Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-06 18:21:00    
Mauna ya sanaa yachanua katika shule za vijiji nchini China

cri

Elimu ya sanaa ni moja ya maeneo muhimu katika elimu ya shuleni nchini China, lakini kutokana na upungufu wa walimu na miundombinu, hivi sasa elimu ya sanaa katika shule zilizoko sehemu za vijijini nchini China bado iko kwenye kiwango cha kimsingi, shughuli zake ni kuwafundisha watoto kuimba na kuchora tu. Lakini katika mkoa wa Jilin ulioko kaskazini mashariki ya China, shule ya Piaoyang ya vijijini inasifiwa kwa elimu yake ya muziki wa kijadi.

Wasikilizaji wapendwa, muziki wa ala ya Erhu "mashindano ya farasi" mnaosikiliza ulipigwa na wanafunzi wa shule hiyo. Muziki huo unaonesha hali ya furaha ambayo wamongolia wa China wakisherehekea sikuu na kufanya mashindano ya farasi, na kuonesha upendo wao kwa maisha na mbuga wa majani. Muziki huo ni moja ya muziki zinazopigwa vizuri kabisa na wanafunzi wa shule hiyo. Hivi karibuni, wanafunzi wa shule hiyo wamekwenda miji mikubwa ikiwemo Beijing kufanya maonesho ya michezo.

Mkuu wa shule hiyo Bw. Dong Hezhi alieleza, zamani shule ya Piaoyang ilikuwa ni shule moja ya msingi ya kawaida. Ili kuweka mazingira ya kufahamu na kujifunza sanaa kwa wanafunzi wa vijijini, mwaka 1993, shule hiyo ilianza kutoa elimu bure ya ala za kijadi kwa wanfunzi.

"tunatumia nafasi ya sikukuu na siku za mapumziko kutoa elimu ya sanaa, wanafunzi wanafanya mazoezi ya sanaa shuleni. Kwa hivyo si kama tu wamejifunza ujuzi maalum wa sanaa bali pia walijipanua pazio la macho."

Ingawa nia hiyo ni nzuri, lakini utekelezaji wake ni mgumu sana. Mwalimu wa shule hiyo Bw. Yu Wenshun alisema, ala za muziki ni gharama kubwa kwa familia za vijijini, hivyo walimu walienda katika familia hizo kuwastawisha wazazi wa watoto kuunga mkono watoto wao kujifunza muziki wa kijadi; kutokana na kuwa shule ya vijijini inatoa pato ndogo, ni vigumu kuajiri walimu hodari wa muziki kutoka mijini, hivyo walimu wa shule hiyo walifanya juhudi kubwa kujifunza mwenyewe, kujitahidi kuinua kiwango cha kupiga ala, na kuwafundisha watoto hatua kwa hatua.

"mwanzoni ilikuwa vigumu, wanafunzi hawajui la kufanya hata kidogo, niliwafundisha mmoja mmoja na hatua kwa hatua. Hivi sasa wanafunzi hao wamepata maendeleo makubwa, tunafurahi sana."

Elimu ya muziki wa kijadi inawavutia sana wanafunzi. Mwaka 1994, shule ya Piaoyang ilianzisha kundi la sanaa ya Xinlei, na kutumai kuinua zaidi uwezo wa muziki wa wanafunzi wenye kipaji.

Serikali ya China pia imeanza kutekeleza mradi mmoja unaoitwa "mpango wa Pugongying" ili kuendeleza na kuimarisha elimu ya sanaa kwa watoto wa vijijini. Kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji wa serikali, shule ya Piaoyang ilikamilisha ukarabati wa majengo ya shule, na kuongeza vyumba vya mazoezi, vyumba vya uchoraji, vyumba vya kompyuta na jumba la maonesho.

Kutokana na hali hiyo, shule ya Piaoyang ilipanua elimu yake na sanaa na kuanzisha elimu ya uimbaji, dansi, uchoraji na uandikaji, ili kuwawezesha kila mwanafunzi aweze kujifunza aina moja ya sanaa. Katika miaka iliyopita, shule hiyo imekuwa inajulikana sana huko, na wanafunzi wengi walisajiliwa na makundi maarufu ya sanaa.

Kwa mujibu wa mkuu wa shule ya Piaoyang Bw. Dong Zhihe, kutokana na umaalumu wa shule hiyo na kuendelea kwa ubora wa mazingira yake ya elimu, shule hiyo imewavutia wanafunzi wengi wa vijiji vilivyoko karibu. Hivi sasa, shule hiyo ina wanafunzi wapatao 600. wanafunzi hao wanasema, wakiwa wanaishi vijijini, hawana fursa ya kujifunza kupiga ala za muziki, lakini shule ya Piaoyang inawatoa fursa hiyo. Wanafunzi walisema:

Msichana Gaoqiang: naona elimu ya sanaa imeburudisha maisha yangu baada ya masomo, pia nimepata manufaa makubwa.

Msichana Li Chunyan: naona kujifunza kupiga Erhu kumeburudisha maisha yangu na kuongeza ujuzi wangu.

Hivi karibuni, shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO lilichukulia shule ya Piaoyang katika orodha ya klabu ya UNESCO. Mkuu wa shule hiyo Bw. Dong Zhihe alisema, anataka tumia jukwaa hiyo kuonesha sura mpya za watoto wa vijijini wa China.

"shule ya Piaoyang ikiwa ni kituo kimoja cha UNESCO, tunataka kutumia fursa hiyo kushirikiana na pande mbalimbali duniani kusaidiana na kufundishana. Hatua hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya shule yetu katika siku za baadaye. Pia tanawakaribisha watoto wa nchi mbalimbali duniani kuja kutembelea katika shule ya Piaoyang."

Idhaa ya Kiswahili 2006-12-6