Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-21 16:21:21    
Kuimarisha uvumbuzi kwahitaji kuhimiza uwekezaji unaoweza kukabiliana na hatari na ujenzi wa soko la mitaji

cri

Waziri wa sayansi na teknolojia ambaye ni mjumbe wa taasisi ya sayansi ya China, Bw. Xu Guanhua amesema, kuimarisha uwezo wa uvumbuzi kunatakiwa kuhimiza uwekezaji wenye uwezo wa kukabiliana na hali ya hatari na ujenzi wa soko la mitaji ili kuimarisha uwezo wa uvumbuzi wa kampuni na viwanda vya wastani na vidogo.

Bw. Xu alisema hivi sasa hitilafu iliyoko katika utaratibu wa wa soko la mitaji nchini imekuwa ni kitu kikubwa kinachokwamisha uunganishaji wa uvumbuzi wa kisayansi na mitaji. Kwa upande mmoja, kampuni na viwanda vingi vya wastani na vidogo vyenye uwezo wa uvumbuzi vinapungukiwa uungaji mkono wa mitaji. Kwa upande mwingine soko la mitaji halina mpango wa utaratibu wa kutoka kwa uwekezaji wenye uwezo wa kukabiliana na hali ya hatari, jambo ambalo linasababisha kuzorota kwa uwekezaji wa nchini wenye uwezekano wa kukabili hali ya hatari na upungufu wa uwekezaji kwa kampuni na viwanda vya teknolojia ya kisayansi, ambavyo bado havijaimarika.

Bw. Xu Guanhua alisema katika hali ya namna hiyo, ni vigumu kwa kampuni na viwanda vidogo vya teknolojia ya kisasa kupata maendeleo, na kufanya uvumbuzi wa China ukabiliwe na matatizo. Kutekeleza mkakati mpya wa uvumbuzi, kunahitaji soko la mitaji na uwekezaji wenye uwezekano wa kukabiliana hali ya hatari kufanya kazi muhimu ya kuunga mkono kampuni na viwanda vidogo. Kwanza ni kutumia uwezo wa soko la mitaji kuhimiza mageuzi ya utaratibu wa uwekezaji na ukusanyaji wa fedha za kuunga mkono maendeleo ya sayansi na teknolojia na utaratibu wa uhimizaji wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia. Pili, kutumia ipasavyo umuhimu mkubwa wa soko la mitaji wa kuhimiza maendeleo ya uwekezaji wenye uwezekano wa kukabiliana na hali ya hatari. Aliongeza kuwa bila kutumia soko la mitaji, njia ya kutoka kwenye soko kwa uwekezaji unaoweza kukabiliana na hatari haitaweza kuanzishwa na faida ya uwekezaji wa aina hiyo haitaongezeka kwa mfululizo. Tatu, ni uungaji mkono mkubwa wa mitaji wa soko la mitaji kwa kampuni na viwanda vipya vidogo ndio utaweza kuhimiza uvumbuzi.

Bw. Xu Guanghua alidokeza kuwa hivi sasa Benki ya Wananchi wa China, kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa, wizara ya fedha na wizara ya sayansi na teknolojia zinafanya utafiti na kubuni mbinu halisi za kisera za kuhimiza uwekezaji unaoweza kukabiliana na hatari na maendeleo ya soko la mitaji zikiwa ni pamoja na kuhimiza ujenzi wa mfumo wa soko la mitaji wa ngazi mbalimbali unaolenga kuhimiza uvumbuzi, na kuwa wakala katika uuzaji wa hisa. Pili, kuimarisha uelekezaji kwa uwekezaji unaoweza kukabiliana na hatari, na kuweka mfuko wa fedha wa taifa wa kushawishi uwekezaji unaoweza kukabiliana na hatari. Tatu, ni kuelekeza uwekezaji kushiriki kwenye mkakati mpya wa uvumbuzi wa China, kusaidia na kuhimiza kampuni na viwanda vya teknolojia ya kisasa vyenye uwezo wa uvumbuzi kukusanya mitaji.

Idhaa ya kiswahili 2006-11-21