilianzishwa rasmi kwenye Chuo Kikuu cha Rome nchini humo.

Chuo cha Confucius kilianzishwa rasmi tarehe 29 mwezi Septemba kwenye Chuo Kikuu cha Rome, balozi wa China nchini Italia Bw. Dong Jinyi anasema:

"Chuo cha Confucius kinaanzishwa rasmi katika Chuo Kikuu cha Rome mwaka huu ambao ni mwaka wa 2557 tangu kuzaliwa kwa mwanafikra, na mwanaelimu maarufu wa China Confucius."

Miaka 200 iliyopita, mmisionari wa Italia alitambulisha kuhusu Confucius na nadharia yake kwa nchi za magharibi. Hivi sasa elimu ya Confucius imekuwa tena daraja maalum la mawasiliano ya utamaduni na nje wa China. Mashirika yote ya China yanayoshughulikia uenezi wa lugha ya kichina yaliyoanzishwa katika nchi za nje yanapewa jina la "Chuo cha Confucius". Hadi sasa vyuo karibu mia moja vya Confucius vimeanzishwa katika nchi na sehemu 36 duniani. Bibi Zhong Meisun ambaye ni mkuu wa Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing kinachoendesha Chuo cha Confucius kwa pamoja na Chuo kikuu cha Rome anasema:

"Hivi leo vyuo vya Confucius vilivyoanzishwa duniani na Wizara ya elimu ya China ni mashirika yanayodhamiria kufundisha lugha ya kichina na kueneza utamaduni wa China, ambapo madhumuni yake si kuchuma pesa. Vyuo hivyo vinafuata nadharia ya Confucius na kusukuma mbele maingiliano na mapatano ya utamaduni kati ya China na nchi za nje, ili kujenga dunia yenye masikilizano na amani ya kudumu, na kupata ufanisi wa pamoja."

Hivi sasa Chuo cha Rome ni chuo pekee cha Confucius nchini Italia. Chuo kikuu cha Rome kina historia ya miaka 700, na kina heshima kubwa nchini Italia na barani Ulaya. Chuo hicho kilianzisha masomo ya kichina mwanzoni mwa karne ya 20, na ni moja kati ya vyuo vikuu vilivyoanzisha mapema zaidi mafunzo ya lugha ya kichina nchini Italia.

Siku hiyo Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Rome kilipoanzishwa, wananchi wengi wa Italia wanaopenda lugha ya kichina waliuliza maswali mbalimbali kuhusu masomo ya Kichina. Kazi ya Antonio ambaye ni kijana wa Italia anayezungumza kichina vizuri ni kutoa misaada kwa watu hao. Akizungumzia sababu ya yeye kujifunza lugha ya kichina anasema:

"Napenda China, na kuna fursa nyingi za kupata ajira nchini China. Nilikwenda China mara nne, na kujifunza lugha ya Kichina kwa miezi mitatu katika Chuo Kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing. Natumai kwenda tena China mwaka 2008."

Msichana mwingine wa Italia anapendelea utafiti kuhusu lugha ya Kichina, anasema:

"Nimejifunza lugha ya kichina kwa miaka 8, nilihitimu kutoka Chuo cha Mashariki kwenye Chuo kikuu cha Rome, sasa nasomea shahada ya tatu. Nafurahi sana kushiriki kwenye sherehe za uzinduzi wa Chuo cha Confucius. Chuo hicho si kama tu ni muhimu kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya kichina, bali pia kwa watu wengine, kwa sababu nadharia ya Confucius ni mali kwa binadamu wote."

Kwa kufuata mchakato wa utandawazi wa dunia, ili kutafuta historia ya ustaarabu wa kale wa China, na kupata fursa za kujiendeleza nchini China, watu wengi zaidi wa nchi za nje wanaanza kujifunza lugha ya kichina na utamaduni wa China. Kama mkuu wa chuo kikuu cha Rome Bw. Renato Guarini anavyosema:

"Leo ni kituo cha mwanzo kwa mawasiliano na ushirikiano kati ya Italia na China. Tuna uhakika kuwa utamaduni na teknolojia zitatoa mchango muhimu kwa maendeleo ya jamii na amani ya binadamu."

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-25