Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-12-26 19:24:19    
China yaingia katika kipindi kipya cha kufungua mlango

cri

Tarehe 11 mwezi Desemba ni siku ambayo China ilitimiza miaka 5 tangu China ijiunge na shirika la biashara duniani, WTO. Muda wa miaka 5 unamaanisha kumalizika kwa kipindi cha mpito cha kujiunga na WTO kwa China, ambapo inaonesha kuwa China imeingia kipindi kipya ya kufungua mlango kwa pande zote. Ofisa wa ngazi ya juu wa serikali ya China amesema, kipindi cha sasa ni "kipindi cha pili cha mpito", ambacho China imetimiza ahadi muhimu ilizotoa wakati wa kujiunga na WTO, na maendeleo ya uchumi wa China yako katika mwanzo mpya.

Mkutano wa taifa wa kazi za uchumi uliomalizika hivi karibuni ulisema, baada ya kutupia macho mazingira ya uchumi wa dunia, inaonekana kuwa maendeleo ya China yanapata nafasi nzuri, na pia yanakabiliwa na changamoto kali, lakini fursa ni kubwa kuliko changamoto. Moja ya majukumu muhimu ya uchumi ya serikali kuu ni kushikilia sera za ufunguaji mlango za kunufaishana na kuinua kiwango cha ufunguaji mlango. Mtafiti wa taasisi ya utafiti wa ushirikiano wa biashara wa kimataifa ya wizara ya biashara ya China Zhao Yumin alisema, katika "kipindi cha pili cha mpito", utaratibu wa uchumi unaofuatwa hivi sasa nchini China utakabiliwa na changamoto mpya. Ili kuendana na maendeleo ya utandawazi, baadhi ya sekta zilizotumia mbinu za ukiritimba zitalazimika kufungua milango.

Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa uchumi wa China na WTO ya chuo kikuu cha Beijing anayeshughulikia utafiti wa uchumi binafsi Bw. Shan Zhongdong alisema, katika kipindi kipya, serikali inatakiwa kubadilisha majukumu yake, kuanzisha utaratibu wa uchumi wa soko huria; Kuboresha uhusiano wa biashara kati ya China na nchi za nje; Na kufuatilia hatari ya kupanda kwa kiwango cha kubadilisha fedha za Renminbi kwa fedha za kigeni.

Katika miaka 5 iliyopita tangu China ijiunge na WTO, pato la China la nchini limekuwa zaidi ya dola za kimarekani trilioni 2 likichukua nafasi ya 4 duniani katika mwaka 2005; na thamani ya biashara ya nje imekuwa ni zaidi ya dola za kimarekani trilioni 1, ikichukua nafasi ya tatu duniani mwaka 2005, wakati wastani wa mitaji ya kigeni inayotumika ilikaribia dola za kimarekani bilioni 55 kwa mwaka, na jumla ya mitaji ya kigeni iliyotumika nchini China imefikia dola za kimarekani bilioni 274.1.

Naibu waziri wa biashara Bw. Yi Xiaozhun tarehe 11 mwezi Desemba alisema, katika miaka mitano iliyopita ufunguaji mlango wa China kwa nje ulikuwa na mabadiliko makubwa matatu: la kwanza, ni ufunguaji mlango wa kikanda kubadilika kuwa wa pande zote; Pili, sekta zinazofungua mlango kutoka zile za jadi za biashara ya bidhaa hadi biashara ya huduma; Na tatu, masharti ya uidhinishaji wa maombi ya kuingia kwenye masoko ya China yamebadilika kuwa ya utaratibu, wazi na kufuata vigezo.

Alisema, katika miaka mitano iliyopita wazo lililofuatwa na WTO limeeleweka zaidi kwa watu wa China, kanuni za WTO za "Uwazi" na "Bila Ubaguzi" zimekuwa mujibu wa utungaji sheria kwa China, mtazamo wa kimataifa, uvumbuzi, ushidani, maendeleo, utaratibu wa kisheria na hakimiliki ya kiujuzi vimeingia katika mawazo ya watu, utaratibu wa viwanda na utaratibu wa uhasibu wa kisasa unaanzishwa hatua kwa hatua, sifa za viwanda na wananchi zinainuka zaidi.

Katika miaka mitano iliyopita China ilijitahidi kutekeleza ahadi ilizotoa wakati inajiunga na WTO. Ushuru wa forodha wa China umeshuka hadi 9.9% kutoka 15.3% ya hapo awali, China imeondoa vizuizi vyote visivyo vya ushuru wa forodha, imefungua mlango kwa uendeshaji shughuli za biashara na kufungua mlango wa soko la biashara ya huduma, hivi sasa China imekuwa moja ya masoko yanaliyofunguliwa mlango kabisa duniani. Licha ya hayo, China imeimarisha ulinzi kuhusu hakimiliki ya kiujuzi, imerekebisha sheria na kanuni zinazohusika na mambo ya biashara, na imejenga utaratibu wa sheria wenye uwiano, uwazi na wenye kuambatana na matakwa ya WTO.

Idhaa ya Kiswahili 2006-12-26