Kuanzia tarehe 7 mwezi Novemba mwaka huu watu 5 kutoka Zanzibar Tanzania ambao ni pamoja na Fundi mkuu wa Radio Tanzania Zanzibar Bwana Ali Abdula na daktari kutoka wizara ya afya ya Zanzibar Bi. Zuhura Balozi walikuja Beijjing kuhudhuria semina ya usimamizi wa msaada wa China kwa ajili ya kudumisha urafiki mzuri uliokuwepo baina ya China na nchi za Afrika. Tarehe 22 kabla ya kurudi nchini kwao walikuja kutembelea Radio China Kimataifa. Yafuatayo ni mahojiano kati ya mtangazaji wa CRI na marafiki zetu.
CRI: Wakati wa semina hiyo mlijifunza nini na kupata nini?
Ali: Tumejifunza mambo mengi sana, kwanza tumejifunza jinsi wenzetu wa China wanavyofanya katika kukuza uchumi wao ili sisi tukirudi nyumbani tuweze kufanya hivyo, halafu tumefundishwa namna gani ya kusimamia ile misaada tuliyopewa na serikali ya China ili uweze kudumu kwa muda mrefu.
CRI: Mnaona semina hiyo inawasaadia waafrika?
Ali: Inasaidia sana, na tunaomba zitaendelea kufanya.
CRI: Watu walioshiriki semina hiyo wanatoka nchi gani?
Ali: Walioshiriki semina hiyo wanatoka nchi 14 zikiwemo nchi 7 za Afrika,
CRI: Mliwahi kutembelea hapa Beijing au sehemu nyingine nchini China?
Ali: Ndiyo tulipata nafasi ya kutembelea sehemu nyingi, sehemu tofauti za kihistoria za Beijing, mji wa Nanning na mji wa Guilin kusini maghairbi mwa China, ambao ni sehemu maaruffu za kitalii. Tumefurahia hizo safari.
CRI: Mnazoea chakula hapa Beijing, pamoja na hali ya hewa?
Ali: Hali ya hewa ni baridi tukilinganishwa na kwetu, lakini tunavaa nguo za joto, kwa hiyo tunaweza kushinda hali ya hewa ya Beijing. Lakini chakula hatuwezi kuzoea, chakula cha China ni kipya sana kwetu, lakini tumejaribu hata kula kwa kutumia vijiti.
CRI: Kwa mnavyoona hali ya hapa hapa Beijjing na sehemu nyingine nchini China, ni tofuati na mlivyoona kabla ya kuja China?
Ali: Ya, hali tofauti, tulikuwa tunajua kuwa China imeendelea, kumbe maendeleo ni makubwa sana. Baada ya kuona tumejua wenzetu wamefanya kazi kubwa. Sisi tutajitahidi kufanye tuige ili tufikie kama mlivyokuwa sasa hivi.
CRI: Unaonaje ushirikiano kati ya Radio China Kimataifa na Radio Zanzibar Tanzania? Utakuwa na mustakabali mzuri?
Ali: Kipindi chote tangu Radio yetu kuwa na uhusiano na Radio China Kimataifa ni mzuri, na hizi siku za mwisho umezidi kuwa mzuri zaidi kwa sababu kila siku tunakuwa karibu, mnakuja kututembelea mara kwa mara, mnatusaidia. Tumekubaliana Radio China Kimataifa kufungua kituo chenu kule Zanzibar, tayari mmeangalia sehemu ya kuweka mnara, na nafikiria sasa mnajitayarisha ili siku za karibuni tu mje manze matangazo kule Zanzibar. Na mkianza matangazo Zanzibar, ule udugu utakuwa karibu zaidi kwa sababu kila mzanzibar atasikiliza matangazo yenu kwa urahisi hata wasikilizaji wa Tanzania bara upande wa Dar es Salaam.
CRI: Unatoka wizara ya afya Zanzibar. Huko Zanzibar wako madaktari wengi wa China, siku hizi wanafanyaje kazi yao?
Zuhura Balozi: Wanafanya vizuri, wanaingia asubuhi wanatoka mchana, wanakuja tena jioni. Wanasifiwa sana na wakazi wa Zanzibar, kwa sababu hata kama muda wanarefushwa, hawana malalamiko, wanatoa huduma vizuri.
CRI: Hii ni mara yako ya kwanza kufika China? Unaonaje China?
Zuhura Balozi: Ndiyo, hii ni mara yangu ya kwanza kufika China, japokuwa hali ya hewa, maisha na chakula cha hapa China ni tofauti na ya kwetu, lakini nakupenda, ni pazuri sana.
Idhaa ya kiswahili 2006-11-24
|