Mwezi Aprili mwaka 2006 taasisi ya bendi ya symphony ya Chuo kikuu cha muziki cha China kinachotoa mafunzo ya kitaalamu kwa wapigaji wa muziki wa symphony wenye kiwango cha kimataifa ilianzishwa hapa Beijing, na mwanzilishi wake ni mmarekani mwenye asili ya China Bw. Hu Yongyan. Katika muda mrefu uliopita, China imekuwa ikiweka mkazo katika kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wapigaji muziki wa solo, na wamejitokeza wapigaji muziki hodari mbalimbali wakiwemo Lu Siqing na Chen Xi waliopata tuzo katika mashindano makubwa ya kimataifa. Lakini wapigaji muziki hao wanapaswa kutumia muda mrefu kuzoea kujiunga na bendi ya symphony kutokana na kuzoea kupiga muziki peke yake. Bw. Hu Yongyan alisema kiwango cha upigaji muziki cha bendi ya symphony kinaweza kuonesha vizuri zaidi sura ya nchi moja.
Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, Bw. Hu Yongyan alikwenda Marekani na kusoma katika Chuo kikuu cha Yale na Chuo cha muziki cha Juilliard. Wakati huo aligundua pengo lililopo kati ya kiwango cha upigaji muziki wa symphony cha China na kiwango sanifu cha kimataifa. Baada ya hapo, uzoefu wake wa kushiriki kwenye kazi ya usimamizi kwenye bendi nyingi za symphony nchini China na nchi za nje na kazi ya uongozaji kwenye bendi ya symphony, ulimsaidia kupata ufahamu wa kina zaidi kwa mafunzo, usimamizi na maendeleo ya bendi ya symphony. Mwaka 2004 baada ya karudi nchini China, Bw. Hu Yongyan aliongoza bendi ya symphony ya Chuo kikuu cha muziki kufanya maonesho katika nchi za nje, ili kuwasaidia wanafunzi wa China kufanya mazoezi na kupata uzoefu, na kufanya maandalizi kuanzisha Chuo cha bendi ya symphony.
Tofauti na njia zilizotumiwa zamani za kutoa mafunzo, Chuo hicho kina lengo la kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wapigaji muziki wa symphony, na kimeweka mkazo katika kufanya mazoezi ya kupiga muziki wa symphony ni wenye mitindo mbalimbali na katika vipindi mbalimbali, na kutoa fursa za kutosha kwa wanafunzi kufanya maonesho ili kuwasaidia wainue uwezo wa upigaji muziki. Kama Bw. Hu Yongyan alivyosema Chuo cha bendi ya symphony kimetoa mafunzo kwa kufuata kiwango cha kimataifa, na kila mwanafunzi ana nafasi maalum kwenye bendi ya symphony, kwa mfano mwanafunzi anayepiga zumari anaweza kushika nafasi hiyo kwenye bendi yoyote baada ya kuhitimu kutoka chuo hicho bila ya kuchukua muda mrefu wa kufanya mazoezi.
Mwalimu wa upigaji wa violin ya wastani wa chuo hicho Bw. He Rong alihitimu kutoka Chuo cha muziki cha Yale, ana uzeofu wa miaka mingi wa kupiga muziki na kutoa mafunzo ya kitaalamu katika bendi za symphony katika nchi za nje. Akizungumzia mafunzo ya Chuo cha bendi ya symphony alisema:
"Utaratibu kama huu wa upigaji wa muziki wa Chuo cha bendi ya symphony haujaonekana nchini China. Tunawahimiza wanafunzi kufanya mazoezi na maonesho, kwa sababu wengi kati yao watashughulikia upigaji muziki katika bendi za symphony. Chuo hicho ni kituo cha kutoa mafunzo ya kitaalamu."
Vyuo vya bendi ya symphony kama hicho vimeonekana katika nchi za Ulaya na Marekani katika muda mrefu uliopita. Chuo cha bendi ya symphony cha Berlin cha Ujerumani (the Orchestra Academy of Berliner Philharmoniker) kilianzishwa mwaka 1972, na kilikuwa na lengo la kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wapigaji muziki wenye uwezo wa juu kwa bendi ya symphony ya Berlin. Mwaka 1987 Kundi la simphoni la dunia mpya (New World Symphony) lilianzishwa nchini Marekani na kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wapigaji muziki wanaoshika nafasi ya kwanza kwenye bendi kubwa mbalimbali za symphony duniani. Hizo vilevile ni sababu muhimu kwa baadhi ya bendi za symphony katika nchi za magharibi hupata wapigaji muziki hodari na kuwa bendi za symphony za kiwango cha juu duniani. Lakini katika muda mrefu uliopita hakukuwa na mashirika kama hayo nchini China. Kutokana na hali hiyo, Bw. Hu Yongyan alianzisha bendi ya symphony kwenye chuo kikuu cha muziki cha China. Mwaka 2006 chuo hicho kiliandikisha kikundi cha kwanza cha wanafunzi. Wu Meng ambaye ni mmoja kati ya wanafunzi hao, sasa anapiga muziki kwenye nafasi ya kwanza ya kupiga violin katika bendi ya symphony alisema:
"Kila mwanafunzi ana mwalimu mmoja, na maonesho ya muziki yanafanyika mara mbili kwa mwezi."
Mbali na mafunzo ya kitaalamu na maonesho, Bw. Hu Yongyan pia ametoa fursa nyingi kwa wanafunzi hao kufanya shughuli za mawasiliano ya kimataifa, na kuwaongoza wanafunzi kufanya maonesho katika nchi za nje, ili kuwasaidia wainue uwezo wao na kiwango cha jumla cha upigaji muziki cha bendi. Bw. Hu Yongyan alisema anafanya hivyo kwa sababu anatumai kuwa wanafunzi wa bendi ya symphony katika Chuo kikuu cha muziki cha China wataajiriwa katika bendi za symphony za kiwango cha juu baada ya kuhitimu.
Chuo kikuu cha muziki cha China kina wanafunzi wengi wenye uwezo mkubwa. Micky Wrobleski kutoka Marekani ambaye anapiga muziki kwenye nafasi ya kwanza ya kupiga tarumbeta kwenye bendi ya symphony ya Beijing anasema:
"Hivi sasa chuo hicho kinaendeshwa vizuri, na kimefanya kazi nyingi zenye ufanisi. Bw. Hu Yongyan ni mtu mwenye matumaini makubwa, na ana uwezo wa kuwahimiza wenzake kushiriki kwenye kazi yake. Kuanzishwa kwa chuo hicho kuna umuhimu mkubwa."
Akiwa mwanzilishi wa Chuo cha bendi ya symphony, Bw. Hu Yongyan anafahamu sana lengo la chuo hicho, yaani kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wapigaji hodari wa muziki wa symphony wa China, na kuinua kiwango na athari ya upiaji wa muziki wa symphony wa China duniani.
"Tutawavutia wanafunzi wengi zaidi wanaohitimu kutoka chuo kikuu cha muziki cha China. Na Chuo cha bendi ya symphony kitaendeshwa kuwa chuo cha elimu na utafiti chenye sifa bora. Juhudi zetu ni hatua muhimu kwa maendeleo ya upigaji muziki wa symphony nchini China."
Bw. Hu Yongyan alisema mwezi Machi mwaka kesho Chuo cha bendi ya symphony kitafanya maonesho ya upigaji muziki wa Symphony na Koncheto wa Brahms. Ni vigumu kwa chuo cha bendi ya symphony kilichoanzishwa kwa muda mfupi kupiga muziki huo mgumu sana. Lakini Bw. Hu Yongyan alisema mazoezi hayo ya kiwango cha juu yataweza kuhimiza Chuo cha bendi ya symphony cha chuo kikuu cha muziki cha China kuwa kituo kinachotoa mafunzo ya kitaalamu kwa wapigaji hodari wa muziki wa symphony wenye kiwango cha kimataifa.
Idhaa ya Kiswahili 2006-01-03
|