Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-02 21:41:00    
Ujenzi wa kituo cha mambo ya fedha

cri

Shanghai inajitahidi kujenga mji huo uwe kituo cha mambo ya fedha duniani, na hivi sasa imepata maendeleo makubwa. Shanghai ina mfumo kamili wa soko la mambo ya fedha wenye idadi kubwa ya wataalamu na uwezo mkubwa wa kuunganisha masoko ya mambo ya fedha ya sehemu zilizoko pembezoni mwake.

Baada ya kujiendeleza na kufanya uvumbuzi kwa miaka zaidi ya 20, hivi sasa Shanghai imekuwa na mfumo mkubwa kamili wa mambo ya fedha wenye masoko ya sarafu, mitaji, fedha za kigeni, bidhaa zitakazozalishwa katika kipindi cha baadaye, dhahabu na haki-miliki za kiujuzi. Takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2005, jumla ya thamani ya biashara iliyofanyika kwenye soko la mambo ya fedha la Shanghai ilikuwa Yuan trilioni 35 ikiwa ni ongezeko la mara 5.2 kuliko ile ya mwaka 2001. Kati ya hizo thamani ya biashara kwenye soko la hisa ilikuwa Yuan trilioni 5 zikiwa ni 79% ya ile ya China nzima; Thamani ya biashara ya bidhaa zitakazozalishwa ilikuwa Yuan trilioni 6.5 zikiwa ni 49% ya ile ya China; Thamani ya biashara ya kati ya benki ilikuwa Yuan trilioni 23.2; Thamani ya biashara ya soko la dhahabu ilikuwa Yuan bilioni 116.8; Wakati thamani ya biashara kwenye soko la fedha za kigeni inaongezeka hatua kwa hatua. Soko la fedha za kigeni la Shanghai ni soko muhimu linaloamua kiasi cha ubadilishaji wa fedha za Renminbi kwa fedha za kigeni.

Shanghai inachukua nafasi ya kwanza nchini China kwa wingi wa mashirika ya mambo ya fedha ya nchi za kigeni, ambapo licha ya benki za biashara za China kujenga matawi yake, mashirika ya mambo ya fedha zaidi ya 300 ya nchi za kigeni yakiwa ni pamoja na National city Bank of New York, Benki ya Marekani na Benki ya Uswisi. Takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, Shanghai ilikuwa na mashirika ya fedha ya aina mbalimbali zaidi ya 610 ikiwa ni pamoja na benki 231, kampuni za hisa 110 na kampuni za bima 269; ambazo jumla ya mitaji yake imezidi 50% ya jumla ya mitaji ya benki za kigeni zilizoko nchini China, na jumla ya mitaji ya kampuni za bima za nchi za kigeni imefikia 30% ya jumla ya mitaji ya kampuni za bima za nchi za kigeni zilizoko nchini China. Jumla ya mitaji ya sekta ya mambo ya fedha ya Shanghai imefikia Yuan trilioni 3.2, zikiwa ni kiasi cha 9% ya China nzima.

Uzoefu wa kimataifa unaonesha kuwa, sharti moja muhimu la kujenga kituo cha mambo ya fedha cha kimataifa ni kupanua uwezo wa kujiamulia mambo na uvumbuzi katika mambo ya fedha. Kwa kawaida kituo cha mambo ya fedha cha kimataifa ni mahali penye uvumbuzi mwingi wa mambo ya fedha kwa nchi moja. Shanghai inapoendeleza ujenzi wa kituo cha kimataifa inazingatia sana uvumbuvi wa China katika mambo ya fedha. Mji wa Shanghai unaongoza katika mazingira ya kuendelezwa mageuzi ya mambo ya fedha kote nchini China, na kuharakisha hatua za uvumbuzi wa mambo ya fedha. Hivi sasa mji wa Shanghai unaongoza kwa wingi wa aina za mambo ya fedha nchini China.

Tarehe 20 mwezi Desemba mwaka 2005, kampuni ya Shanghai International Trust ikishirikiana na kampuni ya Tullett Prebon ya Uingereza zilianzisha kampuni ya kwanza ya wakala wa biashara sarafu nchini China. Mwaka 2005 ongezeko la nyongeza ya thamani ya uzalishaji mali ya sekta ya mambo ya fedha ya Shanghai ilikuwa karibu Yuan milioni 690. Umuhimu wa sekta ya mambo ya fedha katika maendeleo ya uchumi na kuboresha uwezo wa mji ulithibitishwa kabisa, ambayo inahamasisha maendeleo ya uchumi na sekta ya mambo ya fedha ya sehemu ya delta ya mto Changjiang.

Idhaa ya kiswahili 2006-11-02