Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-31 16:10:44    
Sehemu ya kusini magharibi mwa China yavutia uwekezaji kutoka nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki

cri

Tokea miaka ya 70 ya karne iliyopita, wafanyabiashara wenye asili ya China wa nchi mbalimbali za Umoja wa Asia ya kusini mashariki wamekuwa chanzo muhimu cha uwekezaji kutoka nchi za kigeni nchini China, ambao wametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa China. Katika muda mrefu uliopita, sehemu ya pwani ya mashariki ya China iliyoendelea kiuchumi ilikuwa shabaha ya kwanza ya wafanyabiashara wa nchi za Asia ya kusini mashariki. Lakini katika miaka ya karibuni, sehemu ya kusini magharibi, ambayo ilikuwa nyuma kimaendeleo kwa ikilinganishwa na sehemu nyingine za China, pole pole imekuwa sehemu inayowekezwa na wafanyabiashara wenye asili ya China.

Sehemu ya kusini magharibi mwa China ina eneo la kilomita za mraba milioni zaidi ya 2.5 na idadi ya watu milioni karibu 200, sehemu hiyo ambayo ina mikoa 6, ni sehemu yenye rasilimali nyingi na kituo cha nishati kwa sekta ya viwanda. Kutokana na vyanzo vya mazingira ya kimaumbile na kihistoria, sehemu ya kusini magharibi iko nyuma kimaendeleo. Katika miaka ya hivi karibuni serikali si tu kuwa ilitoa uungaji mkono mkubwa wa kifedha, pia inasaidia mikoa ya huko kuvutia uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni, hususan wafanyabiashara wenye asili ya China wa nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki.

Naibu mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya wachina wanaoishi nchi za nje ya baraza la serikali Bibi Li Haifeng alipoeleza hali husika alisema,

"Katika miaka ya hivi karibuni, ili kuhimiza utekelezaji wa sera za ufunguaji kwenye sehemu ya kusini magharibi, serikali ya China imetoa mfululizo wa sera nafuu na kuongeza nguvu ya uungaji mkono. Serikali za mikoa ya sehemu ya kusini magharibi pia zimetenga fedha nyingi mfululizo kwa ajili ya ujenzi wa miundo-mbinu na kuboresha mazingira ya uwekezaji. Miradi inayowekezwa na wafanyabiashara wenye asili ya China wa nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki inaongezeka mwaka hadi mwaka, ambapo fedha zilizowekezwa pia ziliongezeka kwa udhahiri. Hivi sasa wachina wanaoishi katika nchi za nje na wageni wenye asili ya China wamekuwa moja ya nguvu muhimu zinazohimiza maendeleo ya sehemu ya kusini magharibi."

Katika miaka ya karibuni, pamoja na kuharakishwa kwa ujenzi kwenye sehemu ya biashara huria kati ya China na nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili umeimarishwa zaidi. Sehemu ya kusini magharibi ya China inapakana na nchi nyingi za umoja wa Asia ya kusini mashariki, ambapo utamaduni kwenye sehemu hiyo karibu ni wa namna moja, hivyo kuna mazingira bora ya kukuza uhusiano wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara. Licha ya hayo hali ya kunufaishana katika miundo ya rasilimali na sekta ya uzalishaji mali pamoja na bidhaa za viwanda na mazao ya kilimo, inatoa nafasi kubwa kwa upanuaji wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara. Katika mazingira ya namna hiyo, uwekezaji wa wafanyabiashara wenye asili ya China kutoka nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki unaongezeka kwa mfululizo, na thamani ya uwekezaji inafikia dola za kimarekani bilioni kadhaa kwa mwaka.

Tokea mwaka 2003, kila mwaka serikali ya China inaitisha mkutano wa utoaji habari kwa ajili ya uwekezaji wa wafanyabiashara wenye asili ya China wa nchi za Asia ya kusini mashariki. Hivi sasa mkutano wa utoaji habari umekuwa kitu muhimu cha kuhimiza maendeleo kwa sehemu ya kusini magharibi ya China na wafanyabiashara wenye asili ya China wa nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki, na kupendwa sana na wafanyabiashara hao.

Mkutano wa nne wa utoaji habari kuhusu uwekezaji wa wafanyabiashara wenye asili ya China wa nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki, ambapo pia ni mkutano wa kwanza wa baraza la wafanyabiashara wa sehemu ya Asia na Pasifiki ulifanyika hivi karibuni kwenye mji wa Kunming, mji mkuu wa mkoa wa Yunnan ulioko kusini magharibi mwa China. Wawakilishi wa wafanyabiashara wenye asili ya China wa nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki pamoja na wawakilishi wa viwanda na kampuni za mikoa 6 ya sehemu ya kusini magharibi ya China zaidi ya 180 kwa jumla walishiriki kwenye mkutano huo. Naibu mkuu wa mkoa wa Yunnan ulioandaa mkutano huo Bw. Qin Guangrong alisema, mkoa wa Yunnan uko sehemu ya mpakani ya kusini magharibi mwa China, mkoa huo una ubora wa kijiografia kwa kupakana na nchi za Asia ya kusini mashariki na Asia ya kusini, hivyo mkoa huo unatarajia kuijenga Yunnan kuwa daraja la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya sehemu ya kusini magharibi mwa China na nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki. Alisema,

"Mkutano wa nne kuhusu uwekezaji wa wafanyabiashara wenye asili ya China wa nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki unatoa fursa kubwa kwa mkoa wa Yunnan kutumia ubora wa kijografia, kupanua ufunguaji, kuharakisha maendeleo, kuijenga Yunnan kuwa nyumbani kwa wafanyabiashara wenye asili ya China wa Asia na sehemu ya Pasifiki, na kuimarisha hadhi ya Yunnan kwenye sehemu ya Asia ya Pasifiki. Tunaamini kuwa kufanikiwa kwa mkutano huo, kutaiwezesha Yunnan kuwa muhimu katika ushirikiano na maingiliano kati ya China na sehemu ya Asia na Pasifiki, na kujenga daraja la dhahabu la urafiki na kunufaishana kati ya nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki na kwa ushirikiano wa sehemu ya kusini magharibi mwa China."

Takwimu zinaonesha kuwa, wafanyabiashara wenye asili ya China zaidi ya 500 kutoka nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki walishiriki kwenye mikutano mitatu iliyopita kuhusu uwekezaji kwenye miradi ya sehemu ya kusini magharibi ya China, na thamani ya uwekezaji uliotiwa saini ni dola za kimarekani karibu bilioni 1.2. Thamani ya uwekezaji na mafanikio ya mkutano wa mwaka huu, vyote vimezidi vile vya mikutano mitatu iliyopita, katika muda wa siku mbili, makubaliano 36 yalifikiwa kuhusu miradi ya ushirikiano, na thamani ya miradi hiyo ni kiasi cha dola za kimarekani bilioni 1.7.

Takwimu hizo zinaonesha hamasa ya wafanyabiashara wenye asili ya China katika uwekezaji, na kuona hisia zao za kutoa misaada kwa nchi ya asili yao. Pamoja na maendeleo ya utandawazi wa uchumi na umoja wa uchumi wa kikanda, uhusiano wa kutegemeana kati ya China na nchi zilizoko karibu na China unaongezeka siku hadi siku. Wafanyabiashara wenye asili ya China wanatoa mchango mkubwa katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi zilizoko karibu.

Mfanyabiashara mwenye asili ya China kutoka Singapore Bw. Gao Xinping alipozungumzia wazo lake la kuwekeza kwenye sehemu ya kusini magharibi mwa China alisema,

"Nilianza kuwekeza China bara miaka mingi iliyopita, hapo zamani niliwekeza kwenye sehemu ya pwani ikiwemo Fujian, Jiangsu na Shanghai. Safari hii nimepata nafasi ya kufika sehemu ya kusini magharibi. Harakati za kustawisha sehemu ya magharibi zilianza miaka michache iliyopita, uchumi wa China umepata maendeleo ya kasi, sisi watu wenye asili ya China tuna matarajio kuwa China itaimarika na kustawi zaidi."

Naibu mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la taifa Bw. Luo Haocai alipongeza watu wenye asili ya China waliotoa mchango kwa maendeleo ya uchumi wa China. Alisema kuna milioni makumi kadhaa ya watu wenye asili ya China, ambao wanaishi katika sehemu mbalimbali duniani. Licha ya kutoa mchango kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi walizoko, pia wanatoa mchango muhimu kwa uchumi na ujenzi wa China. Bw. Luo aliongeza kuwa, China itaharakisha ushirikiano na nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki, na itatoa fursa nzuri kwa maendeleo ya wafanyabiashara wenye asili ya China.

Idhaa ya kiswahili 2006-10-31