Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-11-22 18:05:26    
Bw. Li Yuanchang anayependa kazi ya kufundisha vijijini

cri

   

Katika muda mrefu uliopita, shule za vijijini kwenye sehemu zilizo nyuma kiuchumi zimekuwa zinakabiliwa na matatizo ya upungufu wa walimu wenye uwezo mkubwa wa kufundisha na kukosa fedha za kuendesha shule, hivyo wanafunzi wanaoishi huko hawawezi kupata elimu nzuri kama wanafunzi wa mijini. Ili kubadilisha hali hiyo, walimu wengi wanafanya juhudi kuendeleza elimu vijijini, Bw. Li Yuanchang ni mmoja kati ya walimu hao. Alitumia miaka 6 kutembelea shule karibu 200 za msingi na za sekondari vijijini mkoani Jinlin, na kujenga vituo 42 vya kutoa mafunzo kwa walimu wa vijijini, na ameanzisha njia mpya ya kufanya mageuzi ya elimu katika vijiji maskini.

Kijiji cha Yaoweizi kiko mkoani Jilin, kaskazini mashariki mwa China. Wanakijiji wa kijiji hicho wanapenda kufuata njia ya jadi ya maisha, pia wanapopumzika, wanapenda kusikiliza sauti za wanafunzi wakisoma shuleni. Bw. Li Yuanchang alizaliwa na kukua katika kijiji hicho. Bw. Li mwenye umri wa miaka 57 anakumbuka kuwa, alipokuwa mtoto alipenda sana kusoma, ingawa hali ya maisha ilikuwa ngumu, lakini hakuwahi kuacha masomo yake, na baada ya kuhitimu chuoni alichagua kuwa mwalimu bila ya kusitasita. Alisema akiwa mwalimu wa kijijini, jambo linalomsikitisha zaidi ni kuona kuwa baadhi ya watoto wanaacha masomo yao.

"Wanafunzi wa darasa langu wote wanafanana na watoto wangu. Hivyo nawashauri walimu wawapende wanafunzi wao kama watoto wao. Mwanafunzi mmoja aliacha masomo kutokana na umaskini, alikwenda kufanya kazi mashambani. Nilikwenda nyumbani kwao mara tano hadi mara sita, mwishowe nilifanikiwa kuwashauri wazazi wake wakubali mwanafunzi huyo aendelee na masomo yake, na nilimbeba kwenda shuleni kwa baiskeli yangu.

Bw. Li Yuanchang alianza kuwa mwalimu wa lugha ya Kichina kwenye shule moja ya sekondari kuanzia mwaka 1985. Wakati huo alianza kufanya mageuzi ya mafunzo ya lugha ya taifa la China yanayoifaa elimu ya vijijini. Alivichukulia vijiji kama ni darasa kubwa la wanafunzi, na kuwahimiza wanafunzi wafanye mazoezi vijijini. Mashamba ya mahindi, vitanda na hata mitemba vyote vimekuwa vyombo vya kutoa elimu kwa wanafunzi. Mwalimu Wang Wei ambaye aliwahi kufanya kazi pamoja na Bw. Li Yuanchang anakubali kabisa mawazo hayo ya kutoa elimu.

"Mawazo ya kutoa elimu ya Bw. Li ni kuandaa wafanyakazi hodari kwa kijiji chetu. Anaona shule na darasa letu ni dogo. Anawaongoza wanafunzi wajifunze kutokana na maisha ya jamii na mazingira ya kimaumbile, na anachukua maisha ya jamii kama ni shule kubwa kwa wanafunzi. Hivyo aliwahi kuwaongoza wanafunzi wafanye mazoezi ya kilimo mashambani."

Bw. Li Yuanchang anawaongoza wanafunzi kwenda nje ya darasa, anawataka watazame kwa macho yao na kufiriki kwa kutumia akili zao, na kuandika makala zinazoweza kuonesha mawazo yao, na misimamo yao wenyewe. Bw. Li alisema, ingawa mazingira ya kujifunza vijijini ni magumu, lakini hayatawazuia wanafunzi wasifikiri wao wenyewe. Ukweli wa mambo unathibitisha kuwa, njia hiyo ya kutoa elimu imepata maendeleo mazuri. Bw. Li alitoa mfano akisema,

"Kijiji chetu kiko karibu na Mto SonghuaJiang, tukichimba kidogo kando ya mto huo tunapata mchanga na mawe. Mchanga na mawe ni rasilimali ya ujenzi, na bei yake ni kubwa. Hivyo mashamba mengi yamechimbwa na kuwa mashimo makubwa. Mwanafunzi mmoja alitumia nusu mwezi kufanya uchunguzi huko, baadaye aliandika makala akisema wazee wakiendela kuuza mchanga na kuharibu mashamba, watoto hawatakuwa na mashamba na watakumbwa na maafa, hivyo ni lazima tusimamishe uchimbaji huo unaoharibu mazingira. Baada ya kusoma makala hiyo, kiongozi wa kijiji chetu alisema mtoto mwenye umri wa miaka 15 hadi miaka 16 anaweza kutambua athari ya uchimbaji huo, aliwakusanya wafanyakazi wa kiwanda cha mchanga mara moja na kuwasomea makala hiyo, na wafanyakazi hao walisema wameelewa, na hawataendelea kuchimba michanga tena."

Habari zinasema miongoni mwa wanafunzi wa Bw. Li Yuanchang, wanafunzi wengi wamekwenda kusoma vyuoni, na wengine wengi wamekuwa watu hodari wa kupanda mimea na wana ujuzi wa kilimo. Yan Zhaodong ambaye ni mwanafunzi wa Bw. Li Yanchang alimwambia mwandishi wa habari kuwa,

"Bw. Li si kama tu anatufundisha ujuzi, bali pia anatuwezesha kuongeza uwezo uwezo wa kujifunza na kupata ujuzi, hivyo ni uwezo unaoweza kutusaidia katika maisha yetu."

Lakini miaka 6 iliyopita, Bw. Li alipata ugonjwa mkali, na ilimbidi aache kuwafundisha wanafunzi shuleni. Kutokana na afya yake, idara ya elimu ya sehemu hiyo ilimhamisha kufanya kazi ya utafiti wa mafunzo ya lugha ya Kichina katika chuo cha elimu cha Jilin. Idara ya elimu ilifanya hivyo ili aweze kupumzika vizuri, lakini Bw. Li Yuanchang anaichukulia kazi hiyo kama ni mwanzo mpya wa kuihudumia elimu ya vijijini.

"Baada ya kupata nafuu kidogo nilianza kwenda vijijini, kazi yangu imebadilika, sasa mimi ni mtafiti wa elimu. Nafiriki nikitaka kuwa mtafiti mzuri, ni lazima nijue hali ya elimu mkoani Jilin."

Baadaye alikuwa vijijini zaidi ya miezi minne kila mwaka, hivi sasa ametembelea asilimia 80 ya shule za wilayani na vijijini mkoani humo. Baada ya kufanya uchunguzi, Bw. Li Yanchang amegundua kuwa ukosefu wa walimu wenye uwezo mkubwa wa kufundisha umekuwa ni sababu muhimu inayozuia maendeleo ya elimu vijijini. Lakini kutokana na upungufu wa fedha, kazi ya kutoa mafunzo kwa walimu haiwezi kufanyika mara kwa mara. Katika hali hiyo, Bw. Li alitoa mapendekezo ya kujenga vituo vya kutoa mafunzo kwa walimu. Katika vituo hivyo walimu kutoka shule nyingi vijijini wanaweza kufanya maandalizi ya masomo pamoja, kusikiliza masomo kwenye madarasa ya walimu wengine, na kujadiliana pamoja. Kutokana na juhudi zake shule 42 za aina hiyo zilianzishwa mkoani Jilin, na walimu wengi vijijini wameinua uwezo wao wa kufundisha.

Hivi sasa Bw. Li Yuanchang bado anatafuta njia mpya ya kuendeleza elimu vijijini. Alisema anafanya hivyo kwa lengo moja tu, yaani watoto wa vijijini wapate elimu nzuri kama watoto wa mijini mapema iwezekanavyo.

Idhaa ya Kiswahili 2006-11-22