Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-16 14:53:41    
Benki ya Ujenzi ya China yanunua tawi la Asia la Benki ya Marekani

cri

Bodi ya Benki ya Ujenzi ya China tarehe 29 mwezi Desemba mwaka 2006 ilitangaza kuwa imenunua hisa zote za tawi la Asia la Benki ya Marekani. Baada ya hapo tawi la Asia la Benki ya Marekani lilibadilishwa jina na kuitwa "tawi la Asia la Benki ya Ujenzi ya China", ambapo alama za mikataba na nyaraka za benki pamoja na majina ya vitengo vya benki hiyo pia yalibadilika.

Tarehe 24 mwezi Agosti mwaka 2006, Benki ya Ujenzi ya China ilisaini mkataba na Benki ya Marekani kuhusu kununua hisa zote zilizouzwa na tawi la Asia la Benki ya Marekani zenye thamani ya dola za Hong Kong bilioni 9.71, ambayo ni mara 1.32 ya thamani ya mali ya tawi hilo mwishoni mwa mwaka 2005. Benki ya Ujenzi ya China iliitisha mkutano wa dharura wa wenye hisa za benki tarehe 20 mwezi Oktoba mwaka 2006, ambao ulipitisha uamuzi wa kununua hisa za tawi la Asia la Benki ya Marekani. Kwa kufuata sheria za usimamizi, shughuli za ununuzi huo ziliidhinishwa na kamati ya usimamzi ya sekta ya benki ya China, idara za usimamizi wa mambo ya fedha za mikoa ya Hong Kong na Macau.

Ili kuhakikisha kuwa shughuli za benki zinakwenda vizuri baada ya tawi la Asia la Benki ya Marekani kukabidhiwa, Benki ya Ujenzi ya China, Benki ya Marekani na tawi la Asia la Benki ya Marekani ziliunda kikundi maalumu kushughulikia mambo ya makabidhiano. Kutokana na ushirikiano mzuri wa pande hizo tatu pamoja na ukaguzi na tathimini zilizofanyika, pande hizo zilibuni mpango wa kazi na sera za benki katika kipindi cha mpito, kufanya tathimini baada ya kuachana kati ya mfumo wa uendeshaji shughuli za benki na usimamizi kuhusu hatari zinazoikabili benki, pamoja na kufanya maandalizi kuhusu kubadilisha alama za benki. Kati ya shughuli hizo, ili kuweka msingi imara kwa makabidhiano tulivu, Benki ya Ujenzi na Benki ya Marekani pamoja na tawi la Asia la Benki ya Marekani zilisaini rasmi "mkataba ya huduma katika kipindi cha mpito", ambao unaagiza kuwa baada ya kumaliza makabidhiano, Benki ya Marekani itaendelea kutoa huduma za uungaji mkono kwa muda wa miezi 18 kwa Benki ya Ujenzi na tawi la Asia la zamani la Benki ya Marekani kuhusu usimamizi wa hatari na uendeshaji shughuli za benki.

Hadi kufikia tarehe 30 mwezi Juni mwaka 2006, jumla ya thamani ya mali ya Benki ya Ujenzi katika Hong Kong ni kiasi cha Renminbi Yuan bilioni 54.8 na jumla ya mikopo iliyotolewa ni Yuan bilioni 32.2, ambapo jumla ya thamani ya mali ya tawi la Asia la Benki ya Marekani ni dola za Hong Kong bilioni 50.2, jumla ya mikopo iliyotolewa ni dola za Hong Kong bilioni 26 na jumla ya thamani ya mali halisi ya tawi hilo ilikuwa dola za Hong Kong bilioni 7.8.

Kiongozi husika wa Benki ya Ujenzi tarehe 29 mwezi Desemba mwaka 2006 alisema, baada ya makabidhiano ya benki hizo mbili, shughuli za Benki ya Ujenzi huko Hong Kong zitaongezeka haraka na kufikia maradufu kuliko kabla ya hapo, ambapo mikopo ya wateja imeongezeka na kufikia nafasi ya 9 kutoka ile ya 16 ya hapo zamani. Kutokana na ununuzi huo wa hisa, Benki ya Ujenzi imepata vitengo, wafanyakazi, mfumo, shughuli za benki na wateja inavyovihitaji katika kukuza shughuli zake huko Hong Kong, na kukuza uwezo wake wa kutoa huduma kwa ajili ya wafanyabiashara wa uuzaji wa rejareja na kampuni za biashara. Kwa upande mwingine shughuli za Benki ya Ujenzi huko Hong Kong pia zitaongezeka kutokana na mfumo mkubwa wa benki hiyo pamoja na idadi kubwa ya wateja kwenye China bara, na kutoa huduma bora kwa shughuli za wateja katika nchi za nje.

Mwaka 2005 Benki ya Ujenzi, ambayo ni moja ya benki nne kubwa za biashara za serikali, ilitangulia kumaliza mageuzi ya kufuata utaratibu wa hisa na kuuza hisa zake kwenye soko la Hong Kong. Baada ya hapo Benki ya Ujenzi ilifanya mageuzi na uvumbuzi wenye ufanisi, sasa imekuwa moja ya benki za biashara, ambazo serikali inamiliki sehemu kubwa ya hisa, zenye nguvu kubwa ya ushindani, uwezo mkubwa wa shughuli za benki, udhibiti wa hali ya hatari, utoaji huduma kwa wateja na kupata faida.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-16