Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-01-22 16:25:11    
Mikahawa ya chai ya Tianjin yenye burudani ya kufurahisha

cri

Watalii waliowahi kutembelea mjini Tianjin wote walipata picha nzuri juu ya mikahawa ya chai mikubwa na midogo mjini Tianjin. Mji wa Tianjin unasifiwa kuwa ni "chimbuko la michezo ya sanaa ya ngonjera" kaskazini mwa China, mikahawa ya chai ya Tianjin ni sehemu inayoweza kuonesha umaalum huo wa mji huo. Wakazi wa Tianjin wakipata nafasi za mapumziko, huwaalika marafiki wawili watatu kwenda kwenye mikahawa ya chai kunywa chai, kuburudishwa kwa michezo ya ngonjera, Dagu na mingineyo, hata vijana wa Tianjin wana ushabiki huo. Ndiyo maana mikahawa ya chai ya Tianjin inawavutia wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini China. Bwana Ke Qiu kutoka mji wa Wenzhou mkoani Zhejiang alisema:

Nilianza kufanya kazi mjini Tianjin mwaka 2002, mwanzoni kila ifikapo wikiendi nilikuwa na nafasi kubwa, marafiki zangu walinialika kwenda kwenye mkahawa wa chai kusikiliza michezo ya ngonjera, nilifurahishwa sana na michezo hiyo, hata nikaweza kuongea lafudhi ya Tianjin, maneno waliyosema wakazi wa Tianjin ni yenye mvuto pekee wa kuwafurahisha watu. Hivyo katika miaka ya hivi karibuni, hata marafiki na wenzangu walifika Tianjin kunitembelea, niliwaongoza kwenda kwenye mikahawa ya chai kusikiliza ngonjera za Tianjin, na wote hao walifurahishwa na ngonjera hizo.

Mkahawa wa chai wa Qianshangyi ulioko katika mtaa wa Guyi wa eneo la Nankai mjini Tianjin awali ulikuwa duka la hariri lenye historia ya miaka 80, hivi leo duka hilo limekarabatiwa kuwa mkahawa wa chai wenye mtindo wa kale. Mteja akitumia Yuan 10 tu anaweza kunywa chai ndani ya mkahawa huo, ambapo ataburudishwa kwa michezo ya ngonjera na mingine kadha wa kadha, ili kujiburudisha kwa raha mustarehe. Ndiyo maana kila ifikapo wikiendi, mkahawa huo hujaa wateja, ambapo vicheko vya wateja huanguka ukumbini humo kutokana na kuburudishwa kwa michezo ya sanaa.

Mchezaji wa ngonjera Bwana Yang Wei alizaliwa katika familia ya wacheza ngonjera, baba yake Yang Shaohua, na kaka yake mdogo Yang Yi wote ni wana ngonjera maarufu nchini China. Na Bwana Yang Wei anapendwa na wakazi wa Tianjin kutokana na maonesho yake ya mchezo wa ngonjera katika mkahawa wa chai. Akizungumzia mvuto pekee wa maonesho ya ngonjera kwenye mkahawa wa chai, Bwana Yang Wei alisema: Naona kufanya maonesho ya ngonjera kwenye mkahawa wa chai kunaweza kukaribia zaidi na watazamaji na wasikilizaji. Michezo tuliyoonesha zamani, wasikilizaji na watazamaji wameshaizoea na kuijua, hii inatubidi tubuni michezo mipya ili kuwafurahisha.

Tianjin ni mji wa kale wenye historia ya miaka 600, ambao ni mji muhimu wa bandari nchini China. Shughuli za uchukuzi kwenye mto zilizoendelea zimekuwa msingi wa utamaduni wa Tianjin wenye umaalum wa gati. Watu wa matabaka mbalimbali ya jamii walileta utamaduni wa aina mbalimbali, michezo ya sanaa ya wasanii wa Tianjin huonesha maisha ya watu wa aina mbalimbali kwenye jamii, na michezo ya sanaa ya ngonjera na Dagu imeendelezwa zaidi. Mpaka sasa katika mikahawa ya Chai ya Tianjin, wateja wanaweza kuburudishwa kwa ngonjera za kiasili sana. Meneja wa Shirika la utalii la Jingdian la Tianjin Bwana Chang Zhipeng alisema:

Mjini Beijing kuna mabaki ya bustani ya kifalme na mchezo wa opera ya kibeijing; mijini Suzhou na Hangzhou kuna vivutio mbalimbali na mchezo wa sanaa wa Pingtan. Na mijini Tianjin watalii wanaweza kuona majengo kadha wa kadha ya kale, sanaa za kienyeji, michoro ya mwaka wa jadi ya Yangliuqing, vinyago vya udongo vya mtindo wa Zhang, tiara za mtindo wa Wei na kadhalika. Na michezo ya ngonjera ya Tianjin inawafurahisha watalii zaidi kutokana na mtindo wake pekee. Katika mikahawa ya chai iliyojaa harufu nzito ya uenyeji wa Tianjin, wachezaji wa ngonjera hutumia maneno ya kufurahisha watu kwa kuelezea historia ya Tianjin, mageuzi ya Tianjin, na hadithi mbalimbali kuhusu wakazi wa Tianjian na mambo mbalimbali ya Tianjian?maelezo yao ni mazuri kabisa kuliko yale ya waongozaji wa watalii.

Mjini Tianjin, kila siku wasanii wanafanya maonesho ya michezo ya ngonjela na mingineyo katika Mkahawa wa chai wa Yanle ambao zamani mchezaji maarufu wa ngonjera Ma Sanli alifanya maonesho yake kwenye mkahawa huo, kwenye Jumba la maonesho ya sanaa la China lenye historia ndefu, mikahawa mbalimbali ya chai iliyoendeshwa na watu mashuhuri, ili kuwaburudisha wakazi na watalii ili wafurahie na kuongeza ufahamu juu ya desturi na mila za mji huo.

Idhaa ya kiswahili 2007-01-22