Katika mji wa Harbin mkoani Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, wastani wa hali joto kwa miezi mitano ya mwaka ni chini ya nyuzi ya sifuri, ndiyo maana mji huo unaitwa na watu kuwa ni "mji wa barafu". Hali ya baridi imewapa wakazi wa mji huo mawazo mengi yasiyo na kikomo, ambao wameupamba mji wa Harbin kwa barafu na theluji kama dunia iliyosimuliwa kwenye hadithi za mapokezi.
Mji wa Harbin uko kwenye sehemu yenye mwinuko mkubwa, hali joto ya mwanzoni mwa siku za kipupwe hufikia zaidi ya nyuzi 20 chini ya sifuri. Baridi kali inaufanya mji wa Harbin kuwa mji unaopendeza zaidi kwenye majira ya baridi, ambapo mji wa Harbin unafanya juhudi kubwa za kuenzi utamaduni wake wa siku ya barafu na theluji, siku hiyo imekuwa siku ya kimataifa ya barafu na theluji nchini China. Kuanzia mwaka 1985, kila ifikapo tarehe 5 Januari, siku ya barafu na theluji ya Harbin inaanza na kuwakaribisha wageni kutoka sehemu mbalimbali nchini na duniani.
Katika zaidi ya siku 100 za kusherehekea siku ya barafu na theluji mjini Harbin, popote pale mjini Harbin kuna michongo mbalimbali ya barafu, ambapo watu wanaweza kuona michongo ya piano ya barafu, Harry Potter aliyepanda ufagio na watoto wa alama za baraka za Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Michongo hiyo ya barafu, baadhi yao ni ya rangi nyeupe ya wazi, mingine ilitiwa rangi mbalimbali zinazotumiwa katika utengenezaji wa vyakula, na ndani ya michongo mingine zilifungwa taa za rangi mbalimbali, michongo hiyo inametameta chini ya mwanga wa taa wakati wa usiku, ambayo inawavutia sana watazamaji.
Kila ifikapo siku za baridi, maji ya Mto Songhuajiang mjini Harbin huganda kuwa barafu, ambapo eneo la mto huo linakuwa uwanja mkubwa wa barafu, hata sehemu zenye barafu nene magari yanaweza kupita juu yake. Wakazi wa Mji wa Harbin wenye hulka ya usanii huwa wanatoboa barafu, na kutumia mitambo maalum kukata barafu kuwa vipande vyenye maumbo ya aina mbalimbali, na barafu hizo ni nyenzo asilia za kuchonga michongo ya kupendeza.
Mtalii kutoka mkoa wa Guangdong Bwana Huang Zebiao aliyetembelea mji wa Harbin anapenda sana sanaa ya michongo ya barafu, alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, uzuri wa michongo ya barafu unagusa hata kutingisha sana hisia zake. Alisema:
Naona sanaa ya michongo ya barafu imewawezesha watu waingine katika dunia safi isiyo na uchafuzi wowote, nilipoitazama michongo hiyo niliona kama moyo wangu umetakasika kabisa.
Sehemu iliyoko kwenye kando ya kaskazini ya Mto Songhuajiang yenye eneo la mita laki 4 za mraba, ni bustani kubwa kabisa ya barafu na theluji mjini Harbin. Katika bustani hiyo majengo yote ni michongo ya barafu. Kila ifikapo siku ya barafu na theluji, inatolewa kauli mbiu mpya ya bustani hiyo, kwa mfano kauli mbiu ya mwaka huu ni "Urafiki kati ya China na Korea ya kusini ni mkubwa", watalii wanaweza kuona majengo mengi ya michongo ya barafu yaliyo kama majengo ya zama za kale za Korea ya kusini, hata watalii wanaweza kupanda ngazi za barafu za majengo hayo kuangalia mandhari ya mbali kwenye ngazi ya juu. Wakiona uchovu baada ya matembezi, wanaweza kukaa kwenye baa iliyojengwa kwa barafu ndani ya bustani hiyo, ambapo wahudumu wanaweza kuwaletea bia ya Harbin yenye historia ya miaka mia moja.
Mbali na michongo ya barafu, pia kuna michongo ya theluji kwenye Kisiwa cha Jua kwenye kando ya kaskazini ya Mto Songhua. Kwenye kisiwa hicho hali ya hewa ni safi, hakuna uchafuzi mwingi, hivyo theluji inayoanguka huko huwa ni nyeupe sana, hivyo kisiwa hicho kimekuwa sehemu ya kuandaa maonesho ya michongo ya theluji. Mwaka huu michongo mikubwa ya theluji inayoonesha kuwa ni "Maporomoko ya Niagara" imechongwa kwenye bustani hiyo, urefu wa michongo hiyo umefikia mita 250.
Kwa kawaida watu wanaweza kuona kwamba theluji ni ya laini ambayo haiwezi kutumika kwa kuchonga michongo, je, tofauti kati ya michongo ya theluji na michongo ya barafu ni nini? Msanii wa michongo ya theluji wa Harbin Bwana Zhang Yu akifahamisha alisema:
Michongo ya barafu inapendeza kwa hali yake safi, ambayo inaonesha wazi hali ya ndani na pande mbalimbali za michongo hiyo. Na michongo ya theluji inaonesha maumbo ya vitu mbalimbali. Katika mazingira yenye hali joto chini ya nyuzi sifuri, watu wanaweza kuweka theluji ndani ya sanduku moja la karatasi lenye pande nne, wanapoweka ndani theluji wanatumia nguvu kushindilia theluji hiyo, halafu kuondoa sanduku la karatasi, na kuweza kuchonga maumbo mbalimbali.
Wakazi wa Harbin pia wanajua kutumia barafu na theluji kujenga majengo ya burudani. Katika Bustani ya Zhaolin mjini Harbin, kuna jengo moja kubwa la barafu lenye kimo cha mita 60, watu wakitembelea na kuzungukazunguka ndani ya jengo hilo huenda watapotea njia, na wanapaswa kuchukua tahadhari, kwani kila mara wanaweza kuteleza kwenye barafu na huenda wakaanguka. Wakifika kwenye jengo hilo wanapaswa kukaa kwenye ngazi ya kuteleza ya barafu yenye urefu wa zaidi ya mita 10, wakikaa kwenye ngazi hiyo ya barafu kupanda juu, halafu wanaweza kufuata ngazi hiyo ya kuteleza kushuka chini kwa kasi, wakati wanaweza kusikia upepo unavuma vikali, ambapo watajisikia mioyo yao inadunda vikali kama inataka kuruka. Na watembezi wengine hata wanaweza kupanda baiskeli kwenye barafu, baiskeli hizo ni ndogo kuliko zile za kawaida, na gurudumu lake la mbele siyo gurudumu tena bali ni kisu cha barafu, baiskeli hiyo inaweza kuendeshwa kwa kupitia gurudumu lake la nyuma, hata pande mbili za gurudumu lake la nyuma limefungwa bao moja la kuteleza kwenye barafu. Mkazi wa Harbin Bwana Zi Weidong alisema:
Ukipanda baiskeli hiyo kwenye barafu, unaweza kujisikia kama unaruka kwenye barafu, wakati unaposimamisha baiskeli unaweza kujisikia kama unaelea angani.
Mto Songhuajiang mjini Harbin ambao maji yake huganda kila ifikapo siku za baridi, sehemu ya mto huo huwa ni uwanja wa barafu wa burudani. Watalii wanaweza kupanda mkokoteni unaovutwa na mbwa kutembelea kwenye mto huo na kutazama mandhari nzuri ya kando mbili za mto huo, ambapo wanaweza kuona kuwa mashabiki wa kuogelea wa siku za baridi wanaogelea ndani ya mto huo baada ya kutoboa barafu. Mkazi wa Harbin Bibi Han Sumei alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, kuogelea siku za baridi njia nzuri ya kujenga mwili, alisema:
Nimekuwa na umri wa miaka 62, nimeshiriki kwenye mchezo wa kuogelea siku za baridi, kila siku naogelea, hivyo afya yangu ni nzuri sana, hata maumivu fulani ya zamani mwilini mwangu yanatoweka.
Na vilevile mjini Harbin ni sehemu inayofaa kufanya mchezo wa kuteleza kwenye ardhi inayofunikwa na theluji. Mjini Harbin kuna viwanja vingi vya kuteleza theluji, na Uwanja wa Yabuli ni maarufu kabisa miongoni mwa viwanja hivyo, na ni uwanja mkubwa kabisa wa kuteleza kwenye theluji nchini China, ambapo kuna vifaa vya kisasa zaidi vya mchezo huo nchini China.
Idhaa ya kiswahili 2007-02-12
|