Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-18 15:30:49    
Mkutno mkuu wa wanafasihi na wasanii wa China wafanyika mjini Beijing

cri

Mkutano mkuu wa wanafasihi na wasanii wa China ulifanyika hivi karibuni mjini Beijing. Rais Hu Jintao alihudhuria ufunguzi wa mkutano huo na kutoa hotuba muhimu.

Wajumbe zaidi ya elfu mbili kutoka sehemu mbalimbali nchini China na kutoka Hong Kong, Macau, na nchi za nje walihudhuria mkutano huo. Rais Hu Jintao kwenye ufunguzi alisema,

"Tokea China ianze kufanya mageuzi na kuingia katika kipindi kipya cha historia, watu wa makabila yote wanasonga mbele kwa mshikamano na wameleta mafanikio makubwa katika ujenzi wa taifa, na mafanikio hayo yametia chachu ya maendeleo ya fasihi na sanaa nchini China. Wanafasihi na wasanii wamekuwa na mambo mengi ya kuandika, ustawi mkubwa umetokea katika nyanja za fasihi na sanaa."

Rais Hu Jintao alisifu sana mchango mkubwa waliotolewa na wanafasihi na wasanii katika kukidhi maisha ya utamaduni ya wananchi. Alisema fasihi na sanaa ni sekta muhimu ya kusukuma mbele maendeleo ya jamii na ujenzi wa jamii yenye masikilizano, na sekta hiyo haiwezi kukosekana katika ujenzi wa utamaduni wa kisasa.

Shirikisho la wanafasihi na wasanii lilianzishwa mwaka 1949. Hivi sasa shirikisho hilo lina matawi yake 52 katika mikoa na wilaya. Shirikisho la Waandishi wa Vitabu lilianzishwa mwaka 1947, hivi sasa shirikisho hilo lina matawi 43 kote nchini China.

Shirikisho la waandishi wa vitabu ni idara muhimu katika nyanja ya fasihi nchini China. Waandishi mashuhuri wa vitabu hayati Bw. Mao Dun na Ba Jin waliwahi kuwa wenyekiti wa shirikisho hilo katika nyakati tofauti. Shirikisho hilo lina jukumu la kutathmini na kutoa tuzo za fasihi za Lu Xun na za Mao Dun na linachapisha majarida la "Fasihi na Sanaa", "Fasihi ya Umma", "Mashairi", "Fasihi ya makabila", "Waandishi wa Vitabu wa China", "Riwaya Teule" na lina shrikika kubwa la uchapishaji la waandishi wa vitabu wa China. Shirika hilo ni idara muhimu katika kuandaa waandishi wa vitabu chipukizi, kuhimiza maendeleo ya fasihi ya makabila na kustawisha maingiliano ya fasihi kati ya China na nchi za kigeni.

Kwenye ufunguzi rais Hu Jintao aliwaagiza waandishi wa vitabu na wasanii waende kwenye maisha halisi na kuandika vitabu vinavyovutia na kuendana na wakati. Alisema,

"Kila jamii ya binadamu inapopiga hatua ndipo ustaarabu wa binadamu unapoinuka huambatana na maendeleo ya utamaduni. Kazi za kiutamaduni katika kipindi hiki ni kustawisha utamaduni wa kisasa wa kiujamaa na kutoa mchango katika ujenzi wa jamii yenye masikilizano."

Mkutano huo uliofanyika kwa siku nne, pia umerekebisha katiba ya Shirikisho la Sanaa na Shirikisho la Waandishi wa Vitabu na limechagua mwenyekiti mpya wa mashirika hayo.

Idhaa ya kiswahili 2006-12-18