Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-13 17:00:39    
Mapishi ya mseto wenye vitu vingi

cri

Mahitaji

Bakuli moja ya kiporo cha wali, kiazi kimoja, nyama iliyosagwa gramu 5, mayai mawili, punje za mahindi gramu 5, maharagwe gramu 5, kiasi kidogo cha pilipili hoho na vitunguu maji, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, chumvi vijiko viwili na chembechembe za kuongeza ladha

Njia

1. koroga mayai, kata pilipili hoho, vitunguu maji viwe vipande, kata kiazi kiwe upande, uviweke kwenye maji.

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia mayai, korogakoroga, yapakue. Washa moto tena, tia nyama iliyosagwa, mimina mvinyo wa kupikia korogakoroga, ipakue. Halafu tia vipande vya pilipili hoho na vitunguu maji, korogakoroga halafu tia upangde wa kiazi, korogakoroga, tia punje za mahindi na maharagwe, korogakoroga, tia mayai na nyama iliyosagwa, halafu tia wali, korogakoroga kwa haraka, tia chumvi, chembechembe za kuongeza ladha, korogakoroga halafu pakua. Mpaka hapo mseto huo uko tayari kuliwa.