Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-09 15:31:50    
Ujenzi wa utaratibu wa sheria kwenye soko la mitaji wahimiza mabadiliko ya kihistoria kwenye soko la hisa

cri

Habari kutoka kamati ya usimamizi wa soko la hisa ya China zilisema, tangu "Sheria ya kampuni ya Jamhuri ya watu wa China" na "Sheria ya hisa ya Jamhuri ya watu wa China" zianze kutekelezwa tarehe 1 mwezi Januari mwaka 2006, ujenzi wa utaratibu wa sheria wa soko la mitaji wa China umepata maendeleo makubwa na kuhimiza mabadiliko ya kihistoria kwenye soko la hisa la China, sheria hizo zilirekebishwa na kupitishwa mwaka 2005.

Ofisa husika wa kamati ya usimamizi wa sekta ya hisa alisema, mageuzi yaliyomalizika hivi karibuni kuhusu utenganishaji wa hisa na haki yanatekeleza kanuni ya kila moja ya hisa za aina moja ina haki sawa na kutatua matatizo yaliyoletwa na utenganishaji wa hisa na haki yake, kuondoa vikwazo vya utaratibu na mfumo vinavyoathiri uwezo wa soko la mitaji na kuweka msingi manufaa ya pamoja ya wenye hisa. Mageuzi hayo yameanzisha mazingira kwa uboreshaji wa uwezo wa kuweka bei wa soko la mitaji, kuhimiza mageuzi husika na kuharakisha uvumbuzi wa soko, na kuimarisha msingi na kuboresha utaratibu wa soko la mitaji.

Mwaka 2006, kamati ya usimamizi wa sekta ya hisa ilibuni na kurekebisha kanuni kumi kadhaa zinazoambatana na utekelezaji wa sheria mbili zilizotajwa, na kusawazisha mfumo wa sheria na kanuni za soko la mitaji. Mfumo wa sheria na kanuni hizo utahusisha pande na maeneo mbalimbali yakiwemo utoaji hisa, biashara ya hisa na urari wa hesabu. Mbali na hayo, China itaboresha hatua kwa hatua mfumo wa utekelezaji wa sheria kwenye soko la hisa, kukuza uwezo wa usimamizi wa soko, kuimarisha nguvu ya utekelezaji wa sheria kwenye soko la hisa na kutoa adhabu kwa vitendo vya kukiuka sheria au kanuni za soko la mitaji.

Ofisa huyo alisema mageuzi na uvumbuzi wa soko la mitaji la China limepata maendeleo muhimu. Mfumo wa utoaji hisa na uwekaji bei wa soko la hisa umeundwa kwa hatua ya mwanzo. Shughuli za ukusanyaji mitaji na hisa za kampuni pamoja na biashara ya bidhaa zitakazozalishwa zitafanyika hivi karibuni, soko la hisa, soko la fedha na soko la bima yameungana kwa kiwango fulani.

Hivi sasa muundo wa soko la mitaji la nchini China unabadilika kuwa mzuri zaidi. Viwanda na kampuni ndogo na za wastani zinapata maendeleo kwa hatua imara, mfumo wa wakala wa mauzo unapanuka hatua kwa hatua, majaribio ya uwekaji bei na mauzo ya hisa za kampuni ambazo hazijaidhinishwa kuingia katika soko la hisa, yamefanyika kwenye eneo la sayansi na teknolojia la Zhongguancun, ujenzi wa mfumo wa masoko umepata maendeleo ya mwanzo; kuingia katika soko la hisa kwa baadhi ya kampuni kubwa zikiwemo Benki ya China na Benki ya Viwanda na Biashara, kuuza hisa kwa wateja maalumu, na kampuni zilizofilisika kununuliwa na kampuni nyingine imewezesha kampuni nyingi kuingia kwenye soko la hisa, umuhimu wa hisa zenye thamani za kampuni kubwa zenye mustakabali mzuri umeonekana kwenye soko la hisa; hisa zinazomilikiwa na wakala wa hisa, wafanya-biashara wa hisa, bima, mfuko wa fedha za kiinua mgongo cha uzeeni na wawekezaji wa nchi za nje zimefikia 41% za hisa zilizoko katika mzunguko wa hisa kwenye soko la hisa, ikiwa ni ongezeko la 10% kuliko mwishoni mwa mwaka 2005, hali ya wawekezaji pia imebadilika kwa udhahiri; kutolewa kwa aina nyingi za biashara ya hisa kumetoa nafasi kubwa ya kuchagua kwa wawekezaji.

Tangu kutolewa upya kwa hisa mpya mwezi Mei mwaka 2006, hisa za kampuni nyingi kubwa zenye mustakabali mzuri wa maendeleo zikiwemo Benki ya China, Benki ya Viwanda na Biashara, Shirika la Ndege la China na reli ya Daqin, fedha zilizokusanywa kwenye soko la hisa zilifikia Yuan bilioni 210, ambazo ni rekodi mpya katika historia. Uwezo wa soko la hisa wa kupanga upya matumizi ya mitaji umekuwa vizuri, hatua ambayo inahimiza maendeleo ya uchumi wa taifa, marekebisho ya muundo wa sekta ya uzalishaji mali na kukua kwa uwezo wa uvumbuzi wa China, na kiwango cha uhusiano kati ya soko la mitaji na uchumi wa taifa kimeinuka kwa udhahiri.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-09