Mahitaji: Nyama ya ng'ombe gramu 350, unga wa mchele gramu 75, mafuta gramu 50, mchuzi wa sosi gramu 30, unga wa pilipili hoho gramu 3, unga wa pilipili manga gramu 2, vitunguu maji na tangawizi kila kimoja gramu 8, mchuzi wa kambamti, kiasi kidogo cha kisibiti
Njia :
1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande vyembamba, kata vitunguu maji, saga tangawizi halafu weka kwenye maji, koroga vipande vya nyama ya ng'ombe pamoja na mafuta, mchuzi wa kambamti, mchuzi wa sosi, tangawizi, unga wa pilipili manga, unga wa mchele, halafu weka kwenye bakuli.
2. mimina maji kwenye sufuria, weka bakuli hiyo kwenye sufuria, washa moto chemsha kwa mvuke. Baada ya kuiva, pakua na uweke nyama ya ng'ombe kwenye sahani. Tia vipande vya vitunguu maji, kisibiti, unga wa pilipili hoho. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
Idhaa ya Kiswahili 2007-01-10
|