Mahitaji:
doufu gramu 200, nyama ya samaki gramu 20, ute wa yai gramu 15, slesi za kuku gramu 50, kamba mwakaje gramu 20, paja ash la nguruwe gramu 15, uyoga gramu 15, maharagwe gramu 15, vichipukizi vya mianzi gramu 15, chumvi gramu 5, chembechembe za kukoleza ladha gramu 2, mvinyo wa kupikia gramu 25, mchuzi wa soya gramu 15.
Njia :
1. saga nyama ya samaki halafu koroga pamoja na ute wa yai, mvinyo wa kupikia na chumvi. Saga doufu na koroga pamoja na nyama ya samaki. Weka slesi ya nyama ya kuku kwenye sahani halafu weka doufu na nyama ya samaki iliyosagwa kwenye slesi ya nyama ya kuku.
2. pasha moto mimina maji kwenye sufuria na kuweka sahani hiyo kwenye sufuria chemsha kwa mvuke kwa dakika 10, pakua.
3. mimina ute wa yai kwenye doufu, na weka kamba mwakaje paja, ash la nguruwe, uyoga, maharagwe, vichipukizi vya mianzi kwenye doufu, weka kwenye sufuria endelea kuchemsha kwa dakika 5.
4. chemsha maji, mimina mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia, chembechembe za kukoleza ladha, chumvi, korogakoroga baada ya kuchemka, mimina kwenye doufu. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|