Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-03 19:19:45    
Mapishi ya bilinganya na nyanya

cri

Mahitaji

Bilinganya tatu, nyanya mbili, asali vijiko viwili, yai moja, unga wa ngano wa vijiko vitano, kiasi kidogo cha chumvi, mchuzi wa sosi, vitunguu maji na tangawizi.

Njia

1. kata bilinganya ziwe vipande, koroga pamoja na asali, yai na unga. Kata nyanya ziwe vipande.

2. washa moto na tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe joto la nyuzi ya 80, tia vipande vya bilinganya kwenye sufuria vikaange mpaka viwe na rangi ya hudhurungi kasha vipakue.

3. washa moto tena, tia vipande vya bilinganya, vipande vya vitunguu maji na tangawizi, tia vipande vya nyanya, chumvi na mchuzi wa sosi, mimina maji kidogo, chemsha kwa dakika mbili, mimina mafuta ya ufuta, pakua na mimina vipande vya vitunguu maji. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.