Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-05 16:40:29    
Jumba la maonesho la Hanyangling

cri

Watalii wa China na wa nchi za nje wakifunga safari kwenye barabara la mwendo kasi kutoka uwanja wa ndege wa Xian kuelekea mjini Xian, njiani wanaweza kuona malundo makubwa mawili ya udongo. Chini ya malundo hayo kuna kaburi la Hanyangling ambalo ni ghala ya hazina ya mabaki ya utamaduni yenye historia ya zaidi ya miaka 2100. Mwezi Machi 2006, Jumba la kwanza la kisasa la maonesho kuhusu kaburi la mfalme la Hanyangling lilifunguliwa, jumba hilo liliwaonesha walimwengu mpangilio mkubwa wa kaburi la mfalme wa Enzi ya Han na mabaki mengi ya kale.

Kaburi la Hanyangling ni kaburi lililozikwa miili ya mfalme Hanjingdi na malkia wake wa Enzi ya Han ya magharibi yenye ustawi mkubwa, kaburi hilo lilijengwa kuanzia mwaka 153 KK. Watafiti wa mambo ya kale wa China walianza kufanya utafutaji na ufukuzi kuanzia miaka ya 90 ya karne iliyopita. Kaburi hilo ni mabaki ya majengo ya kaburi la mfalme na sehemu ya kutambika, ambalo eneo lake lililoshughulikiwa na kuonekana kihalisi ni kubwa kabisa kuliko makaburi mengine yaliyofukuliwa.

Mkuu wa Jumba la maonesho la Hanyangling Bwana Wu Xiaocong alifahamisha kuwa, kaburi la Hanyangling ni ghala kubwa sana la hazina ya utamaduni, kaburi hilo limeonesha hali ya ustawi na neema za enzi ya Han ya magharibi zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Bwana Wu alisema:

Kaburi la Hanyangling ni mabaki ya kale yanayotiliwa maanani zaidi kuhifadhiwa kwenye ngazi ya kitaifa. Mazingira yake ni ya kiasili, kaburi hilo pamoja na eneo zima la kaburi la mfalme wa Han ya magharibi linaweza kuomba kuorodheshwa kuwa mali ya urithi wa utamaduni duniani.

Kaburi la Hanyangling lina eneo la kilomita 20 za mraba, kwenye eneo hilo kuna mashimo zaidi ya 190 ya kuzikwa vitu nje ya kaburi, na katika mashimo 81 kati ya hayo, ambayo yalizunguka kaburi la mfalme yalifukuliwa mabaki ya vinyago vingi vya askari, watumishi wa kasri ya mfalme, maofisa, mifugo na magari ya farasi ya mbao. Jumba la maonesho ya uhifadhi wa mashimo ya kuzikwa vitu nje ya kaburi la mfalme liliojengwa hivi karibuni, ni Jumba la maonesho ya mabaki ya kale lililojengwa chini ya ardhi, ambalo limeonesha kazi ya kisasa kabisa ya uhifadhi wa mabaki ya kale, na pia limeonesha mtizamo wa kisasa kuhusu maonesho.

Jumba hilo lilithibitishwa kuwa mradi wa vielelezo vya uhifadhi na maonesho ya mabaki ya kale ya utamaduni duniani, kwenye Mkutano wa 15 wa mwaka wa Baraza la uhifadhi wa mabaki ya kale duniani. Katika jumba hilo la maonesho, eneo la mabaki ya kale limefungwa kikamilifu, jumba hilo na ukumbi wa watembezi vimetengana kwenye mazingira mawili tofauti, ili mabaki ya kale yaweze kuhifadhiwa vizuri bila matatizo yoyote.

Jumba hilo la maonesho lilijengwa kwa teknolojia ya kisasa duniani yenye hataza kuhusu uhifadhi wa mabaki ya kale, Jumba la maonesho ya mabaki ya kale linatengwa na jumba la watazamaji kwa kupitia kuta za vioo na njia ya vioo, na mazingira ya majumba hayo mawili ni tofauti. Mkuu wa Jumba la maonesho la Hanyangling Bwana Wu Xiaocong alisema:

Baada ya kufunguliwa kwa ukumbi wa maonesho ya kaburi la mfalme, watu wengi wamelisifu Jumba hilo la maonesho kuwa ni jumba la kwanza la kisasa la kuonesha mabaki ya kale chini ya ardhi nchini China.

Katika mazingira yaliyojaa hali ya miujiza, watazamaji wanaweza kuangalia mabaki mengi ya kale kutoka pande mbalimbali, ambapo wanaweza kuona maisha ya aina mbalimbali katika kasri la zamani la kifalme, bali pia wanaweza kufahamishwa mbinu za kisasa za kisayansi na kiteknolojia zinazotumiwa katika utafiti wa mabaki ya kale, pamoja na ufufuzi na uhifadhi wa mabaki hayo ya kale.

Kwenye ukumbi wa maonesho ya kaburi la Hanyangling, kuna vinyago vingi vya wanaume na wanawake wasio na mikono, ambavyo ni nadra kugunduliwa. Vinyago hivyo vya rangi vilipozikwa kwenye kaburi, vilikuwa na mikono ya mbao. Lakini kutokana na kuzikwa chini ya ardhi kwa miaka mingi, vilipofukuliwa, nguo na mikono ya mbao vyote vilioza na kuanguka. Kufukuliwa kwa vinyago hivyo kuliwashangaza sana watu, hata wasomi na wataalamu wengi waliona kwamba thamani ya utafiti wa vinyago hivyo ni kubwa kuliko vinyago vya askari na farasi vilivyofukuliwa kutoka kwenye kaburi la Mfalme Qinshihuang, walisema vinyago hivyo vimeonesha hali ya kupevuka kwa sanaa ya michongo ya China. Wataalam wanaohusika waliona kuwa, vinyago hivyo vilifinywagwa kwa njia ya kulingana na hali halisi, vinyago vyote vilifinywagwa vizuri na sura zake zinapendeza.

Na vingine vingi vya wanyama pia vilifukuliwa kwenye kaburi la Hanyangling, vinyago hivyo vya mbuzi, mbwa mwitu, nguruwe na kadhalika viliunda "dunia ya wanyama chini ya ardhi". Mtaalamu wa mambo ya kale wa Chuo kikuu cha Beijing Bwana Li Li alidhihirisha kuwa, mpaka sasa vinyago hivyo ni vingi kabisa na vinapendeza kabisa kati ya vinyago vilivyofukuliwa nchini China, katika siku zijazo kaburi la Hanyangling litaweza kuwa kiini cha utamaduni wa Enzi ya Han ya magharibi. Alisema:

Tukitupia macho siku za mbele, tunaona ujenzi wa sehemu hiyo utaendelea kufanyika. Kwanza kazi za kufukuliwa kwa mabaki ya kale zitaendelea kufanyika, pia jumba jingine kubwa zaidi la maonesho litajengwa tena, jumba hilo litaonesha mabaki mengi ya kale ya Enzi ya Han ya zama za kale katika sehemu ya Shanxi, ambalo litakuwa kiini cha maonesho ya utamaduni wa Enzi ya Han ya magharibi nchini China.

Kutembelea Kaburi la Hanyangling kunawawezesha watu waelewe moja kwa moja historia ya Enzi ya Han ya zama za kale za China. Mwalimu wa shule ya sekondari ya juu ya utalii ya Xian Duan Jin alisema:

Baada ya kutembelea kaburi hilo, naona kaburi hilo limedumisha utamaduni wa kung'ara wa taifa la China, vitu vingi vya mabaki ya kale vilinishangaza sana. Wakati wa Enzi ya Han ya zama za kale, sanaa ya ufinyanzi wa vinyago, na majengo mengi yaliyojengwa vimefikia kiwango cha juu namna hii, naona taifa la China lina utamaduni wa kung'ara, ni lazima kuuenzi zaidi, na kuwawezesha watu wa nchi mbalimbali wapate nafasi za kutembelea kaburi hilo ili kuelewa historia ya ustaarabu wa China yenye miaka elfu 5.

Idhaa ya kiswahili 2007-02-05