Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-17 21:02:57    
Mapishi samaki ya aina ya Lu wa kuchemsha kwa mvuke

cri

Mahitaji

Samaki mmoja aina ya lu, uyoga gramu 10, paja la nguruwe gramu 20, vipande vya vitunguu maji na tangawizi kila kimoja gramu 5, kiasi kidogo cha kisibiti, mchuzi wa sosi vijiko viwili, M.S.G kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, na wanga vijiko viwili

Njia

1. ondoa kichwa na mkia wa samaki, kata mgongo wa samaki vipande viwili, na kata kila kipande kiwe vipande sita, weka kwenye bakuli moja koroga pamoja na chumvi na M.S.G. kata uyoga na paja la nguruwe liwe vipande. Koroga mchuzi wa sosi, sukari, M.S.G, wanga na maji kwenye bakuli moja.

2. weka kila kipande cha samaki kati ya kipande cha uyoga na paja la nguruwe. Weka vipande hicho kwenye sahani, weka kichwa na mkia wa samaki kama akiwa samaki mmoja. Weka sahani hiyo kwenye sufuria uichemshe kwa mvuke kwa dakika 8, ipakue. Pasha moto tena, tia mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe joto la nyuzi 80 yamimine kwenye samaki pamoja na mchuzi uliokorogwa. Hadi hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.