Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-16 16:16:25    
Sudan yanufaika zaidi na ushirikiano katika sekta ya nishati kati yake na China

cri

Ushirikiano katika sekta ya nishati kati ya China na Sudan ulioanza katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, ni sehemu moja muhimu ya ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili. Wachunguzi na wachambuzi wa Sudan wameona kwa kauli moja kuwa, ushirikiano wa nishati kati ya China na Sudan umepata mafanikio, na wananchi wa Sudan ndio wananufaika zaidi kutokana na ushirikiano huo.

Mtaalamu maarufu wa mambo ya kidiplomasia wa Sudan Bwana Caral alidhihirisha kuwa, kutokana na kukumbwa na vurugu za kivita minka mingi kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na nchi za magharibi, uchumi wa Sudan ulididimia siku zote. Kutokana na ombi la serikali ya Sudan, serikali ya China iliipatia Sudan misaada ya kifedha, teknolojia na watu wenye ujuzi katika kutafuta na kuzalisha mafuta, na kuiwezesha Sudan ipate ongezeko kubwa katika uzalishaji wa mafuta.

Waziri wa nishati na madini wa Sudan Bwana Awadh Ahmed al-Gaz alisema, ushirikiano katika sekta ya nishati kati ya China na Sudan umepata mafanikio makubwa, kuanzia mwezi Agosti mwaka 1999 Sudan iliposafirisha meli ya kwanza ya mafuta kutoka nchi iliyoagiza mafuta, hali ya Sudan ilibadilika kuwa nchi inayouza mafuta. Mfumo wa uzalishaji mafuta wa Sudan pia umekamilika, hivi sasa shirika la nchi zinazozalisha mafuta duniani OPEC limeanza kuzingatia kuipokea Sudan kuwa nchi mwanachama wa shirika hilo.

Maendeleo makubwa ya uzalishaji mafuta nchini Sudan yamechangia kwanza ustawi wa uchumi wa nchi hiyo. Katika miaka mitano iliyopita, wastani wa ongezeko la pato la taifa la Sudan ulizidi asilimia 8. Ongezeko la uchumi na uboreshaji wa maisha ya wananchi yamehimiza mchakato wa maafikiano ya kisiasa nchini Sudan. Katika miaka miwili iliyopita, serikali ya Sudan kwa nyakati tofauti ilisaini makubaliano ya amani kati yake na makundi mbalimbali ya upinzani yaliyoko katika sehemu ya kusini, magharibi na mashariki ya nchi hiyo, na hali ya kisiasa ya nchi hiyo imetulia hatua kwa hatua. Rais Omar Al Bashir wa nchi hiyo amesema mara kwa mara kuwa, China imeisaidia Sudan kutafuta mafuta na kuchimba mafuta, ambapo uzalishaji wa mafuta umechagia kutimiza amani katika sehemu ya kusini mwa nchi hiyo.

Konsela wa ofisi ya uchumi katika ubalozi wa China nchini Sudan Bw. Hao Hongshe alisema, mafanikio ya ushirikiano katika sekta ya nishati kati ya China na Sudan yanaonekana katika kila upande wa sekta za uchumi na kimaisha nchini Sudan. Kwanza uzalishaji wa mafuta katika visima vitatu vikubwa vya mafuta vilivyojengwa kwa msaada wa makampuni ya mafuta ya China unachukua asilimia kubwa ya uzalishaji mafuta nchini humo. Kiwanda cha kusafisha mafuta ya Khartoum kilichojengwa kwa ushirikiano kati ya China na Sudan mwezi Julai mwaka jana kilimaliza ujenzi wa kipindi cha pili wa mradi wa upanuaji, kiwanda hicho kina uwezo wa kusafisha tani milioni tano za mafuta ghafi kwa mwaka, si kama tu kinaweza kukidhi mahitaji ya mafuta nchini Sudan, bali zinaweza kusafirishwa nje. Zaidi ya hayo, China pia imeisaidia Sudan kuweka mabomba ya kupitisha mafuta na vifaa vingine.

Pili, ushirikiano katika sekta ya nishati kati ya China na Sudan umepanuka hadi kwenye sekta nyingine. Ujenzi wa mradi wa kipindi cha kwanza wa kiwanda cha kuzalisha umeme cha Jieli uliojengwa kwa msaada wa China umekamilika, mradi huo una uwezo wa kuzalisha umeme kilowatt laki mbili kwa mwaka, ambao unachukua robo moja ya vinu vyote vya Sudan vya kuzalisha umeme. Mradi wa kipindi cha pili unaojengwa pia una uwezo wa kuzalisha kilowatt laki mbili za umeme kwa mwaka, baada ya ujenzi wake kukamlika, tatizo la upungufu wa umeme mjini Khartoum litatatuliwa kabisa. Mradi mwingine unaojengwa na wachina ni bwawa Xielovi la litakalohifadhi maji ya mto Nile, ambalo litakapokamilika mwishoni mwa mwaka 2008, litakuwa na uwezo wa kuzalisha kilowatt milioni 1.25 za umeme kwa nguvu ya maji, si kama tu litatatua shida ya upungufu wa umeme kote nchini Sudan, bali pia itaweza kusafirisha umeme nje ya nchi.

Tatu, ushirikiano katika sekta ya nishati kati ya China na Sudan umeongeza nafasi nyingi za ajira kwa wananchi wa Sudan. Hivi sasa watu zaidi ya laki moja wameajiriwa moja kwa moja kutokana na ushirikiano kwenye sekta ya nishati kati ya China na Sudan. Na idadi ya watu wa Sudan walioajiriwa katika shughuli zinazohusiana na uzalishaji mafuta ni kubwa zaidi.

Nne, China inapoisaidia Sudan kutafuta na kuchimba mafuta, pia imesaidia kuwaandaa wasimamizi, mafundi na wafanyakazi, na kuweka msingi mzuri wa watu wenye ujuzi katika kuleta maendeleo endelevu ya uzalishaji wa nishati na madini nchini humo. Zaidi ya hayo, makampuni ya China yamejenga miundo mbinu kama vile barabara, hospitali na vifaa vya kutoa maji ili kuboresha kidhahiri mazingira ya kuishi kwa wakazi wa huko.

Profesa wa idara ya elimu ya jamii ya chuo kikuu cha Khartoum Bwana Said amesema, ushirikiano katika sekta ya nishati kati ya Sudan na China unazinufaisha pande zote mbili, nchi hizo mbili zimejenga uhusiano halisi wa kiwenzi, anaamini kuwa uhusiano huo wa kiwenzi utaendelea kuimarika. Mtaalamu wa elimu ya uchumiSudan Bwana Mahmoud amesema, ushirikiano wa nishati kati ya Sudan na China unaonesha urafiki wa dhati. China inaisaidia Sudan kuendeleza uchumi bila ya masharti, wala kutumia fursa hiyo kuingilia kati mambo ya ndani ya Sudan, na imeweka mfano wa kuigwa katika kuanzisha uhusiano mpya wa kimataifa.

Idhaa ya kiswahili 2007-02-16