Hivi karibuni mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang wa Guangxi, China umeweka kanuni kuhusu kazi ya kutoa misaada kwa wanafunzi wapya wa vyuo vikuu wenye matatizo ya kiuchumi, ili kuhakikisha wanafunzi hao hawaachi shule kutokana na umaskini.
Habari kutoka idara ya elimu ya mkoa unaojiendesha wa kabila la waZhuang Guangxi zinasema, kanuni hizo mpya zimeamua kuwa misaada ya masomo inatakiwa kutolewa kwa wanafunzi wa shule za sekondari ya juu wenye matatizo ya kichumi ambao walifaulu kwenye mtihani wa taifa wa kujiunga na vyuo vikuu na kuandikishwa na chuo kikuu fulani.
Kwa mujibu wa kanuni hizo, wanafunzi kutoka familia iliyopoteza mzazi mmoja na wale wanaotoka kwa familia za walemavu, wanafunzi wa makabila madogomadogo wenye matatizo ya kiuchumi, watoto wa askari au watu waliojitolea muhanga, wanafunzi kutoka familia maskini yenye mzazi mmoja na wanafunzi wa vijijini wenye matatizo ya kiuchumi watapewa kapaumbele katika kupewa misaada. Kuanzia mwaka 2007, mkoa wa Guangxi unatenga yuan milioni 10 kwa ajili ya mpango huo. Ili kuhakikisha uwawa na haki, kanuni hizo zinazitaka, shule za sekondari zinwajibike na kazi ya kuthibitisha na kutangaza orodha ya wanafunzi watakaopewa misaada, na misaada hiyo ni lazima ikabidhwe kwa wanafunzi kabla ya kufungua muhula katika vyuo vikuu.
Kanuni hizo pia zinaagiza kuwa, kikundi cha uongozi wa kazi ya kutoa misaada kwa wanafunzi kinachoundwa na maofisa wa idara za elimu, fedha, mambo ya kiraia na shughuli za kuondokana na umasikini kishughulikie kuratibu na kusawazisha raslimali za pande mbalimbali; shule zenye wanafunzi waliopewa misaada lazima ziweke mafaili husika.
Mwaka 2006, vyuo vikuu 47 vya kiserikali vya mkoa wa Guangxi viliandikisha wanafunzi laki moja na elfu 17, wanafunzi elfu 23.3 kati yao wana matatizo ya kiuchumi. Kutokana na misaada ya kiserikali na fedha zilizochangishwa katika jamii, ada za masomo na gharama za maisha za wanafunzi hao tayari zimetatuliwa.
|