Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-17 21:04:01    
Ushirikiano kati ya China na Zambia

cri

Kutokana na kuhimizwa na wimbi la utandawazi wa uchumi, katika miaka ya hivi karibuni baadhi ya wanaviwanda wa China walikwenda kuwekeza katika nchi za nje, Bw. To Xinghu meneja mkuu wa tawi la Afrika la kampuni ya madini ya China ni mmoja kati yao. Kutokana na uongozi wake kampuni hiyo ya madini katika miaka michache iliyopita ilishiriki kwa juhudi kwenye uendelezaji wa mgodi wa shaba wa Chembezi nchini Zambia na kuwa mfano mzuri wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Zambia.

Afrika ni bara lenye rasilimali nyingi za madini duniani. Ukanda wa shaba iliyoko sehemu ya mpakani kati ya Zambia na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo una urefu wa kilomita zaidi ya 200 na upana wa kilomita 65, unachukua nafasi ya 3 kwa ukubwa duniani. Madini ya shaba ni nguzo ya uchumi wa Zambia, ambayo inaleta 80% ya pato la fedha za kigeni kwa nchi hiyo. Lakini uzalishaji shaba wa Zambia ulishuka hadi kufikia tani laki 3 katika kipindi cha kati cha miaka ya 90 ya karne iliyopita kutoka tani zaidi ya laki 7 katika kipindi cha kati ya miaka ya 70 ya karne ya 20.

Ili kustawisha uzalishaji mali wa migodi ya shaba, mwishoni mwa karne iliyopita serikali ya Zambia iliiuza migodi ya shaba kwa kampuni za kigeni. Katika mazingira hayo, kampuni ya madini ya China ilipata 85% ya hisa ya mgodi wa shaba wa Chembezi kwenye zabuni ya mwaka 1998. Katika miaka michache iliyopita, tawi la Afrika la kampuni ya madini ya China lilishinda shida mbalimbali na kuanza upya shughuli za uchimbaji wa shaba tarehe 28 mwezi Julai mwaka 2003. Rais Levy Mwanawassa wa Zambia alishiriki kwenye sherehe ya uzinduzi na kutoa pongezi kwa kufufuliwa kwa mgodi wa shaba wa Chembezi.

Mgodi wa shaba wa Chembezi ni mradi wa kwanza wa ujenzi ulioidhinishwa na serikali ya China kutekelezwa katika nchi za nje, na pia ni mradi wa kwanza kwa ukubwa wa China nchini Zambia. Katika miaka michache iliyopita, tawi la Afrika la kampuni ya madini ya China lilipata maendeleo ya kufurahisha. Madeni ya tawi hilo yalishuka hadi 48.1% kutoka 71.7%, ambapo faida ya kampuni iliongezeka kwa 96.4%, wastani wa uzalishaji uliongezeka kwa 25%, na jumla ya faida ya kampuni hiyo imefikia dola za kimarekani milioni 46.

Kwa kufuata nafasi nzuri ya kupanda kwa bei ya shaba kwenye soko la kimataifa hivi sasa na kuongeza nguvu ya ushindani duniani ya kampuni ya shaba, kampuni hiyo ya shaba kwa kuungwa mkono na serikali za China na Zambia imeanzisha ujenzi wa eneo la viwanda la China huko Chembezi. Hivi sasa eneo hilo limekuwa na viwanda vya ukarabati wa mitambo na kushughulikia maji machafu, na jumla ya thamani ya uzalishaji mali imefikia Renminbi Yuan milioni 580.

Ujenzi wa eneo la viwanda, si tu kuwa umetumia vilivyo ardhi na miundo-mbinu iliyopo hivi sasa ya maji, umeme na barabara na kupanua wigo wa uzalishaji mali kwa sasa, bali pia unatoa mchango muhimu kwa ajili maendeleo ya jamii, uchumi na utamaduni wa huko. Mgodi wa shaba wa Chembezi na eneo la viwanda la China vimetoa nafasi zaidi ya 2,500 za ajira na kulipa kodi ya dola za kimarekani zaidi ya milioni 10 kwa serikali ya huko.

Hivi sasa uzalishaji shaba wa Zambia unaongezeka na kufikia tani laki 4.4 kwa mwaka, ambazo ni kiwango cha mwaka 2005. Inatarajiwa kuwa uzalishaji shaba utafikia tani laki 7 mwaka 2010, ambazo ni kiwango cha juu kabisa kwenye historia yake, na utaongezeka zaidi hadi tani laki 9 kwa mwaka katika mwaka 2015. Kufufuka kwa uzalishaji shaba wa mgodi wa Chembezi kunahimiza ustawishaji uchimbaji madini na maendeleo ya uchumi ya Zambia. Mwezi Aprili mwaka 2006, kampuni ya madini ya China ilisaini kumbukumbu pamoja na kampuni 3 za Zambia kuhusu kuendeleza uchimbaji wa madini kwa ushirikiano, na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Zambia utaimarishwa hatua kwa hatua.

Idhaa ya Kiswahili 2006-11-17